.....Oopss..... The kid is only 11yrs bana, hata baleghe bado haijakaa sawa unamtisha na HIV, STD and the likes? ....hata kumpa 'smartfone' u chat nae pia ni wrong!
Huyu underage, anatakiwa anolewe hapo hapo kwenye spiritual teachings kujua 'madhambi na madhara yake.' mtoto anaogopa dhambi kuliko haya maradhi ya wakubwa aka ngono!
Samahani lakini...😉
Tatizo si kukabidhiwa kwa mwalimu wa nidhamu...tatizo ni distance yako na wazazi wako...
Kwa nini haukumsemea kwa wazazi???
Mimi babab yetu alikuwa rafiki...hata hao walimu walikuwa wakimpelekea hiyo feedback (umbea) tulikuwa tunanafasi ya ku explain; including kuwakandia baadhi ya walimu kuwa wanajipendekeza tu wala hawatufundishi.
Sasa kama wewe mwalimu alikuwa ana ku abuse (au alitaka kuku abuse) ukakaa kimya eti kisa wazazi wamekukabidhi kwake...tatizo ni la uhusiano wako na wazazi wako...na mwalimu atakuwa alijua hiyo weakness.
Kitu kingine mie naongelea primary school ambayo haikuwa boarding...huyo mwalimu atafanya mapenzi na mie wapi???
Bado nakazania...mwalimu ni vema awe rafiki na mzazi...it works...
Hiyo haina maana kuwa mtoto hana uhuru wa kuongea na haki ya kusikilizwa...triangulation kwa kila information ndio mpango mzima.
King'asti, huwa tuna-underestimate uwezo wa watoto wetu, sababu tunadhani ni wadogo.
Wanajua mengi mno, mengi vingine hadi unashangaa akikueleza.
Mfano kuhusu AIDS wanafundishwa sijui darasa la pili, mie huwa napenda mtoto asikie jambo kutoka kwangu maana najua watoto huamini wazazi zaidi na maneno ya mzazi huwa hayasahauliki kirahisi.
Hahhaha, im sure my parents were not worried about me. Manake akijisemesha mtu anapata majibu ya kumtosha. Kuna mwalimu alinitakaga praimare nikamuambia naenda kukusemea kwa maza. Afu nilimuambia mama, tukamtetaa weeeh. Ila seems hakumuuliza manake leo tukikutana namuambia nilikusemeaga haamini. Dah, them days!
King'asti (Komando)Tell him all about sex, how it can ruin him hopelessly. Muambie about hiv, stds na unawanted pregnancies. Jinsi anavyoweza kujitwika ubaba na utakavyomhenyesha na kumnyima utoto. Muambie na kuhusu same sex problems na ilivyo laana kwa mtu binafsi na familia pia. Tell him how you wish you were a kid and dont have to worry about stuff. Kikubwa mjengee hofu ya Mungu na sio ya mzazi.
Tell him popote alipo God is watching over him. He should fear God than humans. Whatever he feels to do in the hiding must be wrong, so bora asifanye manake hakuna ambacho Mungu amekataza ambacho hakina madhara kwa binaadamu.
Kama ana maswali muambie auntie king'asti is ready for him,lol. Mpe hiyo iPhone nichat nae😀
Duh, BAK umenitisha hiyo ya kunyonya nanilii; kweli l am more scared.
Naipata pia point ya Dark City na Mbu, nimependa ushauri wa King'asti wa kumprobe ndicho nilichoanza kufanya. Kwakweli changamoto ya kuwa single mother of the boy ni pamoja na hii.
Ngoja uncle KIKUNGU aongee naye maana wanaelewana huku nami nikimuuliza vitu na kumuomba opinion yake juu ya baadhi ya mambo.
Kitu ninachoahidi nikutomuamishia wasi wasi wangu.
Thanks EMT kwa uchambuzi yakinifu, anaenda Feza Boys sasa sijui for sure iko kwenye kundi gani. Labda waliosoma hapo wanaweza nitoa wasiwasi juu ya malezi.
Kwenye rules zao, bullying inalead kwa sunspension but shule gani ambayo haina adhabu kama hizo kwa bullying.
Nimeamua aende boarding kwakuwa huku niliko hakuna shule nzuri, na pia sipendi sana kuwa mzigo kwa ndugu zangu; inaepusha maneno na inaleta ukaribu ukipunguza unnecessary usumbufu.
Kweli nilikuwa sijawahi mwambia kuhusu sex na pregnancy na STD.
Alishawahi kuniuliza mimba inapatikanaje, nikashindwa kujieleza na kumwambia amuulize mwalimu. That was when he was in grade 5.
Nimeshawahi kumuuliza kuhusu HIV tu na jinsi inavyoambukizwa; tough topic ni kuhusu ushoga, how do you explain jinsi gani mwanaume anakuwa na mwanaume mwenzake?
Kongosho,Babu Dark City, kwa kiwango fulani nakubaliana na wewe.
Kwetu huwa tunasema, usipende kumnenepesha ng'ommbe siku ya mnada, ndio maana kuna vitu ni bora kumwandaa mtoto tangu akiwa kinda.
Ila, kama mzazi, kuna speech lazima umkalishe mtoto kidogo useme naye.
Hasa kwenye mambo ya msingi kama ya mahusiano, huu ushoga unatusha sana kama una mtoto wa kiume. Hata matumizi ya mlango haramu unatisha pia, ila ukifundishwa ni 'don't touch' ukiwa mdogo hausahau kabisa.
Mie nadhani huwa nasambaza sumu zangu kwa watoto, inawezekana nakosea lakini nahisi ni wajibu wangu. Atachagua njia yake akiwa mkubwa.
NB: Binti wa JF mwenye story yake ya boarding kama nimeikosea awe huru kunisahihisha
he he he, yaani wewe bhange tangia primari??
Mie nilizitumia sekendari, kuna ticha aliniganda hadi nikaichukia kemia hadi kesho.
Imagine fomu wani libaba hadi linatoa mchozi, likiniona tu mahali hili hapa lol
wakati bado napanga mashambulizi likahamisha, nilipop shampeni, oops nilipop maji tu.
Kuna jingine nikalichuna twisheni miezi mitatu afu nikasepa, chezeiya mtoto wa manzese wewe.
Nilidhani ni Smile lakini nafikiri alisema shuleni kwao walikuwa wanaminywa minywa matiti na mwalimu wa kiume kuona kama..... ila jinsi mwalimu alivyokuwa anayamisya alikuwa na lake.