CCM inatekeleza sera za CHADEMA-Dr SLAA, Kinana, Nape Wazomewa Sumbawanga!

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,057
309
• KINANA, NAPE WAZOMEWA SUMBAWANGA na Mwandishi wetu,

Karagwe CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kinafurahi kuona kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatekeleza sera walizozianzisha wao. Wakati CHADEMA wakijivunia CCM kutumia sera zao, hali si shwari kwa mahasimu wao hao baada ya Katibu Mkuu wake mpya, Abdullahman Kinana, pamoja na wajumbe wenzake wa Sekretarieti kukumbana na zomeazomea mjini Sumbawanga jana.

Kauli ya CHADEMA ilitolewa na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, wakati akifungua rasmi Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kagera ambalo linaundwa na viongozi kutoka katika kila jimbo la mkoa huo, linalofanyika kwa muda wa siku tatu katika wilaya ya Karagwe. Dk. Slaa alisema CHADEMA waliwezesha kufutwa kwa kodi za manyanyaso katika wilaya ya Karatu baada ya kulikalia kidete suala hilo, na ndipo CCM ilitumia sera hiyo na kuondoa kodi za namna hiyo takriban nchi nzima.

Aliongeza kuwa walianzisha pia sera ya kujenga zahanati kila kata wilayani Karatu, ambayo nayo CCM baadaye ilichukua na kisha kutangaza kuanzisha utaratibu wa kujenga zahanati kila kata nchi nzima. "Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010, CHADEMA tuliahidi sera ya kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi nchi nzima kama tungeingia madarakani.

Wakati huo CCM ilidai haiwezekani ila sasa nao wametangaza kupunguza gharama za bidhaa hizo," alisema. Alifafanua ni wazi kuwa CCM ikiweza kutekeleza sera ya CHADEMA ya kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi na kutoa elimu bure kabla ya mwaka 2015, watafurahi maana hawana wivu, lakini wakishindwa itakuwa ndiyo njia yao ya kuondoka madarakani.

Dk. Slaa aliongeza kuwa CHADEMA haiwezi kuchukia kutokana na CCM kutekeleza sera zake maana zinapotekelezwa wananchi wanapata mabadiliko na unafuu wa maisha. Alisema kuwa kelele zao zinahitaji uchumi wa nchi usimamiwe vizuri na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wote, na kwamba mpaka sasa inashangaza kuona CCM imeshindwa kupata majibu yanayosababisha wananchi kuendelea kuwa maskini.

Dk. Slaa alichanganua kuwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliweza kuanzisha viwanda ambavyo sasa vingi vimefungwa, bila kuchimba dhahabu na wala kuuza samaki nje ya nchi, lakini akahoji ni kwa nini wakati huu ambao tunauza madini, samaki nje ya nchi maendeleo yamedumaa.

"Mfano Waingereza hawana mashamba makubwa lakini hata siku moja hawakuwahi kulia njaa. Sisi Tanzania tuna mabonde makubwa ambayo yakitumiwa ipasavyo mawili yanaweza kutosha kulisha nchi nzima, lakini bado tunalia njaa," alisema. Alibainisha kuwa kutokana na kutokuwa na mpangilio mzuri, mawazo mgando yaliyopo hayawezi kuleta maendeleo. Alitolea mfano kuwa inashangaza kuona bado tuna treni inayosafiri siku tatu kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Katibu huyo aliwataka viongozi wa chama hicho kutoogopa kukemea maovu yanayofanywa na baadhi ya viongozi walioko madarakani na kwamba kiongozi bora lazima aonyeshe madadiliko katika eneo lake.

Alisema CHADEMA iko katika harakati za kuboresha na kuimarisha utendaji kazi wa ndani kwa kununua pikipiki kila kata nchi nzima, kuajiri makatibu na kutafuta ofisi za kudumu na zenye hadhi. CCM wazomewa Mjini Sumbawanga mambo yalikuwa magumu kwa viongozi wapya wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wao, Kinana, baada ya kukumbana na zomeazomea ya wananchi kwenye mkutano wake.

Kinana aliingia mjini humo jana kwa ndege akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Organizesheni Seif Khatib na Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwandri, na kisha kwenda eneo la Isesa kufanya mkutano. Kwa kuwa eneo hilo ni ngome kuu ya CHADEMA, viongozi hao walianza kuzomewa na hivyo wakati wakiondoka wafuasi wao waling'oa bendera na mlingoti kwenye shina la wapinzani wao na hivyo kuzidisha chuki.

Wakiwa katika mkutano wao wa ndani, uliibuka mzozo mkubwa baina ya viongozi na waendesha bodaboda waliokuwa wamekodishwa kubeba bendera kwa ujira wa kujaziwa mafuta na sh 10,000.

"Walitaka kuwageuka vijana wale ambao kimsngi wengi wao si wafuasi wao kwa kuwalipa sh 2,000 badala ya 10,000 lakini baadaye walilazimika kuwalipa kulingana na makubaliano," kilisema chanzo chetu. Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana mimba.

Hata Mwanri naye alipata wakati mgumu wakati akitoa ufafanuzi wake na hata Mkuu wa Mkoa, Stella Manyanya, alipoitwa na Kinana afafanue naye alizomewa hatua iliyomfanya Katibu huyo kutumia busara ya hali ya juu kuwatuliza wananchi na mkutano ukamalizika.

Source:Tanzania daima
 
hii ni picha mojawapo toka Karagwe kwenye mkutano ulioanza leo
 

Attachments

  • Conchesta akifungua kikao.JPG
    Conchesta akifungua kikao.JPG
    414.6 KB · Views: 1,296
Chama Cha Majangili kinapata tabu sana safari hii.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Slaa amesahau kuwaambia wananchi pia kwamba hata mchakato wa katiba mpya ni sera ya CHADEMA. CCM hawakuwahi kabisa kuwa na hilo wazo la kuandikwa katiba mpya.
Lakini kwenye zomea zomea ya CCM natamani vyombo vingi vya habari viandike haya. Ili kuwaamusha wananchi wa mikoa mingine pia kufanya hivyohivyo. Kama itatokea hiyo, basi naamini CCM watachanganyikiwa sana, na watatambua kwamba nchi si mali yao bali ni ya wananchi wa Tanzania.
 
Magazeti ya bongo bana.

Sijui yataondokana lini na huu msingi wake wa bora habari kuliko habari bora.

Inawezekana viongozi wa CCM walizomewa lakini gazeti linapoanza kutoa habari na kunukuu 'kilisema chanzo chetu' na bila kukitaja, kwa msingi wa uandishi wa habari, habari hiyo inakuwa imetiwa doa. Reliable sources mara zote huwa zinatajwa na kwa kutokufanya hivyo, habari inakuwa kama ya kuokota vijiweni.

Siyo kitu cha kushangaza hata mambo yetu mengine yanafanyika kwa ovyo ovyo.
 
Kauli kama hiyo kwenye rangi nyekundu ilikuwa ya lazima kutolewa na Nape? Busara iko wapi kwa viongozi kama hawa? Ina maana wenye mimba ndo wana tabia za kuzomea? Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana.

• mambo yalikuwa magumu kwa viongozi wapya wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wao, Kinana, baada ya kukumbana na zomeazomea ya wananchi kwenye mkutano wake. Kinana aliingia mjini humo jana kwa ndege akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Organizesheni Seif Khatib na Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwandri, na kisha kwenda eneo la Isesa kufanya mkutano. Kwa kuwa eneo hilo ni ngome kuu ya CHADEMA, viongozi hao walianza kuzomewa na hivyo wakati wakiondoka wafuasi wao waling'oa bendera na mlingoti kwenye shina la wapinzani wao na hivyo kuzidisha chuki. Wakiwa katika mkutano wao wa ndani, uliibuka mzozo mkubwa baina ya viongozi na waendesha bodaboda waliokuwa wamekodishwa kubeba bendera kwa ujira wa kujaziwa mafuta na sh 10,000. "Walitaka kuwageuka vijana wale ambao kimsingi wengi wao si wafuasi wao kwa kuwalipa sh 2,000 badala ya 10,000 lakini baadaye walilazimika kuwalipa kulingana na makubaliano," kilisema chanzo chetu.

Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana mimba. Hata Mwanri naye alipata wakati mgumu wakati akitoa ufafanuzi wake na hata Mkuu wa Mkoa, Stella Manyanya, alipoitwa na Kinana afafanue naye alizomewa hatua iliyomfanya Katibu huyo kutumia busara ya hali ya juu kuwatuliza wananchi na mkutano ukamalizika.
 
Slaa amesahau kuwaambia
wananchi pia kwamba hata mchakato wa katiba mpya ni sera ya CHADEMA. CCM
hawakuwahi kabisa kuwa na hilo wazo la kuandikwa katiba mpya.
Lakini kwenye zomea zomea ya CCM natamani vyombo vingi vya habari
viandike haya. Ili kuwaamusha wananchi wa mikoa mingine pia kufanya
hivyohivyo. Kama itatokea hiyo, basi naamini CCM watachanganyikiwa sana,
na watatambua kwamba nchi si mali yao bali ni ya wananchi wa
Tanzania.

mtawalipa watu kuzomea sana lakini mwisho wa siku wananchi wataona juhudi za CCM katika kuisimamia serikali
 
Magazeti ya bongo bana.

Sijui yataondokana lini na huu msingi wake wa bora habari kuliko habari bora.

Inawezekana viongozi wa CCM walizomewa lakini gazeti linapoanza kutoa habari na kunukuu 'kilisema chanzo chetu' na bila kukitaja, kwa msingi wa uandishi wa habari, habari hiyo inakuwa imetiwa doa. Reliable sources mara zote huwa zinatajwa na kwa kutokufanya hivyo, habari inakuwa kama ya kuokota vijiweni.

Siyo kitu cha kushangaza hata mambo yetu mengine yanafanyika kwa ovyo ovyo.

kweli mkuu nani anaweza zomea chama kubwa,bado kinapendwa usipime jipe moyo hizo ni propaganda za chadema i think. Ha ha haa nafwa
 
Hizi ziara za Jangili Kinana hazina faida yoyote kwa chama, serikali au wananchi, zaidi ni kwamba zinakichafua chama tu.
 
kweli mkuu nani anaweza zomea chama kubwa,bado kinapendwa usipime jipe moyo hizo ni propaganda za chadema i think. Ha ha haa nafwa
CCM ni chama kubwa kilichojaa mazezeta tupu, Kila anachosema JK wao wanameza, ipo siku JK atawaambia mwende kwa wananchi na kuvua nguo na bado mtafanya tu.
 
Cha Mtema Kuni Watakiona, Wamechelewa na ni mbwa mwitu walivaa ngozi ya kondoo. Waangalieni kisha wazomeeni.
 
ccm wanajaribu kupiga promo nzito kwa kinana na Nape ili angalau wajaribu kuamsha wananchi kurudi upande wao..na kwa kweli hili ni jaribio la mwisho kwao kujaribu kujiweka vizuri kabla ya uchaguzi unaokuja, vinginevyo, kama juhudi hazitafanikiwa kuna kishindo kizito cha kuanguka kinawanyemelea
 
Kauli kama hiyo kwenye rangi nyekundu ilikuwa ya lazima kutolewa na Nape? Busara iko wapi kwa viongozi kama hawa? Ina maana wenye mimba ndo wana tabia za kuzomea? Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sana.

Unatarajia kinywa kilichojaa kinyesi kitoe harufu gani? Mkuu, na huyu ni moja ya mategemeo ya CCM. Nape asipotukana hapati usingizi. Kwake yeye busara ni matusi.
 
mtawalipa watu kuzomea sana lakini mwisho wa siku wananchi wataona juhudi za CCM katika kuisimamia serikali

iiishi! CCM si ndo serikali? Kikwete, Shein si ndo wenyeviti. Iiiishi, we mzima kweli?
 
mtawalipa watu kuzomea sana lakini mwisho wa siku wananchi wataona juhudi za CCM katika kuisimamia serikali
Hivi kwa uhalisia wa mambo inahitaji kumlipa mtu ili awazomee viongozi hawa wa mafisadi? Mwananchi wa kawaida ambaye kila kukicha maisha yake yanaongezewa ugumu kwa mfuko wa bei akiona wadanganyaji wanazidi kudanganya unadhani atafanya nini? Watanzania ni wastaarabu sana. Ilikuwa haki kuchukua hatua ya juu kuzidi ile ya kuzomea tu. Inabidi kila waendapo wazomewe!
 
CCM ni chama kubwa kilichojaa mazezeta tupu, Kila anachosema JK wao wanameza, ipo siku JK atawaambia mwende kwa wananchi na kuvua nguo na bado mtafanya tu.

it's ironic mwenye akili timamu hawezi penda magamba read between the line
 
Back
Top Bottom