Nape: CHADEMA iwajibike matukio ya mauaji

Huyu kweli ni KATIBU MWENEZI.............. bila polisi kutumia nguvu na kuziacha akili mahabusu, hayo mauaji yangelitoka vipi...............? inamaana hata lile liaskari lililoshika ile bunduki akimuelekeza marehemu mwangosi huyu nape ndo tuseme picha zile hajaziona na ukatibu wake....................?
 
nani analeta stress tena huku...kuna watu nikiona majina yao humu,natokaga nje kuvuta sigara...woyiii...enda kule!
 
Nepi safi sana hawa jamaa wawajibike na ujinga wao na tendwa aharakishe mchakato wa kukifutilia mbali na kuzuia wanachama wake kushiriki siasa miaka 50
 
Slaa niwakunyongwa kwa kusababisha yote haya.Kama umeshindwa kufuata Amri za kanisa za serikali hata ziweza Kweli huyu mtu ni zaidi ya Nduli
 
Sijapata kuona katibu mwenezi mwongo na asiyemkweli kama huyu jamaa. Hivi jaribu kufikilia katika mazingira haya ambayo dunia nzima imeona kupitia picha namna polisi walivyoua kwa uwazi na ukatili mkubwa, lakini bado mtu mwenye roho ya chuma Nape nnauye anataka kusingizia CDM. Mungu mkubwa kwani kila kitu kinachofanyika ukweli unawekwa wazi.Sijui wakina nape watajifichia wapi.
 
Kwanini walimpa jina baya hili la NEPI LAMANI?
MATOKEO NDIO HAYA HADI LEO ANAVAA NEPI, AKIKUA ATAACHA
 
Huyu kweli ni KATIBU MWENEZI.............. bila polisi kutumia nguvu na kuziacha akili mahabusu, hayo mauaji yangelitoka vipi...............? inamaana hata lile liaskari lililoshika ile bunduki akimuelekeza marehemu mwangosi huyu nape ndo tuseme picha zile hajaziona na ukatibu wake....................?

Slaa niwakunyongwa kwa kusababisha yote haya.Kama umeshindwa kufuata Amri za kanisa za serikali hata ziweza Kweli huyu mtu ni zaidi ya Nduli

Kitendo cha polisi kuua raia ni kinyume cha sheria.


Polisi walichemsha, na wana kesi ya kujibu.
Polisi hawana kinga ya kuwaruhusu kuua kwa visingizio vyepesi.

Nape analifahamu hilo na anataka awatoe watu kwenye point muhimu. Na hapa nanukuu sheria.

Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20 ibara ya 21
21.-(1) Afisa polisi au mtu mwingine hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kutumia nguvu zaidi au kuvunja utu wa mtu huyo zaidi ya ilivyo lazima kufanikisha ukamataji au kumzuia utorokaji wa mtu baada ya kukamatwa.
(2) Bila kupunguza matumizi ya kifungu kidogo cha (1), afisa polisi hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kufanya kitendo kinachoweza kusababisha kifo kwa mtu huyo, isipokuwa kama afisa polisi anaamini kwa sababu za msingi kwamba kufanya kitendo hicho ni muhimu katika kulinda maisha au kuzuia madhara makubwa kwa mtu mwingine.


Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 4 ibara ya 18B.-
(1) Katika kutumia haki ya kujilinda mwenyewe au kumtetea mtu mwingine au kutetea mali, mtu atatakiwa tu kutumia nguvu za kiasi zinazostahili ulinzi husika.

(2) Mtu atawajibika kuwa ametenda kosa la jinai kwa kosa lolote litakalotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda au anapomlinda mtu mwingine au anapolinda mali.
(3) Mtu yeyote atakayesababisha kifo cha mtu mwingine kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda, anakuwa ametenda kosa la kuua bila kukusudia.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwajibika kutokana na kuwepo kwa matukio ya watu kupoteza maisha yanayosababishwa na maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wafuasi wake.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Chadema wana kila sababu ya kuwajibika, kwa sababu matukio haya ya mauaji yamekuwa yakitokea kwenye operesheni za mikutano yao na matukio ya aina hii kutokea katika kazi za chama cha siasa ni aibu, hivyo viongozi wa kisiasa wanaokutwa na matukio hayo ni lazima wawajibike kwa umma, lakini matukio haya yamekuwa yakitokea bila wao kuwajibika," alisema Nape na kuongeza:

"Inapotokea shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri wa aina yake."

Alisema CCM inaungana na wanaCCM na wananchi wote kulaani mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu.

"Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao.CCM inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine," alisema Nape.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema CCM imetoa mwito kwa vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza kwa umakini na weledi mauaji ya Mwangosi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.

"Pamoja na mwito wetu wa kuchunguzwa suala hili kwa umakini na weledi mkubwa, pia tunatoa rai kwamba
uchunguzi huu ufanyike kwa kutumia muda mfupi ili ukweli uweze kubainika mapema na hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo," alisema Nape na kuongeza:

"Vilevile CCM inasikitishwa sana na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na Chadema nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombovya ulinzi na usalama."

Aliyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni la kuuawa kwa kada wa CCM mkoani Singida, kuuawa kwa Ali Hassan mjini Morogoro, kuuawa kwa Mwangosi, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na matukio mengine yalitokea wakati viongozi wa Chadema wakiendesha operesheni zao mbalimbali nchini.

Nape alisema matukio hayo si mazuri kutokea kwenye shughuli za chama cha siasa kwa madai ni aibu kwa
wanachama wake na wananchi kwa ujumla na hivyo kupoteza sifa ya kuitwa chama chema cha siasa.

(Source: Habari Leo 6th september 2012)
 
Back
Top Bottom