Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Mkuu, pole sana ila usikate tamaa jipange na uendelee kupiga box kwa angalau miaka mingine 5 au 10.
Je umeoa na una familia?
Kama jibu ni ndio basi ongeza kazi hiyo miaka 10 kwa ajili ya pensheni yako ya uzeeni kwenye kamradi ukirudi TZ.
Pia kama una familia na nyumba haipo, basi chukua bima ya kama Euro 200000 hivi ili iwasaidie endapo utaaga dunia.
Watoto wa kiafika huko ughaibuni wakifika miaka 16 tu wanaanza kuwakoromea wazazi wao kwa kuwahoji kwamba kwanini wao ni maskini, hiyo inauma sana maana huwezi kuchapa viboko.
Kuwa wale wazazi ambao hutumia ile fedha ya watoto ya kila wiki badala ya kuwawekea akiba.
Na kama waishi kihalali huko majuu basi angalau utakuwa umewekeza kwenye mafao yao wazungu angalau kila wiki utakuwa na mshiko kidogo.
Mimi nimeishi huko kama wewe lakini nilipofika miaka 35 nikasoma alama za nyakati na sasa nashukuru Mungu namudu maisha ya pande zote.
Nilikuwa nikirudi bongo kuangalia wapi niweke kitega uchumi na imesaidia sana.
Ila hujachelewa, piga box angalau miaka 5 kama si 10 ili upate chochote kamtaji kuweka kitega uchumi ambacho ukiamua kurudi kimoja utakuwa wasimamia wewe mwenyewe.
Kuwa twarudi nyumbani mara kwa mara kunasaidia sana kupata mawazo mbadala na yale ya kupiga boksi tuu kutwa kucha.