Tafadhali mkuu, Niliposema mi ni mtaalamu sikumaanisha kwamba najifunza kama profesa wetu Muhongo au nahitaji internet kuyajuwa haya. Nilikuongoza uangalie uhusiano wa Uranium na gesi ya radon. Naona wewe unanirudisha kwenye mawe yenye traces za uranium. nini kinatokea baada ya kuyabeba mawe hayo? Hapo ndo tunaonyesha tofauti zetu. Hebu jiulize mazingira ya machimbo ya uranium. Kitu ambacho hujakiangalia ni Mtiririko ktk machimbo. Unakuwa hivi; Uranium 238 >>Radium 226 >>Radon 222 (+alpha particle). Radon ni gesi. Unaivuta ikiwa ni 'pure' na wala hutasubiri ku-concentrate uranium ili upate madhala. Ukizubaa tena Radon 222 >>Polonium 218 (+alpha particle). Muulize Muhongo atawaweka wapi wananchi maskini wanaouzunguka mgodi ktk nchi ambayo hata mabomu ya Mbagala na G'ngolamboto hayatunziki. Hatuhitaji mifano ya malawi na kote africa, huenda hawana cha kuuza kingine. Mbona hata dhahabu haileti faida kwetu?