Naombeni mwongozo

Naombeni mwongozo

mkuu hawa beki 3 ni changamoto kwa kweli ukisema umlimit ndo utaumia kabisa hata mtoto anaweza akaugua gafla akashindwa kukupa taarifa chamsingi nunua sim ya mezani alafu unaunganisha laini moja tu ya kwako akipiga sehem nyingine sim haiendi hapo utakua umemkomesha

exactly! that's a very decent solution.
 
pole mwaya kwa mdada wa kwanza wa kazi hapo home
ninachoomba cha kufanya mketishe chini muelezee kinagaubaga wa
wewe unapomwachia hela ya voucher kuwa ni matumizi ya kinyumbani
na si kibinafsi yake , muelezee kuwa unapo;pigia ujue kuna kitu unataka
kufahamu happo nyumbani pakoje na mambo ya dharula kiujumla akufaahamishe

vilevile mtengenezee jedwari au ratiba kamili ya mzungumko wa voucher zako
uzitoazo hapo home kuanzia tarehe 1-30 ili ujue unatoaga voucher ngapi na za
shilingi ngapi kwa matumizi ya home kwako

labda ratiba hii ambayo ni demo itakusaidia namna ya kuweza kumpangia bajeti za voucher
hapo home kwako bestito

HUU NI MFANO TU KAMA WAWEZA KUCHUKUA CHUKUA AU VYYOVYOTE BEST

Na Matumizi ya Voucher siku mwezi jumla ya mwezi
1 VOUCHER NGAPI KWA SIKU MWEZI YOTE

Nawasalimu wana MMU.

Jamani tuna hawa wadada wanatusaidia kukaa na nyumba zetu.

Kama tujuavyo maisha ya siku hizi bila simu inakuwa patashika kidogo.

Huwa mdada akija kama hana simu huwa nampa simu ambayo nimeinunua kwa ajili ya nyumbani ili niweze kuwasiliana naye naye awasiliane nami ambapo sipo nyumbani.

Na kama inatokea mdada kaja na simu yake basi simlazimishi atumie ile yangu, huwa natumia tu ile namba yake kwa mawasiliano.

Kinachotokea mpaka naomba mwongozo hapa ni kwamba; Huwa nampa sh. 1000 kila wiki kwa ajili ya simu, ili akipata dharura basi aweze kunitaarifu. Mara nyingi mimi huwa napiga simu nyumbani mara kwa mara kwa hiyo inatokea mara nyingi tu ndani ya wiki hajanipigia wala kutuma sms hata moja, na yaweza kuwa hivyo hata mwezi mzima.

Kinachonichosha, siku ikitokea kapata dharura wala hapigi, nikiuliza naambiwa simu haina hela.

Wenzangu pia mnakumbwa na hili tatizo?

Nifanyeje sasa ili hili tatizo liishe?

sababu wakati mwingine ni jambo la maana kabisa linatokea lakini hawezi kuniambia kisa hela kwenye simu kamaliza zoote kupigia watu wake, sasa maana yoooteee ya mimi kumpa hela ya simu inakuwa haipo.

Nimepata mdada mpya sasa nataka nianze naye tangu mwanzo sheria ya hela yangu ya simu iweje........
 
Rafiki baadhi ya Wababa wako tofauti. Wanajua fika kwamba Mama mwenye hawezi kufuatilia mambo ya pale nyumbani 24/7 hivyo nao husaidia ili kuhakikisha huyo msaidizi waliyemfungulia milango na kumkaribisha nyumbani kwao ni mtu salama na anafuata taratibu zote za pale nyumbani na kama Baba mwenye nyumba ataliona lolote ambalo halitamfurahisha basi anaweza kujadiliana na mwenzie ama lirekebishwe au kuamua kuachana naye.

Msaidizi wa nyumbani tajiri wake anaweza kuona anamthamini sana kwa vitu mbali mbali ambavyo humfanyia ikiwemo kula chakula kizuri cha pale nyumbani, kupewa pesa, kulala mahali pazuri n.k. lakini kwa huyo msaidizi jambo kama la kuzuwiwa kuongea na nduguzake akaliona kubwa sana na kusahau mengine yote hivyo kuwaambia watu "Yule mama ana roho mbaya sana hataki niongee na ndugu zangu."

Ubahatike uwe na yule ambaye ataamua kufunga virago kwa kutokubaliana yeye kutoongea na ndugu zake, lakini mwingine anaweza kusema "Huyu mama mwenye nyumba yake na roho mbaya yake ngoja nimkomoe." Akaenda kununua gudulia la mafuta ya taa akasubiri watoto wamelala ndani akatia kiberiti nyumba yote au akatayarisha msosi na kutia sumu ya panya (Mungu apishilie mbali)

Hawa watu wengi wao wana matatizo mbali mbali lakini tunapoamua kuwafungulia milango ya majumbani mwetu basi tuwe karibu nao sana na kuwaona kama ni ndugu zetu hivyo kutowawekea sheria nyingi ambazo hatuwezi kuwawekea ndugu zetu kwa usalama wa wenye nyumba, watoto wao na mali zao.

Good day 🙂🙂🙂
 
Hayo yooooote uliyoaorodhesha hapo ni mambo ambayo ni ya msingi kwa binadamu yoyote yule kuyapata na hutakiwi kuyahesabu kabisa kwa mtu ambae anakulelea wanao,kukufulia,kukusafishia nyumba yako n.k

Mshahara unaompa hautoshi kukamilisha mahitaji yake yote ikiwemo na vicha kwaajili ya kuwasiliana na wazazi,ndugu na jamaa zake,sio kwakuwa yeye ni msaidizi wako basi asiwasiliane nao,lakini cha ajabu zaidi ni wewe kuona mtu kupewa sh 1000 kwaajili ya vocha wiki nzima kuwa ni sawa

Sijui unaonaje kuwa ni sawa hata kama unamhudumia yote hayo uliyoyasema

Ni kwanini ukimfanyia ndugu yako huyahesabu lakini kwa msaidizi wako unayahesabu?

Au ndugu yako ni binadamu kuliko msaidizi wako wa kazi?

Hujaelewa bado. hiyo 1000 ni kwa ajili ya emergency tu. kama akitaka kupiga simu kwa ndugu zake atawekewa airtime atapiga. hakuna mtu aliyesema kwamba anamnyima beki 3 kupiga cm kwa ndugu na jamaa zake.

na kama 1000 ikitumika ikaisha leo ataongezewa nyingine papo hapo--1000 haiko FIXED!
 
If only everyone else had the same perception about house-helps like you then the world would have been a better place!!! Do not underestimate the power of someone who cooks for you, cleans up after you, look after your kids when you are out making money, literally gets the house running in your absence. Tuwapende na kuwaheshimu hawa mabinti jamani, treat them like they were your own family, akikosea mkanye like you would do your own siblings, hizi shida ndogo ndogo za kila siku utazisikia kwa jirani tu!

hakuna mtu anayetaka kuwanyanyasa hawa beki 3 hata kidogo--sote tunaishi nao kiundugu na kirafiki. tunachojaribu kuongelea hapa ni JINSI GANI YA KUWA-SHAPE ILI WAWE NA MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI ZA WAAJIRI WAO--hii ndiyo point and there's no one claiming to look baby sitters down his/her nose!!!
 
Asante sana tpaul kwa kunisaidia kuelezea na kujibu hoja, kweli mada imekuingia kisawasawa, nimejifunza mengi toka kwako
 
Last edited by a moderator:
Rafiki yangu BAK, hakuna sehemu nimesema sitaki aongee na ndugu zake..... aongee nao tu any time, sina shida na hilo.
Sijui naeleweka hapa au la; huyu mtu nampa 1000 kwa wiki kwa ajili ya kunipigia endapo dharura itatokea nyumbani, ni kiasi cha kutoa taarifa tu. Siku hizi bongo simu ni very cheap kupiga, yaani mimi hata sms naonaga uvivu kutuma. napiga kwenye mtandao wowote, muda wowote, ni cheap sana. huyu mdada anaweza kaa mwezi mzima asinipigie simu ya dharura, inawezekana hata miezi mi3 au mi4, kila siku huwa anapokea tu simu zangu. lakini sasa ikija tokea kumetokea dharura na anahitaji kuwasiliana nami anasema hana airtime, unadhani hiyo ni fair?
Kuhusu wababa kusaidia kuangalia wadada endapo mama hayupo hilo halina mjadala, wababa wote wanafanya hilo. Ila naweza kukushangaa sana rafiki mkeo yupo sitting room wewe upo busy kumwelekeza dada jinsi ya kufanya kazi pale nyumbani, utakuwa unafanya kazi si yako.
Have a good day as well:smile-big::smile-big:
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
hakuna mtu anayetaka kuwanyanyasa hawa beki 3 hata kidogo--sote tunaishi nao kiundugu na kirafiki. tunachojaribu kuongelea hapa ni JINSI GANI YA KUWA-SHAPE ILI WAWE NA MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI ZA WAAJIRI WAO--hii ndiyo point and there's no one claiming to look baby sitters down his/her nose!!!
natamani hii pia ionwe na BAK na Eiyer
Asante sana kwa ufafanuzi huu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hahahahaha lol!!!! Rafiki kwenye hili bado msimamo wangu haubadiliki. Tunazungumzia usalama wa familia kwa jambo dogo sana ambalo msaidizi anaweza kabisa kuamua kuipoteza familia nzima au kuiacha na majonzi makubwa sana. Pia simaanishi msaidizi atumie tu financial resources za familia hovyo hovyo kitu ambacho hata ndugu hatuwezi kumruhusu. Ninachosema ni kuwa flexible ili hawa wenzetu wasijione wanabaguliwa na hivyo kuhatarisha uhai na mali za familia au kutafuta mwingine kila baada ya miezi michache baada ya kushindana.

natamani hii pia ionwe na BAK na Eiyer
Asante sana kwa ufafanuzi huu
 
mfundishe huduma ya tafadhali nipigie...mpe mazoezi ya kufanya hivyo angalau mara moja kwa siku....

hata mi nilitaka kumshauri hivi huyu bi dada--na badala ya kumfundisha formula hiyo asevu jina lake kwa kabisa ili kwamba beki 3 akipiga jina lake apokee ujumbe wa pls call me.
 
ukimuunganishia hv ndio ataacha kazi zote atakaa kupiga cm cku nzima! wewe beki 3 huwajui vzr eeh?

Kwani beki 3 hawafai kuwa na social lives? Kuwa na marafiki?

Utamfungia hadi lini?
 
Mie huwa sijitii headache na maid hata siku moja. Kwa suala hili uliloleta hapa, nakushauri ununue mobile fone ya mezani. Nenda voda hapo wanakupa lisimu la mkonge, ukiwa nyumbani unawaka halijafutwa vumbi. Hicho kimobile ndo kwanza unampigia yuko mtaa wa tatu na anakujibu niko home, hali shwari!

but anyways, kukaa na msichana ukimfanya comfortable utafaidi wewe. Mpigie wewe, tena mruhusu akutumie msg ya tafadhali nipigie kama ana shida yoyote. Tena jumapili kaa na wanao, muache dada akabarizi kwa maboifrendi. jirani wa kakangu alikuwa mkali hapo UDSM, hgal haruhusiwi kupiga picha hata na mwanae wala wanae hawaruhusiwi kwenda kwa jirani. Siku mwanae alikuwa anaharisha, kina dada wakakaa kimya tu na sie tuko home tunaangalia tv tu. By the time mama mtoto anarudi saa moja usiku, anakamata mwanae kwenda hospitali, mtoto anafariki!

mtoto anaweza kuungua ama kuumia mbele yako na usiweze kumlinda. Relax

simu la MKONGE? hahaha! mkuu umenichekesha sana! hata mi nalitamani.
 
Rafiki umeshamjua huyu tabia yake kwamba hakupigii hata kuwe na dharura, hivyo kila saa moja tafuta dakika tano tu za kumpigia ili kujua hali nyumbani iko shwari. Mama mwenye nyumba hawezi kuwepo nyumbani 24/7 anaweza kuwa amesafiri kikazi, kwa dharura kama msiba, ugonjwa n.k. Hapo baadhi ya Baba wenye nyumba huamua kufuatilia shughuli za msaidizi ili kujua kila kitu kiko shwari wakati mama mwenye nyumba yuko mbali na nyumbani. Hili la wasaidizi kuikomoa familia limetokea mara nyingi tu sehemu mbali mbali nchini na hata duniani. Hivyo ni vizuri kuhakikisha kila siku iendayo kwa Mungu familia iko salama. Nimeliona dongo lako Hahahahaha lol! Nikabaki natabasamu tu 🙂🙂🙂

Rafiki yangu BAK, hakuna sehemu nimesema sitaki aongee na ndugu zake..... aongee nao tu any time, sina shida na hilo.
Sijui naeleweka hapa au la; huyu mtu nampa 1000 kwa wiki kwa ajili ya kunipigia endapo dharura itatokea nyumbani, ni kiasi cha kutoa taarifa tu. Siku hizi bongo simu ni very cheap kupiga, yaani mimi hata sms naonaga uvivu kutuma. napiga kwenye mtandao wowote, muda wowote, ni cheap sana. huyu mdada anaweza kaa mwezi mzima asinipigie simu ya dharura, inawezekana hata miezi mi3 au mi4, kila siku huwa anapokea tu simu zangu. lakini sasa ikija tokea kumetokea dharura na anahitaji kuwasiliana nami anasema hana airtime, unadhani hiyo ni fair?
Kuhusu wababa kusaidia kuangalia wadada endapo mama hayupo hilo halina mjadala, wababa wote wanafanya hilo. Ila naweza kukushangaa sana rafiki mkeo yupo sitting room wewe upo busy kumwelekeza dada jinsi ya kufanya kazi pale nyumbani, utakuwa unafanya kazi si yako.
Have a good day as well:smile-big::smile-big:
 
elewa somo kwanza kabla ya kutema povu. hakuna mtu aliyemzuia kuwasiliana ila aweke fedha zake, asitumie vibaya mali ya mwajiri.

imagine umemtumia mwanao karo halafu amechukua amekula yote kisha akarudishwa home. unapomuuliza anakuambia alichukua pesa ya karo akachezea kamari! utamuelewa?
Bahati mbaya hata ujui mada ipi ya kutoa povu ila kwa kuwa umejua kusema neno hilo basi unalitumia hata mahali ambapo halina haja,mfano wako ulioutoa mbona haulingani na mada iliyopo?
 
Back
Top Bottom