Naomba ushauri wa kusoma "Masters"

Kuliko kusoma Masters, ni bora uweke malengo na mipango ya kujifunza namna ya kuongeza Kipato nje ya mshahara, kwa maana wekeza kwenye kujifunza yaliyowashinda wengine, iwe biashara au uwekezaji wowote wenye tija kwa miaka yako ya mbele.

Habari za ndoto achana nazo, kipindi upo secondary sidhani kama ulikua na ndoto za kuwepo ulipo sasa.
Ukweli mtupu mkuu wangu, nimepokea ushauri wako kwa mikono miwili.
 
Mdogo wangu hongera sana, ulileta taarifa zako JF wakati umegraduate hiyo ni Sawa kabisa. Baadae ukaleta taarifa jinsi ulivyoulizwa maswali ya interview hii ni sawa pia.
Baada ya hapo tunasema Ahsante MUNGU umepata Ajira!
Kwakuwa sasa Umeajiriwa na Miongoni mwa Viapo ulivyosaini ni kutoongelea inshu za mwajiri wako yaani serikali popote nashauri ubadili mada za kuleta JF, Mambo yako ya kazi yabaki kuwa Siri yako. Narudia stori za Ofisini na Watu wa Ofisini ziache kwenye geti la Halmashauri mdogo wangu. Leo umekuja na inshu unatafuta ushauri wa kusoma wakati hata bado hujathibitishwa kazini.
Utanogewa kesho utakuja na jipya.

Ni wakati wako sasa uweke Strategies za kubadilisha elimu yako ibadilishe maisha ya Wananchi wa Halmashuri yako.

Ni wakati huuu unapaswa kuleta hoja za mikakati na njia zipi sisi Walalahoi tunaweza kujikomboa kwenye umaskini. Tumekuombea dua hapa hapa JF utoboe hebu sasa tulipe fadhira kwa Usomi wako na nafasi yako, achana na papara ka popocorn kikaangoni, tulia tuliiiiii acha mapepe Ofisini.
Ishi kama mjinga usiyejua lolote ila ukipewa kazi unaipiga kwa usahihi wa 100%.
Acha kuchangia mada za Majungu na kumponda boss wako wakati mwingine machawa wapo kazini na huenda wakakurekodi kabisaaaa.
Punguza lopo lopo na mipango miiiingi hadharani bw mdogo.
Jitofautishe kiutendaji na maafisa uliowakuta, tengeneza to do list zako za siku wiki au mwezi, na ukiweza jipe cheo cha back up ya mipango ya idara.
Kumbuka baada ya miezi 12 DSO wako ataombwa taarifa zako za upekuzi ili uthibitishwe kazini, endapo utadharau andiko hili vetting yako yaweza kutoka lkn ukiwa ratted as Rubbish and unpontential staff.
Anyway kila mtu aishi anavyotaka tusipangiane brooo. Mimi nilikua nawaza tuuu jinsi ningekuwa mimi ningeishi. Kineheeee......Kwaheri Ngosha.
Daaah!! Ahsante sana mkuu wangu, hakika wewe ni mshauri mzuri, umenena ukweli mtupu katika taarifa yako nemesoma neno kwa neno, msatari kwa mstari, aya kwa aya, sijaona neno la kinafiki hata moja. Hongera sana ubarikiwe na bwana.
 
poleni na hongera kwa majukumu ya kila siku, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kimsingi nahitaji kusoma "masters" ila sijuwi ni kozi gani itanifaa na kuleta tija kwangu.

Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.

Project management is the best for you, kwa degree yako, hii itakufaa, ukiwa na fursa ya kusoma soma.
 
unaenda kusoma kwa ajili ya mtu, au kwa ajili yako? Km hujui unachotaka kusoma sasa kwanini utamani kwenda kusoma? Hayo ni mambo yako binafsi
 
Hongera sana mkuu kwa kupata ajira.

Kabla ya kuuliza ni masters degree gani itakufaa weka juhudi kwenye kupata uzoefu wa hiyo kazi kwanza. Fanya kazi kwa ufanisi uwezavyo, kwa kuwa upo halmashauri angalia mabosi wako wana nini cha ziada(kielimu). Utaona patterns ya aina za masters degree ambazo ni relevant kwenye field yako na career yako kiujumla. Maana wapo wenye masters hapo ulipo au kwenye halmashauri nyinginezo. Wengi wao ndio hao wakuu wa Idara, But kuwa mkuu wa Idara au Kitengo kigezo sio elimu peke yake bali na uzoefu kazini (seniority) na uchawa.

Pili, kuna wadau wameshakueleza ukweli. Masters haina mchango wowote kwenye kipato kwa kazi za halmashauri. Labda kukupa connection ya kupata cheo cha kiofisi (sio cha mfanyakazi). Kwa kada yako kusoma masters ni kama patapotea.

Tatu, kwa standing order ya serikalini kama sijakosea ni lazima ufanye kazi miaka mitatu (3) kabla ya kuomba likizo ya malipo kwenda kusoma. Hivyo nashauri focus kwenye kazi kwanza wakati unausoma mchezo.

Kama una ndoto za kusoma masters degree endelea kushikilia hapo ila usije ukawa disappointed hapo baadaye.

Notable masters degree zinazoweza kukufaa.

-Project Planning Management
-Social welfare
-Sociology
-Community Development
-Humanities
-Political Science
-Diplomatic Studies
-MBA
-Public Relations
Hongera sana mkuu wangu kwa ushauri wako uliojaa hekima na busara nyingi. Hakika Mungu akutunze kama hadhina, kama kisima cha kuchota maarifa, hekima, busara na uzoefu mbalimbali.
 
Kwanza kachape kazi. Waajiri wengi hawata kupa likizo ya masomo kabla ya muda fulani kupita labda kama utasoma OUT. Muda huo utakupa ikomavu kazini na utajua sheria zao za kwenda kusoma na kama wana masters wanazo zipendelea.
Masters inaweza isibadilishe kipato chako mara moja lakini inaweza kufungua milango mingine na kuna vyeo bila masters utavisikia tu. Ni investment nzuri.
Anzia hapo mengine yatafuata.
Hongera sana mkuu wangu kwa ushauri wako uliojaa hekima na busara nyingi. Hakika Mungu akutunze kama hadhina, kama kisima cha kuchota maarifa, hekima, busara na uzoefu mbalimbali.
 
Hongera

Lakini kumbuka hakuna mshahara wa shahada mbili aka masters ,ukiajiriwa serikalini utaanza sawa na mwenye shahada then vinafuata vyeo,kupanda vyeo kutategemeana na connection au Uchawa na unafiki wako Kwa wakubwa!!

Angalia usije kufa Kwa depression baada ya kupata masters
Noo big no watu wanalipwa mshaara wa mastar ushauri wangu asomee kozi aliyopatia kazi
 
Maono yako,ndoto yako lazima utimize.Usisubiri ukae miaka 5.
Mshahara unapata,nenda OPEN UNIVERSITY Kama kituo kipo karibu,jisajili ingia Kuna kozi Kule ya community development,kasomeee,kasomeeee.
Kasome saaana,haijalishi Kama hutapanda cheo,haijalishi Kama mshahara wako UTAKUWA wa degree.HAPA NI MAONO YAKO,VISION YAKO LAZIMA UITIMIZE.
Kasome,hujui kesho itakuwaje!!
Kikubwa KAWE CHAWA WA MUNGU,JICONNECT NA MUNGU,UTAKUWA JUU SANA MPAKA USHANGAE.
 
Ahsante sana tena sana, nimepokea maoni mengi lakini maoni yako hakika yametisha sanaaaaaaaa. Unafaa kuwa motivation speaker, ubarikiwe na bwana.
 
Maono yako,ndoto yako lazima utimize.Usisubiri ukae miaka 5.
Mshahara unapata,nenda OPEN UNIVERSITY Kama kituo kipo karibu,jisajili ingia Kuna kozi Kule ya community development,kasomeee,kasomeeee.
Kasome saaana,haijalishi Kama hutapanda cheo,haijalishi Kama mshahara wako UTAKUWA wa degree.HAPA NI MAONO YAKO,VISION YAKO LAZIMA UITIMIZE.
Kasome,hujui kesho itakuwaje!!
Kikubwa KAWE CHAWA WA MUNGU,JICONNECT NA MUNGU,UTAKUWA JUU SANA MPAKA USHANGAE.
Mleta mada chukua ushauri huu,
Utakuja kumshukuru huyu ndugu miaka michache ijayo.
 
Kasome angalia na uwezekano wa kufanya kazi kwa miaka 3 then omba ruhusa.

Kwa umri wako ni vyema kusoma kabla ya 40's ...Soma ili uweze kusecure nafasi yako na uombe Mungu unaweza kupata promotion hata kwenda sehemu nyingine..

Kama una nia fanya kusoma ila usifuate mkumbo.
Daaah! Kumbe hakuna faida yoyote tena mkuu, je! Niruhusu ndoto yangu ya kusoma "masters" isitimie mkuu?
 
Kasome angalia na uwezekano wa kufanya kazi kwa miaka 3 then omba ruhusa.

Kwa umri wako ni vyema kusoma kabla ya 40's ...Soma ili uweze kusecure nafasi yako na uombe Mungu unaweza kupata promotion hata kwenda sehemu nyingine..

Kama una nia fanya kusoma ila usifuate mkumbo.
Ahsante sana mkuu, mawazo mazuri kama haya ndio nayahitaji, ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom