Naombeni msaada kurudi bongo

Naombeni msaada kurudi bongo

Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Miaka yote hiyo mzee baba hukufanikiwa kujenga hata kibanda nyumbani?vipi ndugu zako ulikuwa unawatoa kidogo au ndio uliwasahau?kama uliwapotezea jiandae nawe kupotezewa pia,kuna jamaa yangu nae alichomoka kipindi hicho na hadi leo hajatia mguu nyumbani...sema yeye matukio ya nyumbani anashiriki kuchangia kuliko walio huku na keshajiwekea mjengo wake
 
Duh pole mkuu, ina maana kila mwaka ulikuwa una sevu dola 69.23 tu. Kama tayari una nyumba bongo na miradi mingine ambayo tayari inakuingizia hela hapo unaweza kurudi, vinginevyo komaa ughaibuni.

Kusevu nini? sikuwa na habari ya saving. I raised up a family here, kila kile nilipata nilitumia kulea wanangu. Sasa watoto ni wakubwa, sioni tena sababu ya kuishi huku.
Asante ndugu uliesema ruvuma au mpanda kunafaa kwa situation yangu.
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Mkuu upo nchi gani? Yaani $1800 bado hujakata ticket halafu unataka uje bongo uishi comfortable bila hata kupanda daladala unywe na maziwa daily! Usijari njoo utaishi vizuri sana sema hizo dola $1800 zibadilishe ziwe kama za Zimbabwe (Zitakuwa milions) Kwa hiyo utanunua nyumba, gari etc..
 
duuu pole sana.
mini nina uzoefu. mtu yeyote akiondoka kwao muda mrefu bila kuja kusalimia mara kwa mara huwa hawawi na akili nzuri ktk masuala ya jamii. mara nyingi mtu kama huyo utakuta kafiwa na watu wake kibao, pengine hata wazazi. lkn yeye haji tu. hiyo inapelekea kuwa mtu wa tofauti sana, mwingine unakuta hata familia hana. anaanza kuwa mzigo kwa wengine.

kwa habari ya huyu ndugu inabidi aendelee kukusanya nguvu. aone akifika miaka 55 atakuwa na kiasi gani. lkn kwa kiasi cha pesa alicho nacho ni kidogo. kwa wengine ni mshahara wao wa mwezi huo. isitoshe gharama za maisha ziko juu. endelea kudunduliza mpaka at lease 20+k $. hapo unaweza fanya kitu.
 
Jaman mimi nitakuwa tofaut na wote.. hutu age ishaenda tayar na pesa hajapata na nyumbani ni nyumbani. RUDI tu Tanzania hicho ulichokipata hata km.ni milion yako wewe njoo tu kwani kwa age yako utarudi maiti home.. rudi tu.. but kwani kampuni ulonayo hawatoi hela ya wastaafu hukuajiliwa??? Ndugu yangu rudi nyumbani kweni ni kwenu hata ukilala chini.ni kwenu rudi tu.
 
Nyumbani I mean origin yako ya vizazi huko kwingine ni kutafta tu life mkuu. Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani
NYUMBANI KWAKO NI MAHALI POPOTE PALE UNAPO LALA NA KUAMKA, ASUBUHI UNAPATA BREAKFAST, MCHANA - SUPPER , JIONI -DINNER , KOMAA HUKO HUKO
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Aisee mzee kwa umri huo sikushauri ukuje huku?Hujapata muke ya huko?Uko nchi gani maana kukushauri inategemea na nchio uliopo.Una watoto?
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
Unachangamsha genge na $1,800 siyo? Acha utani. Tumia hiyo kununua tiketi halafu njoo ulime. Bado kuna mapori mengi tu.
 
Utateseka mkuu...Hapo una chini ya Tshs milioni 5 yani utaishia kulipa kodi ya miezi sita na kununua vyombo vya ndani. Nakuhakikishia jipange walau uwe na walau USD elfu 7 uje uwekeze kimradi vinginevyo sikushauri urudi kwa kiwango hicho unaweza kukata tamaa ya maisha na unaweza hata kujidhuru
Nakubali 100%. Kuanza maisha na 1800USD kwa umri wa miaka zaidi ya 50 is close to impossible kwa aina ya maisha aliyoitaja. Tena hiyo 7000USD ni ndogo.
Kwa basics alizozitaja ni bora aende kijijini kwao. Otherwise ni bora abaki huko huko aiseee.
Sijui
 
Habari wana jf.
Mimi ni mbongo ambaye nipo ughaibuni tangu 1992 na sijawahi kurudi bongo. Nilikuja huku kutafuta maisha na kusoma, lakini kutokana na gharama za maisha na gharama za elimu sikuweza kusoma. Sasa nina miaka 51 na natamani kurudi bongo. Elimu yangu ni ya form 4 ya pugu secondari 1988. Benki nina dola 1800 tuu. Jee naweza kurudi bongo na kuishi comfortably? Yaani kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).
Kuna fursa gani huko kwa wazee kama mimi?
Naombeni msaada wenu
sijawahi kuona muomba msaada kiburi kama wewe eti chakula kizuri sio nafaka
 
Kwa miaka uliyokaa huko kwa mwezi ulikuwa una-save dola ngapi ndio mpk leo ziwe 18000. Bora ubaki tu hukohuko uendelee kupambana tu la sivyo utakuja kuokota machupa ya palstick huku
Umeongeza 0.
punguza
 
Back
Top Bottom