Habari zenu,
Ni hivi nimeolewa, mume wangu ana watoto 2 kabla ya ndoa yetu nasi tuna watoto wawili. Wote ni waajiriwa nje ya jiji la DSM. Baada ya kuoana tukaanza maisha nikajikuta naachiwa majukumu ya kutunza nyumba. Jamaa kila nikimuuliza anasema hana hela na haishi sababu ambazo mimi zikawa zinanitia shaka. Nikavumilia nikawa natoa hela maisha yanakwenda kama kawaida pale home.
Ikafika kipindi nikaamua kuchunguza kweli hana hela? Nikawa nakuta deposit slip jamaa ana deposit hela kwenye account yake, nikichungulia wallet yake ina hela wekundu wa kutosha n.k. Nikimuomba hela za kuhudumia home anasema hana, nikamuuliza mbona kwenye wallet yako zipo akasema sio zake! Nikaanza kuhisi naibiwa mchana, nikabana uchumi pale home nikawa napika dona na mlenda, dagaa kwa sana basi jamaa baada ya muda akaanza kutoa hela kidogo kidogo.
Chukua hii nunua mchele na kuku! Hahaha kumbe dona na mlenda inachosha anyway nisiwachoshe, jamaa baada ya kipindi cha miezi kadhaa jamaa akarekebika na tukawa tunaishi vizuri tu. Linalonileta hapa ni kuwa sasa mume wangu anataka tujenge wote nyumba kwenye kiwanja chenye jina lake. Jamani naingiwa na ubaridi. Inakuwaje hapa? Ukizingatia background hiyo hapo juu, huyu mtu kabadilika kweli?
Najiuliza sasa tena tujenge wote kwenye kiwanja chake? Pia mwenzangu ana watoto 4 mie nina wawili, hii inakuwaje? Mama wa watoto hawa yu hai na ana uwezo tu kwanini mie nijinyime nijenge kujengea wanne na baba yao? Jamani nakuwa na roho ya kichoyo au nakaribia kuibiwa mchana? Nimejaribu kuzungumza na mume wangu kumwambia japo tutafute kuwanja cha pamoja tujenge huko ila akahamaki na kuanza kunishutumu nina roho mbaya. Ni sawa mie kujenga nae hapo?
Naomba ushauri