Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

Imefika wakati viongozi wa Chadema wawajibike kwa vifo vinavyotokea katika maandamano yao kwa sababu wao ndio wanasababisha na wanakuwa wanafahamu kuwa mtu atafariki, Kifo cha Mwangosi Iringa kabla tukio halijatokea Mwandishi Francis Godwin alimuuliza Dr Slaa kwamba kwa nini wanaenda kufanya Mkutano wakati wamezuiliwa kufanya Mkutano Dr slaa alieleza Liwalo na Liwale na yuko tayari kupoteza Maisha ya Mtanzania yeyote ili kuimarisha Chama.
Hivi kwa nn Dr Slaa asiuzulu pamoja na Mwenyeki kama kweli wana nia ya dhati na Watanzania?
Kwa maneno aliyoyatoa ilikuwa ni lazima nguvu itumike kwa Sababu CDM Wakivunja Sheria wasiposhughulikiwa wanasema Serikali ya CCM dhaifu Sasa ili isiwe dhaifu lazima kila mmoja aheshimu sheria na anayevunja achukuliwe Hatua na ninamweleza IGP Na RPC Lazima muuendelee kulinda sheria kila mmoja aheshimu anayebisha ashughulikiwe...

Halafu Dr Alikuwepo Nyololo mbona alipoanzisha fujo tu hatukujua kaelekea wapi au ni Mkakati wa Chadema kuua watanzania wameagizwa na Wafadhili wao?

Kweli nimeamin kikao cha Chadema hakina Tofauti na kikao cha ukoo...Kikao cha Ukoo kinaweza kubadilika kuwa Kikao cha Chama

huna akili hata kidogo. mkutano wa bubuhu Zanzibar ulifuata sheria? naona unatumia masaburi.
 
Imefika wakati viongozi wa Chadema wawajibike kwa vifo vinavyotokea katika maandamano yao kwa sababu wao ndio wanasababisha na wanakuwa wanafahamu kuwa mtu atafariki, Kifo cha Mwangosi Iringa kabla tukio halijatokea Mwandishi Francis Godwin alimuuliza Dr Slaa kwamba kwa nini wanaenda kufanya Mkutano wakati wamezuiliwa kufanya Mkutano Dr slaa alieleza Liwalo na Liwjale na yuko tayari kupoteza Maisha ya Mtanzania yeyote ili kuimarisha Chama.
Hivi kwa nn Dr Slaa asiuzulu pamoja na Mwenyeki kama kweli wana nia ya dhati na Watanzania?
Kwa maneno aliyoyatoa ilikuwa ni lazima nguvu itumike kwa Sababu CDM Wakivunja Sheria wasiposhughulikiwa wanasema Serikali ya CCM dhaifu Sasa ili isiwe dhaifu lazima kila mmoja aheshimu sheria na anayevunja achukuliwe Hatua na ninamweleza IGP Na RPC Lazima muuendelee kulinda sheria kila mmoja aheshimu anayebisha ashughulikiwe...

Halafu Dr Alikuwepo Nyololo mbona alipoanzisha fujo tu hatukujua kaelekea wapi au ni Mkakati wa Chadema kuua watanzania wameagizwa na Wafadhili wao?

Kweli nimeamin kikao cha Chadema hakina Tofauti na kikao cha ukoo...Kikao cha Ukoo kinaweza kubadilika kuwa Kikao cha Chama
Unamfanana yule mwenye mkorogo,nakuhakikishia
umesamehewa dhambi zako,nenda kwa amani kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu, Amina.
 
Codom,..Dr Slaa alizungumza hakuna mtu aliyetegemea kama kifo kingetokea ila inaonyesha ni Agenda ya Chadema kuua watanzania ili Chama kiendelee kupewa Misaada na baadhi ya Mataifa ya nje,,
Na hakuna mtu asiyejua mkoani Iringa kuwa Mwangosi alikuwa Chadema na mda mwingine alikuwa anavaa na Magwanda ndio maana Mchangiaji mmoja alisema inawezekana Chadema walimpa Bomu akajilipue kwa Police akakosea Masharti

kumbe alikua chadema damudamu.tunawaita waandishichadema.
Alichanganya ukereketwa na kazi na matokeo ndo haya.
Wandishi muwe makini sana kutoegemea upande mmoja kisiasa.
 
........Dr slaa alieleza Liwalo na Liwale na yuko tayari kupoteza Maisha ya Mtanzania yeyote ili kuimarisha Chama.
Mkuu una hakika kama Dr. Slaa aliyatamka haya kwa kinywa chake? Nadhani hili neno linatakiwa kujibiwa na Dr manake hii ni hatari. Kama ni uongo basi ni uongo hatari sana na kama ni kweli basi ni ukweli hatari sana. Sijui kama tumefikia hatua ya kupoteza maisha ya watu kwa kuimarisha chama.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwajibika kutokana na kuwepo kwa matukio ya watu kupoteza maisha yanayosababishwa na maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wafuasi wake.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Chadema wana kila sababu ya kuwajibika, kwa sababu matukio haya ya mauaji yamekuwa yakitokea kwenye operesheni za mikutano yao na matukio ya aina hii kutokea katika kazi za chama cha siasa ni aibu, hivyo viongozi wa kisiasa wanaokutwa na matukio hayo ni lazima wawajibike kwa umma, lakini matukio haya yamekuwa yakitokea bila wao kuwajibika,” alisema Nape na kuongeza:

“Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.”

Alisema CCM inaungana na wanaCCM na wananchi wote kulaani mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu.

“Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine,” alisema Nape.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema CCM imetoa mwito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza kwa umakini na weledi mauaji ya Mwangosi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.

“Pamoja na mwito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba
uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo,” alisema Nape na kuongeza:

“Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na Chadema nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombovya ulinzi na usalama.”

Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni la kuuawa kwa kada wa CCM mkoani Singida, kuuawa kwa Ali Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Mwangosi, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine yalitokea wakati viongozi wa Chadema wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Nape alisema matukio hayo si mazuri kutokea kwenye shughuli za chama cha siasa kwa madai ni aibu kwa
wanachama wake na wananchi kwa ujumla na hivyo kupoteza sifa ya kuitwa chama chema cha siasa.

(Source: Habari Leo 6th september 2012)
Kweli Tanzania ina viongozi hadi wananuka kuliko mavi. Why can't he just shut his mouth? We are so sick of his nonsense!
 
Awajibike pia na Maandamano ya Maustaadh leo

Jibu hoja ya mleta hoja.,usijitungie swali jepesi ambalo halijaulizwa mkuu. BTW,maandamano ya waislam yamefanyika kwa amani bila kumbughudhi mtu yeyote,bila uvunjifu wa amani. Kama una taarifa za vurugu yoyote iliyosababishwa na waislam tujuze! Hata CDM wangekua wanafata taratibu,kuomba kibali kuandamana,kuendesha mikutano ya hadhara na kuheshimu maagizo ya vyombo vya dola(usalama) nk hakuna tatizo.

Sijasita kuamini mauaji yanayotokea kwenye mikutano na maandamano ya chadema yanasababishwa na chadema na viongozi wake,haswa Slaa.

Kwa msg hii,bado namuona huyu mtu kama muuaji!
"Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague"
 
Crazy movements are endless in JF,tell your chairman J.K that things has fallen apart!
 
Imefika wakati viongozi wa Chadema wawajibike kwa vifo vinavyotokea katika maandamano yao kwa sababu wao ndio wanasababisha na wanakuwa wanafahamu kuwa mtu atafariki, Kifo cha Mwangosi Iringa kabla tukio halijatokea Mwandishi Francis Godwin alimuuliza Dr Slaa kwamba kwa nini wanaenda kufanya Mkutano wakati wamezuiliwa kufanya Mkutano Dr slaa alieleza Liwalo na Liwale na yuko tayari kupoteza Maisha ya Mtanzania yeyote ili kuimarisha Chama.
Hivi kwa nn Dr Slaa asiuzulu pamoja na Mwenyeki kama kweli wana nia ya dhati na Watanzania?
Kwa maneno aliyoyatoa ilikuwa ni lazima nguvu itumike kwa Sababu CDM Wakivunja Sheria wasiposhughulikiwa wanasema Serikali ya CCM dhaifu Sasa ili isiwe dhaifu lazima kila mmoja aheshimu sheria na anayevunja achukuliwe Hatua na ninamweleza IGP Na RPC Lazima muuendelee kulinda sheria kila mmoja aheshimu anayebisha ashughulikiwe...

Halafu Dr Alikuwepo Nyololo mbona alipoanzisha fujo tu hatukujua kaelekea wapi au ni Mkakati wa Chadema kuua watanzania wameagizwa na Wafadhili wao?

Kweli nimeamin kikao cha Chadema hakina Tofauti na kikao cha ukoo...Kikao cha Ukoo kinaweza kubadilika kuwa Kikao cha Chama
We mleta mada unajiona uko salama sana sio? Hawa poilisi waliouwa hawana macho kesho sii ajabu wakakutungua wewe. Andika kitu chenye sense na ukome kuandika ujinga hapa. Ninakuhakikishia Tanzania itakombolewa na itarudia heshima yake one of this days. Time will tell! Udhalimu hauwezi kushinda haki na ukweli.
 
Nape, i know you read the comments as number of times you posted too,.... brother, don't let your love for your political party (CCM), cripple your sense of reasoning..
 
Masikini weeee!! Inasikitisha sana kuona kijana mwenzetu kama Nape Nnauye anakubali kutumiwa mithili ya kondomu na wanasiasa wa CCM bila ya yeye mwenyewe kujiambua anatumika ndivyo sivyo. Yeye anawalaumu Chadema kwa mauaji ya Mwangosi na Polisisiemu wamewashikilia askari watano waliohusika na mauaji yale, tumsikilize nani tumuache nani.
 
Kweli ajira Tanzania hii ni mgogoro, yaani Nape na shule yake hiyo ya India kaona ni bora akalie kiti hicho huku akiendelea kuwadanganya watanzania akifikiri wanadangayika karne hii!!!
Hizi santuri zako siku moja zitakuletea matatizo sana......husijesema kuwa hukuonywa.
 
Ni kweli anapaswa kuwajibika, kwani kila sehemu.. kila jamii, kila nchi ina sheria na taratibu...Na ni lazima zifuatwe... Chama kisichokuwa na nidhamu ya kufuata sheria ni hatari kuongoza nchi.... Hakifai hata siku moja......NA HILI NI JAMBO HATARI ZAIDI KATIKA KUJENGA JAMII YA KISTAARABU. Mnahamasisha uvunjaji wa sheria na taratibu matokeo yake watu masikini wanaumia, wanakufa na kuacha familia zao yatima ...Viongozi waanzilishi wa uvunjaji sheria na taratibu wanakimbia wazima bila kudhurika .... Inasikitisha Maswala ya siasa ni kuyaangalia kwa mbali kabisa.......
 
Jibu hoja ya mleta hoja.,usijitungie swali jepesi ambalo halijaulizwa mkuu. BTW,maandamano ya waislam yamefanyika kwa amani bila kumbughudhi mtu yeyote,bila uvunjifu wa amani. Kama una taarifa za vurugu yoyote iliyosababishwa na waislam tujuze! Hata CDM wangekua wanafata taratibu,kuomba kibali kuandamana,kuendesha mikutano ya hadhara na kuheshimu maagizo ya vyombo vya dola(usalama) nk hakuna tatizo.

Sijasita kuamini mauaji yanayotokea kwenye mikutano na maandamano ya chadema yanasababishwa na chadema na viongozi wake,haswa Slaa.

Kwa msg hii,bado namuona huyu mtu kama muuaji!
"Wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha maana mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague"
Vp Nyie jana, Mlikuwa na kibali cha Maandamano au Ndo wavunjaji wa sheria Namba one, Bahati yenu Mkwer3 ana wa intetain na udini wake na wenu, zingekuwa enzi za Ben Mngeisoma namba jana
 
.
Kwa hiyo mtu akivunja sheria Tz anapigwa bomu au risasi ya kichwa on the sport?
Naona bado upo katika ndoto za Tz ya '47
.
Mkuu hujanisoma vizur, Hawa Magamba kila linalotokea Balaaa tu, lawama wanasukumia kwa CDM/Dr Slaa, thats why nasema, kwa la Jana, waseme pia Maustaadh walitumwa na Dr Slaa pia, hope utakuwa umenisoma nad if so, Gonga like
 
Jimy P. pengine sijakuelewa au na wewew pia hujanielewa. Hapa tunazungumzia kifo cha mwandishi wa habari wa Channel 10 Daudi Mwangosi Iringa Nyololo. Unaposema Dr. Slaa achukuliwe hatua za kisheria una maana kuwa Dr. Slaa ndiye aliyeua? Unaposema wananchi wakivunja sheria wachukuliwe hatua, wanachi wachukuliwe hatua ya kisheria ipi, wauwawe? Mwenye kutoa hukumu ya kifo kwa wananchi wanaotuhumiwa kuvunja sheria awe polisi au nani? Jimy, unasema una wasiwasi Chadema walimpa Bomu akalilipue kwa Police. Chadema walimpa nani? Walimpa police au Dr. Slaa? Chadema hawawezi kumpa bomu polisi Bomu na huwezi kutenganisha kati ya Chadema na Dr. Slaa kwa kuw yeye ( Dr. Slaa) ndiye Katibu Mkuu wa Chadema hivyo ndiye mtendaji mkuu. Labda useme alitengeneza bomu na kwenda kulilipua polisi. Lakini Bomu halikulipuliwa polisi lilipuliwa kwenye ofisi za Chadema Nyololo. Naona tunazungumza vitu tofauti ni kama vile usiku na mchana visivyoweza kukutana
 
Vp Nyie jana, Mlikuwa na kibali cha Maandamano au Ndo wavunjaji wa sheria Namba one, Bahati yenu Mkwer3 ana wa intetain na udini wake na wenu, zingekuwa enzi za Ben Mngeisoma namba jana

Lete hoja acha porojo..
 
Bado siamini na huwezi kuushawishi umma wa watanzania kuwa kama maandamano hayana kibali cha kuandamana suluhu yake ni kuua waandamanaji. Kibali ni karatasi tu kamwe hakiwezi kuwa mbadala wa UHAI wa mtu. Itawezekana tu kwa watawala wakatili ambao madaraka yanathamani kuliko watawaliwa. Watawala wa aina hii wanamabavu hawana hekima. Farao aliwahi kusema. Viongozi wanapaswa kuwa watu wenye Hekima mwiungoni wa jamii, lakini wanaoweza kuwatambua watu wenye Hekima ni wale wenye Hekima pia. Watu wenye Hekima katika jamii yoyote ile ni wachache kulinganisha na wasio na Hekima.
Kama ndani ya serikali yetu viongozi wote wanaamini kuwa suluhu ya maandamano bila kibali ni KUWAUA, basi ni kosa la demokrasi inayosema wengi wape. Mfumo wa uteuzi wa uraisi ndani ya vyama vyetu umeshindwa kuona watu wenye hekima ndani ya jamii. Uliangalia mtu anayekubalika na sio mtu mwenye sifa za uongozi (mwenye hekima.)
Mfalme Sulemani, aliwapima wanawake wawili, waliokuwa wanagombania mtoto. Akasema '' tumkate huyu mtoto vipande viwili ili kila mmoja wenu achukue kipande. Mama mmoja akasema 'basi bora mimi nikose, mwenzangu achukue ili mradi mtoto awe hai'. Mfalme Sulemani akamkabidhi mtoto mama aliyekubali kukosa akathamini uhai.
Kiongozi anayekubali watu wake wafe kwa sababu ya kuonyesha madaraka aliyonayo analinda karatasi kuliko uhai ni kiongozi MWEHU, asingefaa kufikiriwa kwa nafasi yoyote ya uongozi. Uongozi ni maamuzi and there is nothing dangerous than uncriticized wrong decision. Viongozi wasiotaka kusikia la mtu hata kama wameamua vibaya ni hatari kuwapa madaraka kwa kuwa wakiwa nayo ni janga kwa Taifa, kama hivi Leo Dr. Ulimboka, kesho Daudi Mwangosi kesho kutwa mtu mwingine. Serikali bado haioni aibu inanyanyuka kujitetea.
Hata ingalikuwa serikali haihusiki moja kwa moja lakini ina wajibu wa kuwalinda raia wake. Kama haiwalindi inashindwa kutimiza wajibu wake wa msingi. Serikali inayowajibika kwa wananchi ilipaswa kuomba radhi kwa wananchi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake sio kusingizia Dr. Slaa. Kama ni Dr. Slaa alikuwa na nia ya KUUA watu alipaswa kudhibitiwa kabla hajaua. Kusema Dr Slaa alisema hiki, alisema kile bila kuonyesha hatua za kuzuia ni upuuzi. Dr. Slaa hayupo juu ya serikali wala hana wajibu kuwalinda raia wa Tanzania na wala hana kiapo hicho
 
Back
Top Bottom