Naomba ushauri wa kozi ya kusoma kwa Masters

WISE G THE BRAIN

New Member
Jan 17, 2013
4
1
Wadau habari za Muda huu,

Ninaomba ushauri kidogo Kwa wanaojua Nina mdogo wangu ni mwalimu wa sekondari aliyeajiliwa alisoma Bachelor of Arts with Education GPA ya 3.4

Anataka kusoma Masters lengo lake ni kubadili kada kutoka ualimu au kupanda ngazi na kutoka kwenye kufundisha aende kwenye taasisi za Elimu. Je course ipi ni nzuri hapa hasa ukizingatia atasoma Open University sababu eneo alilopo hakuna chuo.

1. Master of Arts in Monitoring and Evaluation (MA M&E)

2. Master of Arts in Governance and Leadership (MAGL)

3. Master of Education in Administration,Planning and Policy studies (MED CDD)

4. Master of Education in Curriculum Design and Development

Pia naomba kujua hawa waalimu walio na masters wanabadili vipi kada Kwa ku apply au wanabadilisha na Waajili Moja Kwa Moja?
 
Taasisi za elimu G.P.A yako haitoshi maana walau ungekua na kuanzia 3.5 hadi 3.8.

Iwapo unataka ukimbie ualimu vizuri angalau kasome bachelor nyingine.

Hizo masters ulizo orodhesha hapo hazina tija kwa sasa.

Ebu ongezea nyama mkuu.
 
Kwanini asiende kampasi moja kwa moja mpaka aamue kusoma Open? Alafu mbona kama ni ww mkuu unaomba ushauri na sio mdgo wako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom