Kabla haujaliona hilo kama tatizo na kuja kuomba muongozo ulipaswa kwanza kujichunguza ili ugundue kikwazo ni kipi.
Pili yakupasa kuelewa kwamba mdada wakazi na yeye pia ana maisha yake anahitaji kuwa huru kufanya baadhi ya mambo yake ambayo hayatavunja misingi ya kazi yake, katika hili swala lako yapo mambo mengi sana ya kuyatazama kiundani zaidi, umedai mara kwa mara huwa unapiga simu sitaki kuuamini kwamba hizo dharura huwa zinategea na kutokea wakati ambao haupigi simu.
Tatizo liko kwenye mitazamo yenu na jinsi mnavyo wachukulia hao wadogo zetu wanapokuja kuwafanyia kazi huko majumbani kwenu, kwanza kabisa kiasi cha pesa mnachowalipa hakiendani kabisa na majuku mnayowatwisha, na pia hauwezi kugharamia mahitaji yake yote, haiitajiki kuchukua maelezo yako mengi ili mtu akusome jinsi unayoishi na binti yako wakazi, kwa maelezo hayo tu inaonesha na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoishi na wadada wandani kwa kuwaendesha kama magari mabovu huku mkiwalipa kiasi kidogo cha pesa.
Nafikiri ungekuwa unamlipa kiasi kizuri cha pesa hata usingekuwa unatoa hiyo 1000 kwaajili ya simu, angeweza kulimudu hili kwa vile na yeye mawasiliano kwake ni muhimu kwa ndugu na jamaa zake. kama kweli kiasi cha pesa unachomlipa kinamtosheleza na hiyo 1000 unayotoa, swali la kujiuliza ni kwamba je, ni mzembe kutoa taarifa inapotokea dharura? kama jibu ni hapana, na sababu ni simu haina vocha basi tunarudi kule kule kwenye malipo unayomlipa ni kidogo.
Kweli pesa ni ngumu, na hakuna pesa ndogo, pia ukidharau mia hauwezi kupata 1000, hivyo bajeti ni muhimu swala la msingi ni je kiasi cha bajeti yako kinatosheleza mahitaji ya dada wa nyumabani?...
Swali la kizushi..
Ikitokea huyo mdada wako wa kazi akawa anakupigia simu mara kwa mara hata kama dharura haijatokea na mara nyingine awe anakurushia salio hata 1500, wakati huo wewe huwa unamuachia 1000 kwa wiki, utajifikiria nini juu ya huyo mdada? na utachukua hatua gani?
CC;
kiwatengu ,
The Boss ,
Mrigariga,
ICHANA ,
Nokia83 ,
dyuteromaikota ,
hips.com ,
Caroline ,
danzi ,
Munambefu ,
Mashaxizo ,
everlenk ,
Joseph ,
Bulldog ,
Eiyer,
Mr mgeni,
stroke,
byb sac,
gfsonwin,
Honey Faith,
bornagain,
thinky,
isha,
Miss Kim,
frank wa moyo,
Chauro,
Mbu,
Escardo-bird, Natanguliza samahani kwa usumbufu kwa kuwakusanya hapa, kilichonifanya niwakusanye hapa naomba muwe watazamaji atakacho nijibu
Fixed Point