Siku nyingi nimekuwa najiuliza, hivi chama hivi sasa hakina mtu wa mikakati na propaganda??, nasema hivi kwa sababu, hatua ambayo CCM wanafanya ya kutaka kujibu MAPIGO kila CDM wanapofanya shughuli zao, inaonyesha kwa kiasi kikubwa anakosa kina. ni cheap kwa kushangaza. Napenda kuwauliza walioandaa mkutano huu wa juzi, kwa nini walikurupuka? kwa nini wametumia agenda ya kupambana na Chadema? lakini kubwa zaidi ni hili la kukusanya kadi feki. Hii inanikumbusha kisa cha mbuni na kuficha kichwa wakati mwili wote uko nje. CCM nawashauri kubadilisha mikakati na hasa kutumia wataalaumu wanaoweza kusoma mazingira/hali na kuitafsiri katika mkakati]
Nimeshindwa kuelewa kama chama kikongwe kama CCM wanaweza fanya upuuzi wa kiwango hiki cha kuwabambika watu wenye kadi mpya na nyingi hazijaandikwa chochote kabisa eti ionekane wanachama wa vyama vya upinzani wamerudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.
Picha hii ambayo ipo pia kwenye blog ya bwana michuzi inadhihirisha uhuni waliofanya kuwahadaa Watanzania.
View attachment 56011