Napata raha sana kuona mashabiki wa Simba na Man U wakiwa hawana raha

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
3,882
4,511
Yaani katika maisha yangu naweza kupata hela nyingi tu na nikaona kawaida yaani. Ila Mashabiki wa Simba na Man wakiishi kwa stress napata faraja sana na naona nina kila kitu katika maisha.

Hasa hasa hawa watu wa Msimbazi wanapoanza kunyosheana vidole, kukamatana uchawi, kufukuzana na kusutana furaha yangu huzidi.

Nimekuwa addicted kufatilia mapovu ya aina zote youtube, JF ndo usiseme siwezi kupitisha dk 2 sijaingia jukwaa la Michezo kuangalia current povu la wanasimba.

Waza unavyowaza ila kila mtu ana namna yake ya kuburudika.

Jana nimeangalia povu la wanaSimba wakiimba hawamtaki Mangungu siafikiani nao ila nilifurahi tu kuona wanavyoumia na kuteseka huku nyuso zao zikiwa zimekunjamana. Kuna shabiki nilikuona analia kisa Simba kutoa sare na Namungo hakika nilifarijika sana mpaka nikamsamehe kodi ya miezi 2 mpangaji wangu.

Mashabiki wa Simba walichangishwa hela ya kujenga uwanja mpka sasa hela zao hazieleweki zimefanya kazi gani.Kitendo cha hela zao kuliwa kinanifurahisha sana maana wanaumia.Natamani aliyekula hizo hela nimpe zawadi.

Ufanisi wangu katika kufanya kazi za Jamhuri umeongeza mara dufu kwa siku hizi chache. Hakika Simba wameineemesha Serikali🤣🤣

Sinywi pombe wala aina yeyote ya anasa furaha yangu ndo hiyo. Kipindi Simba inafanya vizuri niliteseka sana.

Haka kamsemo ka TABULELE nakapenda sana japo sijui maana yake maana kanawakera, kuwahuzunisha sana Mashabiki wa Simba huku kakiniacha na tabasamu pana usoni.

TABULELEE

Waheed.
 
Sinywi pombe wala aina yeyote ya anasa furaha yangu ndo hiyo.Kipindi Simba inafanya vizuri niliteseka sana.
Hahaha, kwa namna hii ukichukua Siku zako za kuishi duniani ukatafuta uwiano wa siku za furaha vs siku za huzuni takwimu zimekaaje?
 
Yaani katika maisha yangu naweza kupata hela nyingi tu na nikaona kawaida yaani.Ila Mashabiki wa Simba na Man wakiishi kwa stress napata faraja sana na naona nina kila kitu katika maisha.

Hasa hasa hawa watu wa Msimbazi wanapoanza kunyosheana vidole,kukamatana uchawi,kufukuzana na kusutana furaha yangu huzidi.

Nimekuwa addicted kufatilia mapovu ya aina zote utube,Jf ndo usiseme siwezi kupitisha dk 2 sijaingia jukwaa la Michezo kuangali current povu la wanasimba.

Waza unavyowaza ila kila mtu ana namna yake ya kuburudika.

Jana nimeangalia povu la wanaSimba wakiimba hawamtaki Mangungu siafikiani nao ila nilifurahi tu kuona wanavyoumia na kuteseka huku nyuso zao zikiwa zimekunjamana.Kuna shabiki nilikuona analia kisa Simba kutoa sare na Namungo hakika nilifarijika sana mpka nikamsamehe kodi ya miezi 2 mpangaji wangu.

Ufanisi wangu katika kufanya kazi za Jamhuri umeongeza mara dufu kwa siku hizi chache.Hakika Simba wameineemesha serikali

Sinywi pombe wala aina yeyote ya anasa furaha yangu ndo hiyo.Kipindi Simba inafanya vizuri niliteseka sana.

Waheed.
Nyambaf


shuwain


Mwehu uliyetukuka


Utopolo mkubwa
JamiiForums598407804.jpg
 
Nipo na wewe bega kwa bega shida ni pale ubao unapogeuka! Anyway tusipangiane furaha kutesa ni kwa zamu
 
Hahaha, kwa namna hii ukichukua Siku zako za kuishi duniani ukatafuta uwiano wa siku za furaha vs siku za huzuni takwimu zimekaaje?
Siku za furaha zimeongezeka mara dufu mkuu
 
Back
Top Bottom