Katibu mkuu wa itikadi na uenezi wa CCM, NAPE Hnauye amesema kuwa kumekuwepo na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari polisi na WAnanchi katika mji wa MAKAMBAKO na maeneo mengine huku nape akiwasihi watanzania wanaoishi maeneo ambayo CHADEMA watafanya maandamano kuchukua tahadhari.
Source: Mtanzania la leo 2/6/2013
ccm acheni utoto, wananchi msitufanye watoto wasio na tafakuri juu ya mambo yanavyo endelea.
Mwigulu alikuja na isue ya ugaidi wa Lwax,mkatengeneza mkanda wa aibu.mlikuwa mnatengeza mazingira ya kufanya unyama mlioupanga wa kunyofoa meno kucha na macho ya watu wasio na hatia ili watu waamini kwamba ni chadema. Sasa mnakuja na hili jipya, ni kama ya mwigulu. Mko tayari kufanya lolote ili mbaki madarakani, mnadhani nyny ndo mlioandikiwa na mungu kuongoza nchi hii?
Msidanganye watu kwa uongo unaotangulia kuandaa mazingira ya ujambazi wenu juu ya wananchi.
Mbona mmechanganyikiwa hivo?
Sijui kama bado mnakwenda misikitini na makanisani kweli kwa dhati maana sasa mnaonekana kabisa mnaongozwa na shetani.
Au ndo mmeamua kumsujudia shetani ili awape vyooote chini ya dunia pamoja na watu wake?
Mtadanganya sana
mtaua sana
mtafunga watu kwa uongo sana
lakini mwisho utafika na mtaondoka kwa aibu.
Nape, Muogopeni Mungu kwani hata shetani anamuogopa sana.