Naomba ushauri wa kusoma "Masters"

Aug 25, 2019
79
80
poleni na hongera kwa majukumu ya kila siku, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kimsingi nahitaji kusoma "masters" ila sijuwi ni kozi gani itanifaa na kuleta tija kwangu.

Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.
 
Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (udom).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.
Hongera kwa kupata ajira..

Ushauri :- fanya kazi kwanza (at least 05 years) maana kama usemavyo umeipata baada ya muda kidogo tangu ulipomaliza chuo, Kuhusu Kozi ya kusoma utaipata as unaendelea kufanya kazi.
 
Hongera

Lakini kumbuka hakuna mshahara wa shahada mbili aka masters ,ukiajiriwa serikalini utaanza sawa na mwenye shahada then vinafuata vyeo,kupanda vyeo kutategemeana na connection au Uchawa na unafiki wako Kwa wakubwa!!

Angalia usije kufa Kwa depression baada ya kupata masters
 
Ushauri wako unachekesha sana mkuu wangu, kwamba "uchawa" but thanks nimejifunza kitu kutoka kwako
 
Kula mshahara kwanza kijana papara za nini?
Shahada umehitimu 2017 halafu umepata Ajira 2023 (miaka 6 upo kitaa unachapika) halafu bado una kiherehere cha kwenda kusoma tena??

Kwa Halmashauri, hususani kada yako ya CDO masters haina faida yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah! Kumbe hakuna faida yoyote tena mkuu, je! Niruhusu ndoto yangu ya kusoma "masters" isitimie mkuu?
 
Hakuna faida yeyote zaidi sana itakuongezea depression tu kuona una masters halafu bado unalipwa mshahara sawa na wenye Bachelor.

Tena usipokaa vizuri huko Halmashauri unaweza pelekwa hata kukaimu ofisi ya mtendaji wa Kijiji akipata likizo na Masters yako au kupelekwa kwenye mageti ya kukusanya ushuru

Hahah! Mambo hayo sasa kutoka kwa wadau.
 
Kuliko kusoma Masters, ni bora uweke malengo na mipango ya kujifunza namna ya kuongeza Kipato nje ya mshahara, kwa maana wekeza kwenye kujifunza yaliyowashinda wengine, iwe biashara au uwekezaji wowote wenye tija kwa miaka yako ya mbele.

Habari za ndoto achana nazo, kipindi upo secondary sidhani kama ulikua na ndoto za kuwepo ulipo sasa.
 
Hongera sana mkuu kwa kupata ajira.

Kabla ya kuuliza ni masters degree gani itakufaa weka juhudi kwenye kupata uzoefu wa hiyo kazi kwanza. Fanya kazi kwa ufanisi uwezavyo, kwa kuwa upo halmashauri angalia mabosi wako wana nini cha ziada(kielimu). Utaona patterns ya aina za masters degree ambazo ni relevant kwenye field yako na career yako kiujumla. Maana wapo wenye masters hapo ulipo au kwenye halmashauri nyinginezo. Wengi wao ndio hao wakuu wa Idara, But kuwa mkuu wa Idara au Kitengo kigezo sio elimu peke yake bali na uzoefu kazini (seniority) na uchawa.

Pili, kuna wadau wameshakueleza ukweli. Masters haina mchango wowote kwenye kipato kwa kazi za halmashauri. Labda kukupa connection ya kupata cheo cha kiofisi (sio cha mfanyakazi). Kwa kada yako kusoma masters ni kama patapotea.

Tatu, kwa standing order ya serikalini kama sijakosea ni lazima ufanye kazi miaka mitatu (3) kabla ya kuomba likizo ya malipo kwenda kusoma. Hivyo nashauri focus kwenye kazi kwanza wakati unausoma mchezo.

Kama una ndoto za kusoma masters degree endelea kushikilia hapo ila usije ukawa disappointed hapo baadaye.

Notable masters degree zinazoweza kukufaa.

-Project Planning Management
-Social welfare
-Sociology
-Community Development
-Humanities
-Political Science
-Diplomatic Studies
-MBA
-Public Relations
 
poleni na hongera kwa majukumu ya kila siku, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kimsingi nahitaji kusoma "masters" ila sijuwi ni kozi gani itanifaa na kuleta tija kwangu.

Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.
Ushauri wangu kwako ni kwamba si unataka kusoma, unashindwa nini sasa......nenda kasome. Hujafungwa mnyororo wala kamba na haukatazwi kusoma.
 
poleni na hongera kwa majukumu ya kila siku, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kimsingi nahitaji kusoma "masters" ila sijuwi ni kozi gani itanifaa na kuleta tija kwangu.

Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.
Mdogo wangu hongera sana, ulileta taarifa zako JF wakati umegraduate hiyo ni Sawa kabisa. Baadae ukaleta taarifa jinsi ulivyoulizwa maswali ya interview hii ni sawa pia.
Baada ya hapo tunasema Ahsante MUNGU umepata Ajira!
Kwakuwa sasa Umeajiriwa na Miongoni mwa Viapo ulivyosaini ni kutoongelea inshu za mwajiri wako yaani serikali popote nashauri ubadili mada za kuleta JF, Mambo yako ya kazi yabaki kuwa Siri yako. Narudia stori za Ofisini na Watu wa Ofisini ziache kwenye geti la Halmashauri mdogo wangu. Leo umekuja na inshu unatafuta ushauri wa kusoma wakati hata bado hujathibitishwa kazini.
Utanogewa kesho utakuja na jipya.

Ni wakati wako sasa uweke Strategies za kubadilisha elimu yako ibadilishe maisha ya Wananchi wa Halmashuri yako.

Ni wakati huuu unapaswa kuleta hoja za mikakati na njia zipi sisi Walalahoi tunaweza kujikomboa kwenye umaskini. Tumekuombea dua hapa hapa JF utoboe hebu sasa tulipe fadhira kwa Usomi wako na nafasi yako, achana na papara ka popocorn kikaangoni, tulia tuliiiiii acha mapepe Ofisini.
Ishi kama mjinga usiyejua lolote ila ukipewa kazi unaipiga kwa usahihi wa 100%.
Acha kuchangia mada za Majungu na kumponda boss wako wakati mwingine machawa wapo kazini na huenda wakakurekodi kabisaaaa.
Punguza lopo lopo na mipango miiiingi hadharani bw mdogo.
Jitofautishe kiutendaji na maafisa uliowakuta, tengeneza to do list zako za siku wiki au mwezi, na ukiweza jipe cheo cha back up ya mipango ya idara.
Kumbuka baada ya miezi 12 DSO wako ataombwa taarifa zako za upekuzi ili uthibitishwe kazini, endapo utadharau andiko hili vetting yako yaweza kutoka lkn ukiwa ratted as Rubbish and unpontential staff.
Anyway kila mtu aishi anavyotaka tusipangiane brooo. Mimi nilikua nawaza tuuu jinsi ningekuwa mimi ningeishi. Kineheeee......Kwaheri Ngosha.
 
Ukweli mchungu kaka, Kuna walimu wana masters lkn tunafundisha nao form 1 C,wakati Kuna watu wana diploma wapo halmashauri ..

Ukiwa na masters kutumwa na mtu mwenye diploma inaudhi sana!
Daaah! Ukweli mchungu lakini umefanya vizuri kuuzungumza mkuu

Back
Top Bottom