Naombeni muongozo wa kupima DNA

Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha

TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA VINASABA

Taratibu za kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba

Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009. Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na

Maafisa ustawi wa jamii, Mawakili, Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro, Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai, Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba, Wakuu wa Wilaya,Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria

3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki .

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
 
Kitanda hakizai haramu piga chini hilo wazo ila kama mamaake anazingua mkazie
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Nov 2023 lenye kichwa Cha habari"Serikali yatoa Mwongozo wanaotaka kupima DNA"

Utaratibu ni kuwa na barua kutoka either 1)Ustawi wa Jamii 2)Mwanasheria au 3) mahakama then utaipeleka ofisi ya mkemia.

Utapewa Control number ulipie 300,000.Then mambo mengine yatafuata.
 

Attachments

  • Screenshot_20231115-194453.png
    Screenshot_20231115-194453.png
    45.6 KB · Views: 19
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Nov 2023 lenye kichwa Cha habari"Serikali yatoa Mwongozo wanaotaka kupima DNA"

Utaratibu ni kuwa na barua kutoka either 1)Ustawi wa Jamii 2)Mwanasheria au 3) mahakama then utaipeleka ofisi ya mkemia.

Utapewa Control number ulipie 300,000.Then mambo mengine yatafuata.
Duuuh, tutegemee ndoa kuendelea kuvunjwa kwa speed ya 5G
 
Pole na majukumu wanajamvi.

Kwa mwenye uelewa na hili naomba mwongo wa hatua za kufuata kupima DNA pale unapokuwa na mashaka juu ya mtoto.

Naomba kuwasilisha
Ulipochomeka dude lako live hilo katikati ya mapaja hukujua kuwa waweza tia mimba mtu au kumpa au kupata ukimwi mjinga wewe?

Unakuja kutusumbua Jamii Forums na ubwege wako
 
Nani alishapima akaambiwa mtoto si wake hapa Tz? Muulize yule anayejiita Simba la masimba la madangote 😂

Jaribu nje ya nchi kama una uwezo.
 
Usijisumbue utapoteza pesa bure mwisho wa siku utaambiwa mtoto ni wako kumbe sio damu yako.
Kubali yote kitanda hakizai haramu
Hii dunia ya sasa sidhani kama ni faraja kuishi na dukuduku la mtoto ambayo huna uhakika ni wako.
Zamani ilikua rahisi, mawasiliano na baba wa mtoto yanapotea kabisa na mkeo na unafurahia ndoa yako.
Zama hizi za technology inawezekana mkeo ana mawasiliano mazuri sana na baba wa mwanawe. Na kwa namna hali ilivyo, huenda mbele huko mtoto atajua wewe si baba yake mzazi?
Ule msemo wa kitanda hakizai haramu umesaidia nini?
Nini ushuhuda ndio maana nimeandika hivi.
 
Back
Top Bottom