Naomba ushauri wa njia bora ya kuendesha Microfinance

Naomba ushauri wa njia bora ya kuendesha Microfinance

Mkopo wako walengwa ni kina nani???, watumishi, wajasiriamali au watu binafsi??

Kama ni wajasiriamali wadogo wadogo nakushauri weka riba asilimia 20% na 4% gharama ya fomu( kama taratibu nyingine za ukaguzi na utambulisho wa serikali za mtaa na malipo ya software kama unatumia)...

Wajasiriamali weka utaratibu wa kua wanaleta marejesho kila siku ili kupunguza risks za kupoteza hela, walau mpaka mwezi ukiisha hatakama anakua hajamaliza basi deni libaki kidogo tofauti na ukimpa mwezi mzima alipe sikumoja kwa MJASIRIAMALI mdogo ni changamoto kupata hela kwa pamoja....,

Kabla hujampa hela make sure unathaminisha dhamana zake walau ziwe na thamani mara mbili au mara tatu ya hela anayochukua,.

Na awe na wadhamini wasiopungua wawili na hakikisha wote wanasign siku ya kuchukua mkopo ili iwe rahisi kupata msaada siku kukitokea changamoto ( Make sure wote watatu wanaambatanisha passport na copy za vitambulisho na muhuri wa kiongozi wa mtaa kwenye fomu yake ya kuombea mkopo)

The last but not least, make sure unakua na system nzuri ya managements( hapa nazungumzia microfinance software's za uhakika kama FIMA), Japo wana cost ghali lakini ufanisi wake ni mkubwa
hii systm naitumia iko poa sana
 
Back
Top Bottom