Nape apiga muziki kwa heshima ya Dr. Slaa

Nape apiga muziki kwa heshima ya Dr. Slaa

Tunajua hamjui Baba yake mzazi ni yupi.unaonaje tumwite hivi NAPE W P SLAA.ili amwite Baba.

Acha hizo bana, mbona aliwahi sema humu "baba yangu Jeetu Patel" !?? au alikuwa anatania kama kawaida yake!??
 
Sijawahi kumuona Dr. Slaa akisocialize nje ya majukwaa ya siasa!!!

KIZURI hujiuza!
KIBAYA hujitembeza!
Mnataka a-socialize ili mmtafutie kisa cha kumbakizia kesi?!
Dr. SLAA hana haja ya kujitembeza....
 
Nape kabla hujahamia cdm ni lazima utueleze kwa nini mliamua kuua watu Arusha ?
 
hivi nape si anamiaka mingapi? Maana najua atakuwa na zaidi ya 35 kwa sasa, dr je? Nadhani wamepishana na kikwete si zaidi ya miaka 2.

Je anaweza kumuita babu kikwete?
Je kikwete anaweza kuwa na mjukuu wa umri wa nape?

mi naona nape kapunguza umri wake kisha hiyo miaka aliyopunguza akamuongezea slaa. Hata babake nape wa kufikia alikuwa mzee kwa slaa nijuavyo mimi, sasa iweje mtu mdogo kuliko baba yako awe babu yako!
 
Hivi Nape si anamiaka mingapi? Maana najua atakuwa na zaidi ya 35 kwa sasa, Dr je? Nadhani wamepishana na Kikwete si zaidi ya Miaka 2.

Je anaweza kumuita Babu Kikwete?
Je Kikwete anaweza kuwa na Mjukuu wa umri wa Nape?

Mimi nilishampa orodha ya mababu zake na mabibi ndani ya CCM ili asihangaike kutafuta nje. Mababu: Jakaya Kikwete, Mohamed G. Bilali, Kingunge N. Mwilu, Steven Wassira, Samwel Sitta, John S. Malecela, Yusuph Makamba, Mizengwe Pinda, Edward Lowassa Ally H. Mwinyi, Ben Mkapa nk. Mabibi: Anne Makinda, Anna Abdalah, Anne Mkapa nk. Nape apewe msaada wa kujua familia yake maana anahangaika kutafuta mbadala. Wanaojua asili yake wamsaidie!
 
Nimekuwepo leo jioni kwenye live band pale Rayol Village mjini Dodoma ambapo baada ya burudani kadhaa aliitwa Bwana Nape kupiga nyimbo mbili alipopanda jukwaani akashika gitaa la rithym alipolipiga kidogo akasema atapiga nyimbo mbili moja kwa ajili ya " dadaake Phillipe mbunge viti maalum Chadema" ambaye alikuwepo ukumbini na kisha akapiga wimbo wa pili kwa heshima ya "babu yangu na kipenzi changu Dr. Slaa"

Akasema anapiga kwa heshima yao katika kutambua mchango wao kwenye kujenga demokrasia na kuthibitisha kuwa siasa sio ugomvi bali ni hoja!

Imekaaje hii wakuu?

Hapa kama Nape anang'ata na kupuliza.
 
Siasa za Tanzania kaaaaazi kweli kweli.
Ingekuwa mbele ningeelewa fasta sana. Ila hapa kwenye mifereji ya maji taka, dah siasa sio kabisa.
Enewei, was just saying
 
Back
Top Bottom