Nape, Kadi ya CCJ Ulimrudishia Nani?

Nape, Kadi ya CCJ Ulimrudishia Nani?

Baada ya kuibuka na hoja zisizokuwa na tija kwa taifa inayoashiria CCM kuishiwa na sera, hasa baada ya kumuuliza Dr. Slaa kama alirudisha kadi ya CCM, Mimi kama mwanaharakati huru, napenda kumuuliza Nape Nauye kama aliirudisha kadi yake ya kudumu ya chama cha jamii yaani CCJ ambaye yeye Nape ni Mwanzilishi wake. Kama aliirudisha alimkabidhi nani?

Ikiwa NAPE hajairudisha, basi anatenda kosa la jinai, kwani ni kinyume cha sheria kwa mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti kwa wakati mmoja.....Hoja ujibiwa na Hoja. Nape Tunaomba ujibu hoja. MODS: Please dont remove this thread. Tunaomba Ukweli kwa sababu NAPE ni mmoja wa waanzishili wa CCJ akiwana Mh. Samwel Sita et al.

Hivi kwani CCJ iliwahi kuwa Chama cha kisiasa chenye usajili?
 
Kama anayo ya zamani kama Dr Slaa hakuna haja ya kuchukua mpya.
Kikwete ndani ya CCJ



Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 May 2011

mpendazoe-242.jpg



NYOTA ya spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta imezimwa, MwanaHALISI limeelezwa.
Sitta, ambaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitegemea akibebe katika kugombea urais mwaka 2015, amehusishwa na uasisi wa "chama ndani ya chama."
Hiki ni Chama cha Jamii (CCJ) kilichoanzishwa kwa makeke karibu na uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kikihofiwa kubeba viongozi ndani ya CCM ambao walionekana kupinga ufisadi.
Aliyemwaga hadharani siri za Sitta kuwa nyuma ya ujio wa CCJ, ni Fred Mpendazoe, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wengine aliowataja kuwa ama washiriki au waanzilishi wa CCJ, ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa (CCM), katibu msaidizi wa CCM wilayani Moshi Mjini, Daniel ole Porokwa na kada wa chama hicho, Paul Makonda.
Akiongea kwa kujiamini, Mpendazoe alisema, "Wote hao, ni wasaliti. Wasiwadanganye kuwa wanapambana na ufisadi wakati ni wanafiki wakubwa."
Kwa mpangilio huo, Rais Jakaya Kikwete yumo katikati ya wapinzani wake au waliokuwa wamejiandaa kuwa wapinzani wake wakuu kisiasa.
Pamoja nao, taarifa zinasema kulikuwa na wabunge wapatao 20 ambao wangechomoka CCM pindi chama hicho kingesajiliwa. Gazeti halikuweza kupata orodha yao.
Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika mji wa Njombe, juzi Jumatatu, Mpendazoe alisema, "Sitta ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa CCJ. Mkakati ulikuwa ni kuondoka ndani ya CCM kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010."
Mpendazoe ambaye huongea kwa vituo ili kusisitiza hoja yake, aliuambia umati wa wasikilizaji "…ilikuwa baadaye tuungane na CHADEMA ili kuongeza nguvu ya kupambana na ufisadi na kuuondoa uongozi mbovu wa CCM."
Hata hivyo, Mpendazoe alisema, "Nasikitika sana, mwenzangu huyu (Sitta), alinisaliti dakika za mwisho baada ya kuahidiwa cheo na Kikwete. Ni kwa sababu hawakuwa na dhamira ya dhati. Waliongozwa na uchu wa madaraka."
Kuvuja kwa taarifa za kuwamo kwa Sitta, Dk. Mwakyembe na vigogo wengine waandamizi wa CCM katika mkakati wa kuanzisha CCJ, kulianza kwa Mpendazoe kusema, wiki iliyopita, kuwa Nape alikuwa mwanzilishi wa CCJ.
Kesho yake, Nape alinukuliwa akikubaliana na kauli za Mpendazoe kwa kutokanusha, bali kusema tu kuwa kinachohitajika ni kujadili ya leo na siyo yaliyopita.
Ni mwaka mmoja sasa tangu zipatikane taarifa kwamba baadhi ya vigogo wa CCM wanataka kuunda chama cha siasa.
Kwa mujibu wa taarifa za kishushushu, siri za vigogo kuanzisha chama zilivujishwa na mmoja wa viongozi hao sita.
Hilo lilifuatiwa na mizengwe ya usajili ikiwa ni pamoja na msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa kudai wakati mmoja kuwa hana fedha za kuzunguka nchi kuthibitisha wanachama wa CCJ.
"Hapa, kama Kikwete hakujua hili mapema, lazima atakuwa ameachwa mdomo wazi. Sasa abaki na Sitta ambaye amehusishwa na ujio wa CCJ au abaki na maswahiba zake wa siku nyingi – Edward Lowassa na Rostam Aziz," ameeleza mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kwa sauti ya uchungu.
Sitta alikuwa ameanza kutajwa katika duru za siasa kuwa pekee ndani ya CCM anayetoka eneo lenye wapigakura wengi na anayeweza kuokoa chama hicho kwa msimamo wake.
Spika huyo wa zamani anatoka mkoani Tabora ambako wafuasi wake kwa misingi ya ukaribu, lugha na kuelewana, wanaunda idadi kubwa ya wapigakura kikanda.
Katika mahojiano yake na gazeti hili kwa njia ya simu mara baada ya kumaliza kuhutubia maelfu ya wananchi, Mpendazoe alitaja ushiriki wa kila mmoja kwenye CCJ.
Alisema, "Sitta ndiye alikuwa akilipia pango la ofisi. Alitoa fenicha za ofisi na ndiye alikuwa analipa mishahara ya katibu mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi na mwenyekiti wake, Richard Kiyabo."
Alisema naye Dk. Mwakyembe, ndiye aliandaa katiba ya CCJ. Alikuwa akitoa ushauri wa kisheria kwa wabunge waliokuwa wanataka kuondoka CCM na ndiye alikuwa anashughulikia masuala yote ya fedha kwa maelekezo ya Sitta."
"Hata yule Makonda aliletwa CCJ na Mwakyembe. Walimuachisha shule kule Chuo cha Ushirika Moshi ili kuja kusimamia usajili wa CCJ kabla sisi wengine hatujajitokeza," alisema Mpendazoe kwa sauti ya kusisitiza.
MwanaHALISI halikuweza kumpata Sitta kujibu tuhuma hizo. Simu yake ya mkononi ilitoa jibu, "Simu unayopiga, haipatikani kwa sasa."
Kwa upande wake, Dk. Mwakyembe alisema, "Ninakushauri kwenda kwa msajili wa vyama, kule kuna orodha ya viongozi waasisi, wadhamini na wanachama waanzilishi. Kueni waangalifu, msiwalishe watu porojo za kina Mpendazoe."
Alisema, "…uandishi wa Kitanzania umekuwa wakipuuzi tu. Wewe si unajua kuna msajili wa vyama? Nendeni huko mtaona."
Majibu ya Mwambalaswa hayakutofautiana na yale ya Dk. Mwakyembe, labda pale aliposema, "Wanaoropoka barabarani wanataka kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi, ambayo inakaribia kushinda."
Naye Nape ameelezwa kuwa ndiye alipewa jukumu la kusaidia upatikanaji wa taarifa juu ya mipango ya siri ya CCM dhidi ya Sitta na wenzake. Alipewa pia jukumu la kwenda kwa wafadhiri kuwashawishi ili wasaidie chama hicho.
Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, kabla ya Mpendazoe kujiondoa CCM, kulifanyika majadiliano ya kina na wenzake hao, huku Sitta akimhakikishia kulipwa mafao yake ya ubunge.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, 30 Machi 2010, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, Mpendazoe alisema, ameamua kuondoka CCM kwa kuwa ndani ya chama hicho "kuna kansa ya uongozi."
Alisema, "Sijutii uamuzi wangu huu…kuna wenzangu, muda si mrefu watanifuata."
Alisema, "Chama legelege kinazaa serikali legelege. CCM kimekuwa ngome ya mafisadi na kimebeba watu waliopoteza maadili ya uongozi."
Alimtuhumu mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete, kwa kukosa uwezo wa kusimamia maadili ndani ya chama chake kwa madai kuwa "ameingizwa madarakani na watu wachafu."
MwanaHALISI limetajiwa sababu kuu tatu za kuanzishwa CCJ. Kwanza , ni CCM kuendelea kukosa hadhi mbele ya jamii kwa kukumbatia ufisadi.
Pili, woga kwamba wabunge wapambanaji dhidi ya ufisadi "watafyekwa" wakati wa kura za maoni, hivyo wawe na pa kukimbilia.
Tatu, kusambaa kwa uvumi kwamba Rais Kikwete anataka kumsafisha Edward Lowassa (aliyekuwa waziri mkuu) na kumrejesha madarakani.
Gazeti lilipowasiliana na Paul Makonda juu ya ushiriki wake katika CCJ, haraka alianza kumtuhumu Mpendazoe kuwa amelenga kuwagombanisha na viongozi wakuu wa CCM.
"Anachokifanya sasa Mpendazoe ni kutaka kutugombanisha na viongozi wakuu wa chama chetu. Hebu tujiulize, madhara ya CCJ ni yapi? Hapa tuna vita moja tu: Kumwondoa Lowassa katika chama chetu," alisisitiza.
Kwa kauli hii ya Makonda, waanzilishi wa CCJ walitaka kuondoka CCM ili kujitenga na Lowassa.
Alipoulizwa kama haoni kuwa vita ya kuondoa Lowassa na wenzake ndani ya chama hicho inaweza kuwa ngumu kutokana na kuibuka kwa tuhuma hizi, Makonda alisema, "Ni kweli. Bali lazima tutashinda."
Renatus Muabhi ambaye alikuwa katibu mkuu wa CCJ, alipoulizwa kuhusu madai ya Mpendazoe, kwanza alisita, kisha akasema, "Hayo mambo sijui..."
Alipobanwa juu ya ununuzi wa samani za ofisi na pango la ofisi ya chama hicho, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambavyo Mpendazoe amedai kuwa vilitolewa na Sitta, Muabhi alikiri kuwa ni kweli.
Hata hivyo, Muabhi alisema suala la Sitta kusaidia chama chake halina uhusiano wowote na yeye kuwa ndiye mwenye chama. "Huyu bwana alisaidia kama walivyosaidia wengine. Msaada wake haukuwa na maana kwamba yeye ndiye alikuwa mwenye chama," alisema.
Taarifa zinasema Sitta na wenzake waliamua kuanzisha CCJ kwa hofu kwamba Kamati ya wazee iliyoundwa na chama hicho kutafuta chanzo cha mpasuko ndani ya Bunge na katika chama ingeshindwa kupata suluhu.


 
Watanzania ni watu wa ajabu sana,yaani chama ni kadi? Je mtu akachukua kadi na kwenda fungia maandazi?
 
Kikwete ndani ya CCJ



Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 May 2011

mpendazoe-242.jpg



NYOTA ya spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta imezimwa, MwanaHALISI limeelezwa.
Sitta, ambaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitegemea akibebe katika kugombea urais mwaka 2015, amehusishwa na uasisi wa chama ndani ya chama.
Hiki ni Chama cha Jamii (CCJ) kilichoanzishwa kwa makeke karibu na uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kikihofiwa kubeba viongozi ndani ya CCM ambao walionekana kupinga ufisadi.
Aliyemwaga hadharani siri za Sitta kuwa nyuma ya ujio wa CCJ, ni Fred Mpendazoe, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wengine aliowataja kuwa ama washiriki au waanzilishi wa CCJ, ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa (CCM), katibu msaidizi wa CCM wilayani Moshi Mjini, Daniel ole Porokwa na kada wa chama hicho, Paul Makonda.
Akiongea kwa kujiamini, Mpendazoe alisema, Wote hao, ni wasaliti. Wasiwadanganye kuwa wanapambana na ufisadi wakati ni wanafiki wakubwa.
Kwa mpangilio huo, Rais Jakaya Kikwete yumo katikati ya wapinzani wake au waliokuwa wamejiandaa kuwa wapinzani wake wakuu kisiasa.
Pamoja nao, taarifa zinasema kulikuwa na wabunge wapatao 20 ambao wangechomoka CCM pindi chama hicho kingesajiliwa. Gazeti halikuweza kupata orodha yao.
Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika mji wa Njombe, juzi Jumatatu, Mpendazoe alisema, Sitta ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa CCJ. Mkakati ulikuwa ni kuondoka ndani ya CCM kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Mpendazoe ambaye huongea kwa vituo ili kusisitiza hoja yake, aliuambia umati wa wasikilizaji ilikuwa baadaye tuungane na CHADEMA ili kuongeza nguvu ya kupambana na ufisadi na kuuondoa uongozi mbovu wa CCM.
Hata hivyo, Mpendazoe alisema, Nasikitika sana, mwenzangu huyu (Sitta), alinisaliti dakika za mwisho baada ya kuahidiwa cheo na Kikwete. Ni kwa sababu hawakuwa na dhamira ya dhati. Waliongozwa na uchu wa madaraka.
Kuvuja kwa taarifa za kuwamo kwa Sitta, Dk. Mwakyembe na vigogo wengine waandamizi wa CCM katika mkakati wa kuanzisha CCJ, kulianza kwa Mpendazoe kusema, wiki iliyopita, kuwa Nape alikuwa mwanzilishi wa CCJ.
Kesho yake, Nape alinukuliwa akikubaliana na kauli za Mpendazoe kwa kutokanusha, bali kusema tu kuwa kinachohitajika ni kujadili ya leo na siyo yaliyopita.
Ni mwaka mmoja sasa tangu zipatikane taarifa kwamba baadhi ya vigogo wa CCM wanataka kuunda chama cha siasa.
Kwa mujibu wa taarifa za kishushushu, siri za vigogo kuanzisha chama zilivujishwa na mmoja wa viongozi hao sita.
Hilo lilifuatiwa na mizengwe ya usajili ikiwa ni pamoja na msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa kudai wakati mmoja kuwa hana fedha za kuzunguka nchi kuthibitisha wanachama wa CCJ.
Hapa, kama Kikwete hakujua hili mapema, lazima atakuwa ameachwa mdomo wazi. Sasa abaki na Sitta ambaye amehusishwa na ujio wa CCJ au abaki na maswahiba zake wa siku nyingi  Edward Lowassa na Rostam Aziz, ameeleza mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kwa sauti ya uchungu.
Sitta alikuwa ameanza kutajwa katika duru za siasa kuwa pekee ndani ya CCM anayetoka eneo lenye wapigakura wengi na anayeweza kuokoa chama hicho kwa msimamo wake.
Spika huyo wa zamani anatoka mkoani Tabora ambako wafuasi wake kwa misingi ya ukaribu, lugha na kuelewana, wanaunda idadi kubwa ya wapigakura kikanda.
Katika mahojiano yake na gazeti hili kwa njia ya simu mara baada ya kumaliza kuhutubia maelfu ya wananchi, Mpendazoe alitaja ushiriki wa kila mmoja kwenye CCJ.
Alisema, Sitta ndiye alikuwa akilipia pango la ofisi. Alitoa fenicha za ofisi na ndiye alikuwa analipa mishahara ya katibu mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi na mwenyekiti wake, Richard Kiyabo.
Alisema naye Dk. Mwakyembe, ndiye aliandaa katiba ya CCJ. Alikuwa akitoa ushauri wa kisheria kwa wabunge waliokuwa wanataka kuondoka CCM na ndiye alikuwa anashughulikia masuala yote ya fedha kwa maelekezo ya Sitta.
Hata yule Makonda aliletwa CCJ na Mwakyembe. Walimuachisha shule kule Chuo cha Ushirika Moshi ili kuja kusimamia usajili wa CCJ kabla sisi wengine hatujajitokeza, alisema Mpendazoe kwa sauti ya kusisitiza.
MwanaHALISI halikuweza kumpata Sitta kujibu tuhuma hizo. Simu yake ya mkononi ilitoa jibu, Simu unayopiga, haipatikani kwa sasa.
Kwa upande wake, Dk. Mwakyembe alisema, Ninakushauri kwenda kwa msajili wa vyama, kule kuna orodha ya viongozi waasisi, wadhamini na wanachama waanzilishi. Kueni waangalifu, msiwalishe watu porojo za kina Mpendazoe.
Alisema, uandishi wa Kitanzania umekuwa wakipuuzi tu. Wewe si unajua kuna msajili wa vyama? Nendeni huko mtaona.
Majibu ya Mwambalaswa hayakutofautiana na yale ya Dk. Mwakyembe, labda pale aliposema, Wanaoropoka barabarani wanataka kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi, ambayo inakaribia kushinda.
Naye Nape ameelezwa kuwa ndiye alipewa jukumu la kusaidia upatikanaji wa taarifa juu ya mipango ya siri ya CCM dhidi ya Sitta na wenzake. Alipewa pia jukumu la kwenda kwa wafadhiri kuwashawishi ili wasaidie chama hicho.
Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, kabla ya Mpendazoe kujiondoa CCM, kulifanyika majadiliano ya kina na wenzake hao, huku Sitta akimhakikishia kulipwa mafao yake ya ubunge.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, 30 Machi 2010, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, Mpendazoe alisema, ameamua kuondoka CCM kwa kuwa ndani ya chama hicho kuna kansa ya uongozi.
Alisema, Sijutii uamuzi wangu huukuna wenzangu, muda si mrefu watanifuata.
Alisema, Chama legelege kinazaa serikali legelege. CCM kimekuwa ngome ya mafisadi na kimebeba watu waliopoteza maadili ya uongozi.
Alimtuhumu mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete, kwa kukosa uwezo wa kusimamia maadili ndani ya chama chake kwa madai kuwa ameingizwa madarakani na watu wachafu.
MwanaHALISI limetajiwa sababu kuu tatu za kuanzishwa CCJ. Kwanza , ni CCM kuendelea kukosa hadhi mbele ya jamii kwa kukumbatia ufisadi.
Pili, woga kwamba wabunge wapambanaji dhidi ya ufisadi watafyekwa wakati wa kura za maoni, hivyo wawe na pa kukimbilia.
Tatu, kusambaa kwa uvumi kwamba Rais Kikwete anataka kumsafisha Edward Lowassa (aliyekuwa waziri mkuu) na kumrejesha madarakani.
Gazeti lilipowasiliana na Paul Makonda juu ya ushiriki wake katika CCJ, haraka alianza kumtuhumu Mpendazoe kuwa amelenga kuwagombanisha na viongozi wakuu wa CCM.
Anachokifanya sasa Mpendazoe ni kutaka kutugombanisha na viongozi wakuu wa chama chetu. Hebu tujiulize, madhara ya CCJ ni yapi? Hapa tuna vita moja tu: Kumwondoa Lowassa katika chama chetu, alisisitiza.
Kwa kauli hii ya Makonda, waanzilishi wa CCJ walitaka kuondoka CCM ili kujitenga na Lowassa.
Alipoulizwa kama haoni kuwa vita ya kuondoa Lowassa na wenzake ndani ya chama hicho inaweza kuwa ngumu kutokana na kuibuka kwa tuhuma hizi, Makonda alisema, Ni kweli. Bali lazima tutashinda.
Renatus Muabhi ambaye alikuwa katibu mkuu wa CCJ, alipoulizwa kuhusu madai ya Mpendazoe, kwanza alisita, kisha akasema, Hayo mambo sijui...
Alipobanwa juu ya ununuzi wa samani za ofisi na pango la ofisi ya chama hicho, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambavyo Mpendazoe amedai kuwa vilitolewa na Sitta, Muabhi alikiri kuwa ni kweli.
Hata hivyo, Muabhi alisema suala la Sitta kusaidia chama chake halina uhusiano wowote na yeye kuwa ndiye mwenye chama. Huyu bwana alisaidia kama walivyosaidia wengine. Msaada wake haukuwa na maana kwamba yeye ndiye alikuwa mwenye chama, alisema.
Taarifa zinasema Sitta na wenzake waliamua kuanzisha CCJ kwa hofu kwamba Kamati ya wazee iliyoundwa na chama hicho kutafuta chanzo cha mpasuko ndani ya Bunge na katika chama ingeshindwa kupata suluhu.



R.I.P Mwanahalisi.
 
Naomba na mimi niulize, hivi mtu aliyehama CCM and then baadae akaamua kurudi, anaendelezewa uanachama kwa kadi ya zamani au anaanza na mpya? Naombeni jibu wazee
Ile ya zamani inaendelea, ila analipia ada ambazo hajalipa.
Hivi mtu akiacha kulipa ada je ananyang'anywa kadi?
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana,yaani chama ni kadi? Je mtu akachukua kadi na kwenda fungia maandazi?
Makala ya Mtangazaji – Porokwa


e6faaa817268d28347d2eecce1d2e5dc.jpg

Na editor - Imechapwa 30 May 2011

porokwa-248.jpg



Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimeripoti maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA, Mh. Anthony Komu, kwamba Nape Nnauye alikuwa mwasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ).
Madai haya yakathibitishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ambaye alitaja watu kadhaa nikiwamo mimi, kuwa walishiriki au waanzilishi wa chama hicho ambacho hakikuwahi kufanikiwa kupata usajili wa kudumu.
Hivyo basi, nimewaita hapa leo hii, ili pamoja na mambo mengine, kueleza ukweli wa hiki ambacho kimeelezwa vizuri na Mheshimiwa Mpendazoe na kimenukuliwa vema na vyombo vya habari, hasa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.
Nimeamua kufanya hivyo kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaonyeshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita na tuamini katika hiyo njia tunayoelekea.
Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu, ni kusema ukweli, na kwamba uwongo na fitina ni mwiko kwa viongozi na wachama wa CCM.
Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mh. Nape Nnauye, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe na Mh. Fred Mpendazoe.
Aidha, nilikutana mara moja na Mh. Samwel Sitta baada ya Mh. Nape na Dk. Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza.
Naye Mh. Sitta alinieleza kuwa nilichoelezwa na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe hakina chembe ya mashaka.
Katika mikutano zaidi ya mitano niliyofanya na Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wenzangu walinieleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM kwa hoja kuwa kilipofikia chama hicho hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka ya kuongoza dola.
Walisema CCM hakiaminiki tena machoni mwa wananchi na kimepoteza mvuto mbele ya umma; yote haya ni kwa kuwa chama hiki kimekuwa kinaacha ile misingi ilivyoasisiwa na waasisi wake, kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Walinieleza, kihistoria Chama Cha Mapinduzi ni chama cha ukombozi na kilijipa kazi ya kupigania wanyonge, lakini kikafika mahali historia hiyo ikaporomoka kwa kuingia katika mikono ya watu wasiojali, wasiokuwa na maadili ya uongozi na labda wasiowaaminifu.
Wakati wote wa mazungumzo yetu, Mh. Nape na Dk. Mwakyembe walikuwa wakisisitiza umuhimu wa mimi kukubali kujiunga haraka na CCJ, ili kurahisisha upatikanaji wa usajili wa kudumu wa chama hiki, lengo likiwa CCJ kiweze kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Hata hivyo, kila muda ulivyozidi kusogea, ndivyo nilivyopata kujua undani Mh. Mwakyembe na Mh. Nape wa kutaka kuanzisha chama chao cha siasa, kwamba kinachowasukuma katika mpango huo, ni matakwa binafsi ya kisiasa na hivyo nikaanza taratibu kuwa mbali na mkakati wao.
Nimeamua kuyasema haya baada ya kuwasikia Mh. Nape na Dk. Mwakyembe wakimkana Mh. Mpendazoe na kimsingi wakikana chama chao – CCJ.
Napenda kuwaambia Watanzania, kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa na kuasisiwa na viongozi hao wawili, pamoja na Mh. Sitta kama ambavyo Mpendazoe alivyoeleza.
Katika mpango huu, mimi niliahidiwa kusaidiwa kugombea ubunge katika jimbo la Monduli kupitia CCJ, huku Mh. Nape akiahidi kusimama katika jimbo la Ubungo.
Nimeyasema haya ili kuondoa unafiki unaojengeka ndani ya chama chetu na taifa kwa jumla, kwamba kuna kikundi cha watu wanaotaka kupotosha umma juu ya uanzishwaji wa CCJ na ujio wake ili umma uwapime na uamue juu ya watu hao.
Mimi kama kada wa CCM niliyefundishwa na kuaminishwa kwamba uongozi ni dhamana na ninayeamini katika misingi ile aliyotuachia Mwalimu Nyerere, nimeamua kuyasema haya ili ukweli ubaki ukweli katika historia ya nchi yetu.
Kuyumba kwa chama chetu na hata kufikia hatua ya kuanza kuporomoka kwa kupoteza nafasi mbalimbali kwa vyama vingine kwa wingi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi katika nchi hii, ni kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye malengo na agenda zao binafsi, tofauti na zile za chama chetu.
Hii bila shaka inanipa sababu ya kuamini kwamba Bunge la Tisa kama mmoja wa mihimili muhimu wa dola, chini ya Mh. Samwel Sitta lilitumika vibaya kufanikisha agenda nyingine ya kuanzisha chama kingine badala ya CCM.
Ni vema Rais Jakaya Kikwete akajua kuwa ndani ya timu yake, kuna wachezaji ambao wako tayari kujifunga na kuinyima timu yao ushindi. Ni vema akaamua kuachana nao kwa maslahi yake na chama chetu.
Ni maoni yangu kwa dhati kabisa na rai yangu kwa viongozi wa chama, kwamba ni wakati mwafaka watu kama hawa wawajibike au wawajibishwe kwa matendo yao.
Baada ya mimi kushutukia na kutokuwa na imani na minendo ya waasisi wa CCJ na hivyo kujiondoa, nilipata taarifa kuwa baada ya kujiridhisha kuwa chama chao hakitasajiliwa na kuwahi uchaguzi wa 2010, waliamua kufanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA na kukubaliana kuwa wote kwa pamoja watajiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA ili kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.
Kwa ushahidi ninaoutoa, ninawachukua hawa niliowataja kuwa si wasaliti kwangu tu, bali hata kwa chama chenyewe. Nisingeshutuka mapema yangenipata yaliyompata Mpendazoe. Ninampa pole sana ndugu yangu Fred Mpendazoe.
Na hili la Mpendazoe ambaye alikuwa mbunge, akaacha mishahara kadhaa na mafao yake kwa makubaliano ya kazi ya pamoja ambayo nilishirikishwa katika hatua za awali na mwisho wake wakamtosa na sasa wanamkana hadharani, ni moja ya sababu iliyonisukuma sana kutoa ushuhuda huu.

Mwandishi wa makala haya, Daniel ole Porokwa, kwa sasa ni Katibu wa CCM, wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza. Ni swahiba wa karibu wa Nape Nnauye.


 
Aache unafiki huyo mtoto wa haramu. Nani asiyejua kuwa huyo Nape siyo mtoto wa NNAUYE. NI MTOTO WA MWANDOSYA. SASA ARUDI KWA BABA YAKE. Hata familia ya NNAUYE haimtambui.
 
Kama anayo ya zamani kama Dr Slaa hakuna haja ya kuchukua mpya.

Ritz,
Heshima mbele mkuu, ila naona hata na wewe unakosa hoja za kukuwezesha kumtetea Nepi Nauye. Atujibu kwamba kadi yake ya CCJ aliipeleka wapi
 
muhongo.jpg


WAZIRI wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo


KWA UFUPI

Hata hivyo Profesa Muhongo akizungumza katika kipindi cha ‘Kumepambazuka' cha Radio One Stereo jana alikosoa taarifa hizo huku akisema huo siyo msimamo wa Serikali ya Ujerumani.

WAZIRI wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amewatoa wasiwasi Watanzania kuhusu utafiti na uchimbaji wa madini ya urani huku akiwaponda wanaharakati kwa madai kuwa wanapotosha Umma.

Hivi karibuni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),kiliitaka Serikali kusitisha shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini ya urani, ili kunusuru afya za Watanzania. Pia, Serikali ya Ujerumani kwa kupitia Mtandao wa Uchimbaji wa Madini hayo, iliitaka Serikali ya Tanzania kufikiri na kufanya tathmini ya kina kuhusu madhara ya madini hayo ambayo yanadaiwa kuwa na uwezo wa kuathiri vizazi hadi vizazi.

Hata hivyo Profesa Muhongo akizungumza katika kipindi cha ‘Kumepambazuka' cha Radio One Stereo jana alikosoa taarifa hizo huku akisema huo siyo msimamo wa Serikali ya Ujerumani. Alisema utafutaji na uchimbaji wa madini ya urani, siyo kitu kigeni duniani na kwamba Tanzania siyo nchi ya kwanza kuchimba madini hayo.

"Ndugu zangu Watanzania lazima tufahamu tusiendelee kupotoshwa. Machimbo makubwa kabisa ya urani duniani yako katika nchi ya Kazakhstan, nchi ya pili ni Canada inayotoa zaidi ya asilimia 18, nchi ya tatu ni Australia inayotoa asilimia 11… nchi ya nne ni Namibia,.. wanatoa asilimia 8.4…kama Namibia wanachimba kwa nini Tanzania tusichimbe?" alihoji Profesa Muhongo na kuendelea:

"Nchi ya tano ni Niger inayotoa asilimia 7.8… nchi ya nane ambayo ni muhimu ni Marekani wanatoa asilimia 3.1 ya urani. Nchi ya 10 ni China, nchi ya 11 ni Malawi jirani zetu wanatoa asilimia 1.2 ya urani ya dunia nzima na nchi ya 12 ni Afrika Kusini wanatoa asilimia 1.1. Kwa hiyo tukichukua tu nchi za Afrika, Namibia, Niger, Malawi, South Africa, Malawi wanachimba Tanzania tusichimbe, je, Watanzania tunajua tunachokishabikia?"

Akizungumzia maandalizi ya uchimbaji huo, Profesa Muhongo alisema kuwa kampuni zinazojiandaa kuchimba urani, zimepitia taratibu zote, ikiwa ni pamoja na kupata cheti cha mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, taratibu za mionzi na kupata kibali cha tume ya mazingira.

Kuhusu madhara yaliyotokea nchini Japan mwaka jana baada ya mitambo ya nyuklia kulipuka kutokana na tufani, alisema kuna tofauti kati ya madhara hayo na uchimbaji unaotarajiwa kufanyika nchini.

"Madhara yaliyotokea nchini Japan ni tofauti na uchimbaji unaofanyika hapa. Kule ilikuwa ni Tsunami na matetemeko yaliyovunja nyuklia…ilikuwa ni urani ambayo tayari imeshaanza kutumika," alisema na kuongeza:

Kuhusu taratibu zilizochukuliwa katika uchimbaji huo, Profesa Muhongo alisema taratibu zote za kimataifa zitafuatwa ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira na kupima kiwango cha mionzi na hatari yake wakati wa uchimbaji. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu athari zitakazotokana na uchimbaji wa madini hayo nchini hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Lulu Urio alisema, ingawa kuna faida ambazo taifa litazipata kama fedha za kigeni, bado madhara yanayotokana na uchimbaji wa madini hayo ni makubwa kuliko inavyofikiriwa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Utafiti wa Madhara ya Uchimbaji wa Madini hayo nchini Ujerumani, Gunter Wippel alisema hadi sasa nchi hiyo imetumia zaidi ya Sh7 bilioni kutibu magonjwa na madhara mengine yaliyosababishwa na uchimbaji wa madini hayo.

Mwananchi: Kitaifa - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza




 
Huyu jamaa ndiye tuliambiwa ni kichwa lakini kwa maoni yangu naona ni mtu wa hivyo sana kwa kuthubutu kuudanganya umma wa Watanzania kwamba uchimbaji wa uranium hau na madhara yoyote. Kuna ushahidi wa kutosha kabisa katika nchi nyingi duniani ambako madini hayo yanachimbwa jinsi yalivyoathiri afya za binadamu na mazingira lakini huyu "msomi" wetu anadai kwamba uchimbaji wa madini ya uranium hauna madhara yoyote kwa binadamu!!!!

Huyu jamaa ndiye tuliambiwa kwamba ni "kichwa" anathubutu kuudanganya umma wa Watanzania kwamba uchimbaji wa madini ya Uranium hauna madhara yoyote kwa binadamu. Kuna ushahidi wa kutosha katika nchi nyingi duniani ambako madini hayo ya uranium yanachimbwa jinsi yalivyoathiri binadamu na mazingira, lakini yeye "msomi" wetu anadai kwamba si kweli!!! Anazidi kujishushia hadhi yake ndogo iliyobaki miongoni mwa Watanzania walio wengi.
 
Wakuu ni kweli kuchimba kama kuchimba hakuna madhara hadi itakapobadilishwa kuwa katika muundo mwingine ambapo uhifadhi wake ni mgumu, na hii ndiyo inayoathiri.
Sikumsikiliza alipokuwa akizungumza, muhimu atueleze kama hatua za kuibadilisha kuwa katika hali ya utumiaji itafanyika hapahapa nchini ama la. Ina gharama kubwa kuihifadhi na madhara yake ni makubwa kiafya vizazi kwa vizazi.
 
Nyie CDM vipi nini jema kwenu aaaahhh mnakera sana mnapinga kila kitu
 
Katika maelezo yake sikuona mantiki ya kutumia mifano na asilimia ya uchimbaji ya nchi nyingine. Kilichokuwa kinapingwa ni uchimbaji wa urani kutokana na madhara ya kiafya. Angeishia tu kusema unprocessed uranium haina madhara, kama hilo ndilo utetezi wake.

Hivi kweli tumeona benchmark ni Malawi??? Jamani!!
 
Back
Top Bottom