CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwajibika kutokana na kuwepo kwa matukio ya watu kupoteza maisha yanayosababishwa na maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wafuasi wake. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Chadema wana kila sababu ya kuwajibika, kwa sababu matukio haya ya mauaji yamekuwa yakitokea kwenye operesheni za mikutano yao na matukio ya aina hii kutokea katika kazi za chama cha siasa ni aibu, hivyo viongozi wa kisiasa wanaokutwa na matukio hayo ni lazima wawajibike kwa umma, lakini matukio haya yamekuwa yakitokea bila wao kuwajibika, alisema Nape na kuongeza:
Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake.
Alisema CCM inaungana na wanaCCM na wananchi wote kulaani mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu.
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao. CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine, alisema Nape.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema CCM imetoa mwito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa
kuchunguza kwa umakini na weledi mauaji ya Mwangosi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.
Pamoja na mwito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba
uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo, alisema Nape na kuongeza:
Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na Chadema nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombovya ulinzi na usalama.
Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni la kuuawa kwa kada wa CCM mkoani Singida, kuuawa kwa Ali Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Mwangosi, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine yalitokea wakati viongozi wa Chadema wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.
Nape alisema matukio hayo si mazuri kutokea kwenye shughuli za chama cha siasa kwa madai ni aibu kwa
wanachama wake na wananchi kwa ujumla na hivyo kupoteza sifa ya kuitwa chama chema cha siasa.(Source: Habari Leo 6th september 2012)
Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine.
Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
Huyu bwana mdogo ni mpumbavu na hajui asemacho. Ila nguvu ya umma itamfundisha muda si mrefu.
huyu anachojua ni kujipaka mkorogo-carolite tuu!NAPE hao watu wameuliwa na polisi au chadema?polisi ipo chini ya ccm au?
Kwa kauli hii ya Nape naanza kuamini kauli za kuwa haya mauaji kwenye mikutano ya chadema yanapangwa na CCM, ili tu watupe lawama kwa chadema. Lakini wamechelewa sana mpango wao umestukiwa.
masters ya kuimba taarabu kaipatia Mombasa.
Tatizo la watu wa CDM ni uhodari wa kutusi wengine wanapokuja na hoja wasizozipenda. Shame on u