Naombeni msaada kurudi bongo

Naombeni msaada kurudi bongo

Ushauri wangu endelea kuzichanga mpaka ukifikisha miaka 65 ndio urudi , kwa umri huo unaweza kukubalika kwenye nyumba za wazee pugu au vingungutu . Hapo ndoto yako ya kulala na kuamka kunywa maziwa itakuwa imetimia , maana huko msosi bure tu.
 
Utafikia wapi? Huko Gonja ukute wazazi walishaenda njia ya wengi.
 
Bongo kuna wanawake wanaoa? Mbona vijana MMU wanalalamika saana?
Watakuwa wanakosea timing! Dogo Mmoja wa kitaaa anauza GAME pale Mlimani city, nilimuuliza why wanafunzi wa vyuo jirani wanajaa sana maeneo yale? Wana purchasing power ya kutosha pale? Akanambia wale boys na mabeg yao mgongoni wanawinda Majimama!
 
Hiyo 1800 bado hujatoa nauli ya kurudia...anyway, karibu tz omba omba siku hz hawabugudhiwi kiviiiile.
 
WÉ RUĐÏ ŢÙ ÙJÎÒÑÊÈ MWĔÑŸËWË
huto tunyodo twako twote tutaisha
 
umenichekesha mnooo yaani sina hofu mume umeniandalia tyr
Naomba nikubuku asee ukifika tu nakutambulisha kwa nabii ili nakupiga ndoa fasta ila ujiandae kufanya kazi ya Mungu. Ila mi Mzee wa miaka 48.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo.
Bora ubaki hukohuko dingi...maana huku Jiwe kawakazia raia hawahemi....
 
Nauli ya kurudia ni sehemu ya hiyo dola 1800? Uko nchi gani? Umeoa au ni Senior Bachelor? Hadi unafikia umri wa miaka 51 bado haujaamua utaseto wapi maisha ya uzeeni? Unafuatilia kujua mabadiliko ya dola na shilingi? Unaomba usaidiwe au anaongea kwa dhihaka? Unaaminisha kweli au umetumia lugha tata kufikisha manung'uniko yako dhidi ya current regime? Nina maswali mengi lakini naomba unijibu hayo ili nione namna ya kukushauri.
Labda bombardier likianza ruti za huko azamie kurudi nyumbani
 
Hutaki kula nafaka unataka chakula yaan wewe nenda tu mbinguni kunakufaa
 
Mkuu ongeza speed kuserch money angalau urudi hata na usd 10000 upate hata cha kujengea kibanda na mtaji wa kulimia tangawizi huko upareni
 
JF raha sana,

Chige, umenichelesha sana.

Mr experience you know!
Hahaha! Raha sana enzi hizo... enzi za Yahoo Messenger! Wanazengo wakikushtukia, si kelele hizo "...don't trust Mr. Experience, he's a Nigerian!" Halafu najiita Mr. Experience wakati ndo kwanza nimetoka chuo... sina cha kufanya zaidi ya kushinda kwenye PC!
 
Le Mutuz na yeye alirudi Bongo akiwa na umri around na huo na hivi sasa nasikia yeye ndo King of Social Networks! Sasa wewe ukitua Bongo itabidi ufungue Instagram Account na ujiite Zee la Mastory Ya Mbele! Au nikukopeshe jina langu nililokuwa natumia miaka hiyo, enzi hizo kabla ya JF... Mr. Experience, na stori zangu za kuuza Tanzanite wakati hata Arusha kwenyewe sikujui!

Dah! Ujana raha sana!!
Lemutuz mbona ana miaka around 56 mtoto wake alivujisha siri
 
Back
Top Bottom