African Geek

JF-Expert Member
Jul 29, 2022
778
1,353
Habari wana JF, Mimi ni Developer ( Web & Mobile ). Nina uzoefu na web development upande wa Backend na Frontend. Pia nimejifunza mobile app development kwa Flutter na nimefanikiwa kufanya project kadhaa ndogo ndogo kwa ajili ya kujiimarisha na kupata uzoefu wa kile nilichojifunza.

Kwa sasa nimeweka nia ya kufanya project rasmi ambayo nitaiweka Play Store na App Store. Hivo nilikua naomba mawazo yenu niweze kuanza hii project. Je, nitengeneze App inayohusiana na masuala gani au inayotatua changamoto gani ?

MCHANGO WAKO NI MUHIMU SANA. NATANGULIZA SHUKRANI 🙏
 
If possible ukifanikiwa kuipata idea na kuweka project git ningependa kuchangia, nimeanza flutter mwaka jana hadi sasa nina project mbili nimezifanya kwa flutter, kwa bahati mbaya siwezi kuzitaja hapa
 
kama uko makini chagua moja hapa
online nida copy
Kuuza za mitandao yote
Kusajili line mitandao yote
Asante kwa mchango wako. Ila hii ya nida copy ni mpaka nipate API yao na ni ngumu kupatikana mana hata wao wenyewe wamesitisha huduma ya kutoa copy za vitambulisho.

Kusajili line haitakuwa practical mana ni lazima mtu apate simcard kwanza ambayo hupatikana kwa mawakala
 
If possible ukifanikiwa kuipata idea na kuweka project git ningependa kuchangia, nimeanza flutter mwaka jana hadi sasa nina project mbili nimezifanya kwa flutter, kwa bahati mbaya siwezi kuzitaja hapa
Asante sana mkuu nitashukuru. Pia sio mbaya ukiweka japo screenshot ya project zako tufaidike na tuwe motivated sisi mabeginner :)
 
Njia nzuri ya kuunda ni ku-observe ww mwenyewe vitu wanavyofanya kundi Fulani la watu halafu tazama mwenyewe kitu gani unaweza kusolve Kwa mfano unaweza kutazama shughuli za walimu baada ya hapo unaweza unda kitu na ukaanza kuuza kwenye mashule bila hata kutegemea ads kama chanzo cha revenue ya app yako.

Ndio maana kampuni kubwa zinawekeza kwenye R&D
 
Imenyooka sana hii. Nadhani hii ni best option
 
Tumia keyword tool kuangalia ni neno gani linatafutwa sana playstore (TZ/Duniani), then unatengeneza app kutokana na keyword
Hiyo itakusadia kupata install za kutosha na reviews(kwa uboreshaji zaidi)

Natafuta mtu wa kuweka Adsblock ya popup kwenye webview , Kama vp utanicheki kwenye ✉️
 
Tengeneza inayohusu masuala ya kifedha kama vile paypal yaan iwe kama wallet unawez hifdh pesa pia unaweza kulipia vitu nk na kama utakwama uje tushlikiane apa
 
Mimi ni flutter developer, shida yangu kubwa ni mfumo wa malipo, naitaji msaada kwa mtu anaeweza ku intergreate mfumo wa malipo yaani mtumiaji aweze lipia kwa mpesa , Airtel au Tigopesa .
 
Ni rahisi sana, nina push to pay API za Airtel & Tigo, ungependa nikupatie?? Lakini pia ili kukamilisha hillo kama unataka ku intergrate na operator moja kwa moja hakikisha una server iliyokuwa hosted kwenye mazingira yenye uwezekano wa ku establish ipSec vpn, ingawaje kwa airtel wao wanatumia open Api hawahitaji mambo ya ipSec tunnel. Kwa kuanzia unaweza anza na Airtel hawana mchakato mrefu compare to other operators.
 
Kaka shukran, nitakutafuta ndg yangu
 
Habari wana JF, Mimi ni Developer ( Web & Mobile ). Nina uzoefu na web development upande wa Backend na Frontend. Pia nimejifunza mobile app development kwa Flutter na nimefanikiwa kufanya project kadhaa ndogo ndogo kwa ajili ya kujiimarisha na kupata uzoefu wa kile nilichojifunza.

Kwa sasa nimeweka nia ya kufanya project rasmi ambayo nitaiweka Play Store na App Store. Hivo nilikua naomba mawazo yenu niweze kuanza hii project. Je, nitengeneze App inayohusiana na masuala gani au inayotatua changamoto gani ?

MCHANGO WAKO NI MUHIMU SANA. NATANGULIZA SHUKRANI
Ila wew
 
Hiyo ya ku-track namba za simu za watu na Location waliyopo achana nayo, watu wanaweza kuitumia kufanya uhalifu, mwishowe ukaingia mgogoro na polisi.

Mimi cha kukushauri, Tengeneza APP maalumu kwa ajili ya watu wanaotafuta Nyumba za kupanga, Nyumba zinazouzwa na Fremu za maduka. Mimi naona kila siku watu wanatembea kwa miguu kutafuta nyumba za kupanga na Fremu za maduka, na wanaouza nyumba nao uangaika... Sasa Tengeneza APP ambayo itakayokuwa inaonesha ramani kama Google Map location, Picha za nyumba, Bei na kadharika... Kama Uber na Bolt wanavyofanya kwenye kukodi usafiri, lakini wewe unatengeneza za wanaotafuta nyumba za kupanga, fremu za maduka na nyumba zinazouzwa... Wewe unadili na REAL ESTATE
 
Kama upo vizuri, tengeneza software za kuunlock modem, router na simu kwa IMEI au direct. Kuna hela balaa
Unlock code kwenye simu moja ina gharimu mpaka 13, 000. Anza na ZTE MF Series modem & router. Angalia mfano wa DC unlocker Client
 
Back
Top Bottom