Nape, Kadi ya CCJ Ulimrudishia Nani?

Nape, Kadi ya CCJ Ulimrudishia Nani?

kwa madini sasa hivi Tanzania yawe na madhara yasiwe nayo hayatusaidii chochote sana sana tunazidi kukaribisha waibaji aka wawekezaji ili waje watuudhi zaidi! madini mengine yametusaidia nini? wezi,utapeli na ubinafsi wa viongozi, tena kwa hilo bora tukatae tu maana hata kama hayana madhara maadamu kuna wasiwasi na wala madini hayatusaidii chochote tumebaki kuwa maskini wa kutupwa bora tupinge labda kweli kuna madhara! dhahabu watu wanachimba wanabeba wanapeleka ulaya sisi tunaishia kuwa manamba tu kwenye migodi,hata historia ya kina chifu mangunga haitusaidii chochote kujifunza tunafanya yaleyale tu.

Mara gesi nyingi imegunduliwa mimi binafsi nilishakata tamaa wala hata sifuatilii tena maana najua haitusaidii kitu watanzania tulio wengi sana sana tutaishia kufukuzwa maeneo tunayo kaa kupisha miradi ya wizi tu. Kilichobaki sasa ni kupigania uhuru upya ili kuikomboa nchi yetu maana hatuko huru tena na hata police nao maskini wenzetu ndiyo wanaotumiwa kutugandamiza wamelewa sifa za kuitwa vyombo vya dola huku maisha yao na wao ya hovyo kama nini,ila hao ndiyo number moja kuwamaliza maskini wenzao!
 
MKUU ukishajiunga kwenye uongozi wa Serikali ya MAGAMBA lazima uwe ZEZETA (zombie)hata kama wewe Profesa

Inaniuma sana moyoni kwa sababu nilimwamini. Inasikiisha kama ameshaambukizwa ugonjwa wa sisiemu.

Hivi haiwezekani sheria ikatungwa kwa viongozi wa kitaifa kulazimishwa kusema kweli? Hii imekuwa too much sasa
 
Hivi mtu Akiingia kwenye siasa anatunza akili zake na kujivika usiasa kwa kila jambo! Maajabu
 
Huyu jamaa ndiye tuliambiwa ni kichwa lakini kwa maoni yangu naona ni mtu wa hivyo sana kwa kuthubutu kuudanganya umma wa Watanzania kwamba uchimbaji wa uranium hau na madhara yoyote. Kuna ushahidi wa kutosha kabisa katika nchi nyingi duniani ambako madini hayo yanachimbwa jinsi yalivyoathiri afya za binadamu na mazingira lakini huyu "msomi" wetu anadai kwamba uchimbaji wa madini ya uranium hauna madhara yoyote kwa binadamu!!!! Huyu jamaa ndiye tuliambiwa kwamba ni "kichwa" anathubutu kuudanganya umma wa Watanzania kwamba uchimbaji wa madini ya Uranium hauna madhara yoyote kwa binadamu. Kuna ushahidi wa kutosha katika nchi nyingi duniani ambako madini hayo ya uranium yanachimbwa jinsi yalivyoathiri binadamu na mazingira, lakini yeye "msomi" wetu anadai kwamba si kweli!!! Anazidi kujishushia hadhi yake ndogo iliyobaki miongoni mwa Watanzania walio wengi.
ndugu BAK, Huyu Muhongu ananitia kichefuchefu anaposema wanajiandaa kuchimba! Hapa Namtumbo mkoani Ruvuma, wazungu wameanza kuchimba na kuzomba Uranium zaidi ya miaka minne kwa sasa!? Hawa mawaziri ni Vipofu au!!? Tumeshuhudia na tunashuhudia kwa macho yetu wala siyo stori! Kila kitu hapa tz wanakifanyia mzahamzaha tu! Mtatumaliza watz jamani! Jalini afya zetu, acheni kuchumia matumbo yenu tu!! Ee Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
 
Wakuu ni kweli kuchimba kama kuchimba hakuna madhara hadi itakapobadilishwa kuwa katika muundo mwingine ambapo uhifadhi wake ni mgumu, na hii ndiyo inayoathiri.
Sikumsikiliza alipokuwa akizungumza, muhimu atueleze kama hatua za kuibadilisha kuwa katika hali ya utumiaji itafanyika hapahapa nchini ama la. Ina gharama kubwa kuihifadhi na madhara yake ni makubwa kiafya vizazi kwa vizazi.

Mkuu tatizo si uranium bali mionzi (radiation) inayotiokana na decay schemes za uranium mfano radon, thorium, etc.
Tusiwe viziwi kwa maneno ya wanasiasa. Uranium ni hatari kwa afya za watanzania wote hata katika hatua za uchimbaji, na usafirishaji. Wanasiasa including political organ Tanzania atomic energy agency hawataki kuwaambia ukweli watanzania. Mfano, madhara makubwa ya uranium ni kansa, kifo na genetic mutations. Tukianza na tatizo kubwa la kansa litakalokwenda kudhihirika miaka michache; je tuna hospital za kutosha za matibabu ya kansa kwa kutumia mionzi ya Co-60 au Lina? au je tumeandaa personnels wakutosha katika matibabu ya kansa. Tukiangalia usalama wa wachimbaji na wakazi wa vijiji vya mgombasi, seluu, na vijiji vingine vinavyozunguka eneo la mgodi, je serikali imeandaa wataalamu wakutosha ( wenye taaluma za radiation protection) ili kuchunguza viwango vya mionzi katika maji, vyakula, mimea,wanyama. Uchimbaji na urutubishaji wa uranium unapingwa karibu dunia nzima mf Japan, German, etc kwani the risks outweigh the benefits.

Mwisho: Prof Muhongo ni injinia tu wa miamba, hajui kitu chochote kuhusu madhara ya uranium wa maisha ya viumbe hai
 
mheshimiwa waziri angetusaidia zaidi kama angeeleza tija ambayo zimepata nchi kama malawi na Niger. taarifa za magazeti mengi na hata kwenye youtube zinaonyesha uchumi wa Malawi unategemea zaidi zao la tumbaku kuliko madini na huko niger wamebakia kuambulia murahaba kiduchu kutoka kampuni ya ufaransa wakati wakizidi kudidimia kwenye dwimbwi la umasikini, uharibufu mkubwa wa mazingira na matatizo ya kiafya vinavyosababishwa na vumbi la urani. Waziri hajatoa majibu ya maswali haya ya msingi badala yake anataka watanzania wasiwe na wasiwasi. Vigezo gani anavitumia kuondoa wasiwasi huo?
 
Acha kuropoka mkuu, wewe una fani gani hapo ulipo mpaka humuelewi, hawafanani wanaojua na wasiojua, huyu ni profesa inahitaji watu walio makini kumuelewa na wenye nia ya kweli kumfahamu. Kwa nini nyie munapenda kushobokea wana harakati koko? Hawa wanatafuta ugali tu tanzania hawana kazi ya kufanya kwa hiyo lazima waonekane kama wapo. Waziri kaingia juzi tu munaanza kumchimba, hoo! Jiuzulu, ohh mtkataba wa mafuta, ohh, ooh sijui, ooh yaani ni upumbafu tu, usipomuamini msomi wa taifa lako utamuamini nani? Yaani ni fitna tuu kisa waziri ni ccm. Acheni mambo hayo! Hata kutia sukari kwa wingi kwenye chai au mafuta mengi kwenye msosi ni hatari kwa afya yako. Tuna mabingwa na wataalamu wa nyukilia na ambao wameshafanya kazi nje kwa muda mrefu na sasa wapo hapa wanatumikia taifa na wapo kimya hawana papara. Kama huwajui bora nikutajie japo mmoja nae makamu wa rais mohammed gharib bilal (kichwa hicho baba usione mvi nyingi- baradei wa tanzania). Malawi nchi ya juzi tu inachimba uranium, why we? Chimba hakuna kurudi nyuma waache wapige domo subirini serikali yenu ya scout, musituletee majungu na fitna si mtaji!
 
Kwa mawaziri haina madhara kwasababu wao wanatibiwa ulaya, hata babu yao alifia ulaya.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Muhongo atujibu haya:-
"kuna wasomi wangapi wazawa wenye weledi wa kutathmini kinachofanywa na hao jamaa?"
"Kuna vifaa vingapi Tanzania vyenye uwezo wa kutambua mtawanyiko/au uchafuzi wa hayo madini kwenye uso wa ardhi wakti na baada ya uchimbaji au utafiti? [equipments that will detect any contamination of such radioactive to the environments]"
 
Tatizo ni Je huyo anaesimamia taratibu zote anafanya hivyo?.Je taratibu zote tunazijua?.

Je nani atasimamia taratibu za uathiri wa mazingira?. Well, kama hazitafuatwa nini kitafanyika?.

Wakaguzi wa hiyo kitu watakaa mjini na watakao pata madhara ni ndugu zenu!

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Maelezo ya kizembe kama ya huyu anayeitwa profesa yanatufanya wa-Tz tueleweke kama wanyama wa serengeti. Mtu anaulizwa juu ya madhala yeye anaibuka na list za nchi zinazochimba au kuzalisha uranium. Huyu jamaa zinamtosha kweli?

Huko kwenye chama chao tena ndo kabisa! Nadhani wao wanadhani wamepata bonanza sasa ni kujitahidi kuchimba, wafaidi kabla ya kuondoka madarakani.
 
Acha kuropoka mkuu, wewe una fani gani hapo ulipo mpaka humuelewi, hawafanani wanaojua na wasiojua, huyu ni profesa inahitaji watu walio makini kumuelewa na wenye nia ya kweli kumfahamu. Kwa nini nyie munapenda kushobokea wana harakati koko? Hawa wanatafuta ugali tu tanzania hawana kazi ya kufanya kwa hiyo lazima waonekane kama wapo. Waziri kaingia juzi tu munaanza kumchimba, hoo! Jiuzulu, ohh mtkataba wa mafuta, ohh, ooh sijui, ooh yaani ni upumbafu tu, usipomuamini msomi wa taifa lako utamuamini nani? Yaani ni fitna tuu kisa waziri ni ccm. Acheni mambo hayo! Hata kutia sukari kwa wingi kwenye chai au mafuta mengi kwenye msosi ni hatari kwa afya yako. Tuna mabingwa na wataalamu wa nyukilia na ambao wameshafanya kazi nje kwa muda mrefu na sasa wapo hapa wanatumikia taifa na wapo kimya hawana papara. Kama huwajui bora nikutajie japo mmoja nae makamu wa rais mohammed gharib bilal (kichwa hicho baba usione mvi nyingi- baradei wa tanzania). Malawi nchi ya juzi tu inachimba uranium, why we? Chimba hakuna kurudi nyuma waache wapige domo subirini serikali yenu ya scout, musituletee majungu na fitna si mtaji!
Yaani watu hawawezi kumuelewa profesa! kwa nini? Mbona wanamuelewa Mungu?

Huyu jamaa kweli kuna mazuri kayatenda na hasa kuzuiya upuuzi wa Tanesco. Lakini sasa naona kuna tatizo kwamba hawezi kumeza sifa. Baada ya kusifiwa kwa hilo la tanesco sasa kalewa kabisa! Amekuwa ndiye msomi pekee nchini anayejua madini, anayejua mazingira, anayejua uranium, ...... huo ni upuuzi.

Si vizuri kuamini kwamba eti profesa ni mtu wa maana sana kama unavyotaka kuaminisha wasomaji. Ktk watu wa maana dunia hii ni wangapi ni maprofesa? U-profesa hauongezi busara. Huyu Muhongo unayemsema ni mzembe hata wa kupanga na kuchagua maneno ya kusema hadhalani. kumbuka maneno ambayo amekuwa akiyatumia bungeni.
 
Kama tutatumia teknolojia ya kisasa ya uchimbaji na uhifadhi pia matumizi sahihi ya urani, hakuna madhara

Swali: je tumejipanga sawia ?

The answer is ............NO. Hatujajipanga, ni bakshishi atakayopewa kwa kufanikisha uchimbaji huo ndiyo inamfanya aongee hivyo. Hivyo ndivyo walivyo viongozi wetu wa serikali yetu ya sasa hivi, maslahi yao binafsi kwanza maslahi ya nchi na wananchi later or never.
 
Ur are the ONE MUONGO MKUBWA...!!!

Quickly clear-up ur poor mind then u will understand what Prof. meant...!!!

Mining Uranium has no effects untill u start processing it...!!
and then processed uranium needs high storage standard to avoid leakage....!!!

So who told you URANIUM WILL BE PROCESSED HERE..!!

Umekurupuka ww....!! Prof. ni msomi wa kimataifa. Huwezi mpuuza, kumdharau, ww ndio VUVUZELA....
just to assure u he is right 100%, for what he said....

Most arrogant people usually fall in FEAR OF UNKNOWN...

Some also use their little IQ to lie public to get their attention of which we know....!!!

Stop looking for cheap popularity through Muhongo...!!! umetumwa ww....!!!

Shikamoo Profesa Muhongo...
 
Mkuu hiyo hatari ya madhara ya uranium ni hadi inaporutubishwa kwa mchakato wa kisayansi ikichanganywa na vitu vingine, uchimbaji hauna madhara mkuu. Futa kauli yako kwamba kadanganya, kasema ukweli!
Ni kweli mkuu , Uranium ore in its natural state haina madhara yanayoonekana mpaka ianze kuwa concentrated.
Kuna processes nyingine za hospitalini ambazo ni hatari zaidi kuliko naturaly mined Uranium ore.

Kitu cha maana ni kujua safe handling ya madini haya.
Vile vile kuna madini mengi tu ambayo yako naturally radioactive.
 
Wakuu ni kweli kuchimba kama kuchimba hakuna madhara hadi itakapobadilishwa kuwa katika muundo mwingine ambapo uhifadhi wake ni mgumu, na hii ndiyo inayoathiri.
Sikumsikiliza alipokuwa akizungumza, muhimu atueleze kama hatua za kuibadilisha kuwa katika hali ya utumiaji itafanyika hapahapa nchini ama la. Ina gharama kubwa kuihifadhi na madhara yake ni makubwa kiafya vizazi kwa vizazi.

Kwa kuzingatia hapo kwenye red Tufafanulie kifungu cha mwisho kweye hiyo post nakirudia hapa chini:

[Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Utafiti wa Madhara ya Uchimbaji wa Madini hayo nchini Ujerumani, Gunter Wippel alisema hadi sasa nchi hiyo imetumia zaidi ya Sh7 bilioni kutibu magonjwa na madhara mengine yaliyosababishwa na uchimbaji wa madini hayo]

Kwanza ujue elements nyingi sana unaweza kuzifanya zikawa radioactive, sema energy utakayotumia itakua kubwa sana.

Ukija kwenye uranium wanayoiongelea hapo ni ile ambayo ni very easy kuifanya ianze kutoa mionzi. Na kutokana na conditions zilizopo sehemu husika uranium inaweza ikawa tayari imesha kuwa forced kutema kwa kiwango fulani, na hicho kiwango kinaweza kikawa ni tosha kabisa kumdhuru binadamu.

Sasa hao wajerumani wametumia pesa hiyo kwa ajili ya madhara, Je na sisi tukiachwa peke yetu tutatumia kiasi gani? je tunazo? na kama tunazo zinamsaidia mlalahoi au mlala-starehe? je ni wepi wengi walalahoi au walalastarehe?

Na ukizingatia kuna sehemu nchini mwetu hata panadol watu hawapati, hii itakuwa ni hatari.

Tutafika huko kwenye kuchimba, lakini kwa sasa hivi hapana.
 
Huyu waziri namheshimu sana, ila alipothubutu kuwaambia watanzania mgao wa umeme tanzania utakuwa historia,huku akijua hakuna chembe ya ukweli ya maneno yake, nilijua kakurupuka, sitoshangaa kama hili nalo kakurupuka.
 
Kama tutatumia teknolojia ya kisasa ya uchimbaji na uhifadhi pia matumizi sahihi ya urani, hakuna madhara

Swali: je tumejipanga sawia ?

wacheni kujidanganya nyie watu wanosafiri kwenda mwezini wanshindwa na hilo seuze nyie omba omba binafsi naomaba Mungu kama leo serekali ianze hiyo kazi .
 
Waogope wanasiasa kama Ukoma. Kwa bahati mbaya, madhara yatakapo kuja kutokea kwa vizazi vijavyo, hawa wanaotuingiza matatani hawatakuwepo, vinginevyo tungewasuta bila kuwa na msaada. Wanasiasa ni wanyama, wakiona pesa tu, mate yanawadondoka. Yawe na madhara, yasiwe na madhara, tuachane nayo. Kama tumeshindwa kuingia mikataba yenye tija kwenye madini mengine, iweje uranium ???????????
 
Nyie CDM vipi nini jema kwenu aaaahhh mnakera sana mnapinga kila kitu

Hao wanaharakati waliotoa hayo matamko ni CDM? usiwe na akili za kuazimwa fikiri kwanza, lakini kwa upande wa pili naweza kukushukuru umefahamu kuwa CDM kinapenda afya na uhai wa watanzania na ndo maana wote unaoona wanapinga juu ya suala hili la uchimbaji wa Urani wa kukurupuka kwa serikali yetu(CCM) kuwa ni CDM.
 
Back
Top Bottom