Naombeni muongozo wa kupima DNA

Naombeni muongozo wa kupima DNA

ya nini hayo
sisi kwetu tarime mmiliki wa mtoto ni aliyetoa mahari kwa mama yake. wengineo wakimzalimzalisha mkeo ni wanakufanya kibarua. tarime tunauliza ukifanya kibarua shambani kwa mtu mazao yanakuwa ya kibarua au ya mwenye shamba
kweli wakuriya mpo vizuri kwenye misimamo
 
Kuna mwamba ninamjua alienda kupima DNA na akaambiwa watoto ni wake ila watu tulikaa kimya tu kwasababu muhuni aliyetia kamba Hana mbele Wala nyuma
Nakwambia tena hiyo ngumu sana kwenye ofisi ya mkemia mkuu, yaani ni ngumu sana. Sisi tulio nje hatujui tu mchakato mzima unavyokuwa mpaka sampuli zinamfikia mtu wa maabara. Hata yeye hajui anapiga sampuli ya nani, yaweza kuwa hata ya ndugu yake
 
Shida wale wapimaji wataanza kuuliza chanzo cha kupima, muwahadithie story za maisha yenu, waangalie hali ya baba, mama na mtoto kisha ndio wawapime.

Hapo lazima majibu yatakua na influences nyingi tu.
Mmeamua kupeana stori za vijiwe vya kahawa.. Forensic analysis zote zinafanyikia pale. Mchukua sampuli sio mpeleka sampuli mpaka maabara, mchakato wake uko tight
 
Nakwambia tena hiyo ngumu sana kwenye ofisi ya mkemia mkuu, yaani ni ngumu sana. Sisi tulio nje hatujui tu mchakato mzima unavyokuwa mpaka sampuli zinamfikia mtu wa maabara. Hata yeye hajui anapiga sampuli ya nani, yaweza kuwa hata ya ndugu yake
Ukitaka majibu ya uhakika pima Nchi tatu, Tanzania, Uganda na Kenya, alafu linganisha majibu yao,yakipishana ujuwe kuna mziki hapo fanya uchunguzi wa kina!!
 
Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha
Kabla hujapima dna unajua Sheria inawaruhusu watoa majibu ya dna kudanganya kuhusu majibu..?
Hiyo ni kwaajili ya kumlinda mtoto asije kukosa mahitaji yake muhimu nakuepusha watoto wa mtaani..?
Unalo hilo mkuu...?😂
 
But kadri ya uelewa wangu hapa Tanzania sheria haziruhusu mtu binafsi kwa mapenzi yake kupima dna. Maombi ya kupima dna huwasilishwa kwa mkemia mkuu na taasisi kama vile mahakama, jeshi la polisi, ofisi ya ustawi wa jamii nk
Hapana,mtu binafsi unapima muhimu uwe na mwanasheria ndiye atakayeomba Hilo ila inapimwa tena Kwa laki 3 tu majibu unayapata
 
Kaka siyo kufafana kipindi cha mimba huyu mwanamke alikuwa amepanga wanaume 3 na alikuwa na kadi 3 za Clinic hospital tofauti.

Baadaye wanaume hao walifahamu wote wakamtema, sasa now ni miaka 7 tangu azae sasa anadai mwanaume mmoja ndiyo mhusika, je utakubalije kiboya hivo.
Wanawake wa hivyo ndo wangekuwa wanaume wangekuwa majambazi au vibaka, fuata nilichokuelekeza hapo.
 
Tafuta wanaume wawili walipe, kisha gombeeni huyo mtoto kila mmoja aseme ni wake alafu sampo zenu zipelekwe kwa Mkemia. Subiri majibu. Hakikisha kila mmoja aseme ni Wake.
 
Madhara yake ni yapi? Kwa mfano mtoto akakutwa kweli ni wa kwako lakini akajua ulikuwa na mashaka naye itakuwaje?
 
Nenda Nairobi Kenya DNA inapimwa chapu km UTI TU. Na hakuna kubebana kinacho toka ndio unapstiwa.
 
Madhara yake ni yapi? Kwa mfano mtoto akakutwa kweli ni wa kwako lakini akajua ulikuwa na mashaka naye itakuwaje?
Hilo siyo tatizo,tena ndiyo anafurahi zaidi! Watu msiogope DNA, sasa mkiogopa DNA mnaweza pima ngoma wenyewe just kuangalia afya yako!!
 
Kama mwanamke anakupenda na mtoto uliyezaa naye ni wako nakuhakikishia ukishatekeleza hilo wazo lako utamsababishia maumivu makali sana moyoni.

Ikiwa umefikia hatua ya kutaka kupima DNA tafsiri yake ni kuwa uaminifu baina yenu haupo, jambo hili kwangu mimi binafsi linaweza kuwa chanzo tosha cha kuamua kutoendelea kuishi na mwenza wangu.

Utaumia sana nafsi yako ikiwa matokeo ya vipimo yataeleza kuwa mtoto hana vinasaba vinavyoshabihiana na wewe.

Je, unao uwezo wa kuhimili kupokea majibu ya matokeo hasa yakija kwa namna ambayo si matarajio yako?
 
Utaratibu ni lazima uwe na mwanasheria alafu uwe na Sababu ya kufanya hivyo pia wahusika ni watatu wewe mkeo na mtoto gharama Ni kila sampuli ni laki moja hivyo jumla ni lakitatu.

Ila angalizo wanaume wengi wanalea watoto wasio wakwao na DNA ya uhakika Ni Ile ya kutuma taasisi binafsi, lakini ya serikali inamiongozo yake Kwa Sababu wanaelewa mzigo wa watoto wasio na baba watakuwa wengi serikali itaitaji kuhudumia na madhara yake Ni makubwa.
Taasisi binafsi ipi inapima DNA kwa hapa Tanzania?
 
Hivi, kwenye mji; mwanamke anayefanya umalaya,na mwanaume mzinzi, bora yupi?
Haiingii akilini,eti mwanaume ukae unajua unachezewa kekundu,wanakuona tahira,af upotezee.
Ushauri huo hauwezi ukatolewa na mwanaume anaejitambua. Undugu mwanaume anao na wanae. Mke,mtoto wa wengine. Sasa akupe mzigo wa kulea mtoto wa watu,baba yake yupo?! Si utahila huo sasa! Mara mia ujue nachukua mwanamke na watoto nalea,si nachukua mwanamke anakuja mzalia mtu kwangu af nazugwa tu.
Kwanza ukijitambua,mbona rahisi tu hata likizaliwa siku hiyo kama si lako utajua tuuu.
Kuliko uhangaike na DNA, tafuta shoga yake,mpe hata laki,mgonge uone kama hutatoka na taarifa kamili
 
Kitanda hakizai haramu piga chini hilo wazo ila kama mamaake anazingua mkazie
Kizazi cha zamani ila cha sasa kimegoma kulea mabao ya watu wengine na kuleta tabia za hovyo kwenye ukoo.

Kila mmoja aubebe msalaba wake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom