Naombeni muongozo wa kupima DNA

Naombeni muongozo wa kupima DNA

Hii dunia ya sasa sidhani kama ni faraja kuishi na dukuduku la mtoto ambayo huna uhakika ni wako.
Zamani ilikua rahisi, mawasiliano na baba wa mtoto yanapotea kabisa na mkeo na unafurahia ndoa yako.
Zama hizi za technology inawezekana mkeo ana mawasiliano mazuri sana na baba wa mwanawe. Na kwa namna hali ilivyo, huenda mbele huko mtoto atajua wewe si baba yake mzazi?
Ule msemo wa kitanda hakizai haramu umesaidia nini?
Nini ushuhuda ndio maana nimeandika hivi.
Kulea mtoto ambaye huna uhakika naye hutampenda kutoka moyoni
 
Wakenya mnajitia wajanja hakuna cha Nairobi wala nini kila kitu hapahapa huko Nairobi mkapimane wakenya kwa wakenya mtu wetu haji huko
Kupima tu DNA inakuwa changamoto, nchi ngumu hii
 
TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA VINASABA

Taratibu za kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba

Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009. Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na

Maafisa ustawi wa jamii, Mawakili, Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro, Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai, Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba, Wakuu wa Wilaya,Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria

3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki .

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
Maabara hizi ndo zile zile za kupimia Covid19 au. 😂😂 kwa hapa utaambiwa tu wako ata kama sio wako, maana mapapai yalikuwa na covid19 sembuse wewe mtoto uyo. Dawa nenda Private akuna kitu kinacho shindikana ukiwa na pesa tu. Hizo zengine ni bwebwetu. 😎
 
Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha
Achana na hayo makitu hayana faida.
 
Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha
Anzia ustawi wa jamii mkikubaliana watawapa mwongozo. Ni rahisi tu lakini umejiandaa. Mimi nalea mmoja najua si chapa yangu na sioni shida kabisa.
 
Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha
Kama wewe ni mchaga mpeleke nyumbani wazee watakupa ufumbuzi.
 
Kulea mtoto ambaye huna uhakika naye hutampenda kutoka moyoni​
Lazima kupima DNA ili hata kama wamepika majibu tayari itajulikana kitaalamu na kisheria kwamba mtoto ni wako........hawa wanawake akili mbovu mkipishana kauli kidogo hachelewi kukutamkia kwamba mtoto si wako, na hapo tayari umeshalea hadi kafikisha miaka 25.

Jambo jingine, mtoto lazima afanane na ndugu zake ndani ya ukoo......mtoto ambaye hana ufanano wowote na wewe au ndugu wengine ndani ya ukoo labda ndo imekupelekea kupata mashaka.

Kwa kuanzia kabla hujaenda kwenye DNA cheki magroup ya damu, la kwako wewe, la mama na la mtoto......halafu utuletee mrejesho.​
 
ya nini hayo
sisi kwetu tarime mmiliki wa mtoto ni aliyetoa mahari kwa mama yake. wengineo wakimzalimzalisha mkeo ni wanakufanya kibarua. tarime tunauliza ukifanya kibarua shambani kwa mtu mazao yanakuwa ya kibarua au ya mwenye shamba
 
Kuna njia Moja naona ni Bora sana, nayo ni njia ya kupitia group la damu. kwangu Mimi namshauri mtu aanze na njia hii kabla ya kuingia maghalama ya DNA na tunajua majibu lazma utakua na mashaka nayo kutokana na picha tuliyojijengea.

Kwa mfano ikitokea wewe baba group lako la damu ni group A na mwanamke ni group A, hapo piga ua galagaza mtoto atadondokea kwenye magroup mawili tu nayo ni A au O. Sasa ikitokea mtoto ni group B au AB basi unajua tayari umeguswa kwenye mshono
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Nov 2023 lenye kichwa Cha habari"Serikali yatoa Mwongozo wanaotaka kupima DNA"

Utaratibu ni kuwa na barua kutoka either 1)Ustawi wa Jamii 2)Mwanasheria au 3) mahakama then utaipeleka ofisi ya mkemia.

Utapewa Control number ulipie 300,000.Then mambo mengine yatafuata.
Tarehe 30 Nov 2023 mbona bado haijafika!? Hii taarifa itakua fake!!
 
1.Tukana marafiki zake was kufa na kuzikana mitusi ya nguoni.

2.Tembelea eneo la Kazi au mahali anapopenda kushinda uone mtoto anafanan na Nani eneo Hilo.

Mbinu Namba moja unalala na majibu yako haina kupoa.
Shikilia moyo tu.
Tz mtoto hakosi Baba.
#Biolab
 
Back
Top Bottom