Naomba ushauri: Mume wangu ananiachia majukumu

Naomba ushauri: Mume wangu ananiachia majukumu

1. kosa la kwanza ni 'kuoana' badala ya wewe kuolewa na yeye kukuoa,
2. Pili, kama anataka mjenge nyumba ya familia basi ni vyema hiyo hati ya kiwanja iwe na 'joint ownership' yaani mkabadilishe ili rohoni mwenu na nje kwa watu wote na objectively ijulikane ni mali yenu. Kama akikataa, basi mpango huo inabidi uwe hadithi kwani huyo jamaa na hayo majibu yake hamtafika mbali.
mmh hujui tu namna ngoma inavyo wambwa....ukishiriki siku moja utaelewa cha kuongea kwenye ngozi hii.
 
Huyo aliozaa nae una ndoa naye? mmefunga ndoa? Kama wewe ni mke wa ndoa jengeni nyumba acha mambo ya ajabu. Mimi nimeoa na kabla ya kuoa nina watoto wawili nimezaa na wanawake tofauti, ila mi na mke wangu tumeamua kujenga nyumba ya kisasa mjini na tumekubaliana yeye alishe familia na matumizi ya kawaida kama umeme na maji mimi nikomae na ujenzi. So zingatia nyie mnachofanya na mlichokubaliana na pia hicho kiwanja tunachojenga nilinunua bado nipo chuo so kina jina langu.

Mghosi
 
Binafs nakuona hujui wajibu wako na hujui kuwa kama upo ndani ya ndoa,mambo yote hayo uliyaona kabla hata hujafunga ndoa...sasa kipya hapo ni kipi??sasa nyie ni mwili mmoja hakuna cha kwako wala chake..vyenu wote
 
Apo no kukaa chini na mumeo na kuyazua tofauti zenu in positive and negativite way.
 
1-anza kuwa na msimamo kwa kumfanya mumeo awajibike kwa nafasi yake kama baba na mume ktk familia kwa kutoa mahitaji kwa kadiri ya uwezo wake. Akisema hana na wewe sema huna, wanunulie watoto chips na waambie baba yao akirudi wamlilie njaa.
2-mkubarie ombi lake ila muwekee masharti kuwa kwa kuwa nyinyi ni mwili mmoja na kuna leo na kesho, mbadilishe kwanza jina ili na wewe uwe sehemu ya umiliki wa hicho kiwanja au hiyo nyumba inayotaka kujengwa ili hata kama kesho na kesho kutwa bahati mbaya umetangaulia, ndugu lawana wasiweze kukupora haki yako.
 
Wanaume siku hizi ni wachache sana aisee....

Inakuwaje unakula tu bila hata kushtuka.....

Wakati wanaume wa enzi za Asprin akikuta umeleta gunia la mchele tu inabidi ujieleze....maana anjua majukumu yake

Hapo hata wakianza ujenzi kuna dalili huyu dada ndie atakayejenga....mwanaume atanyuti tuliiiiiiiiiiiiiiiii

Kuna haja ya kupeleka wanaume wa kizazi hiki jandoni...porini hukooooo wakafunzwe
Hahahahahahaa wife bhana.... khaaa!!
 
Mwambieuna hela ya kula ya kujenga huna, full stop. Watu mnaopenda Shidaaah!!
 
anakiita "chetu" but ni "chake" legally! La sivyo mbona hataki kukiweka "chetu" kimaandishi?

Mi wangu alibadili umiliki bila hata ugomvi. Ni vizuri muamue hizo fixed assets zikawa na umiliki wa pamoja. Inaleta incentive ya kila upande kuinvest pesa yake. Hata mkinunua mali nyingine mnamiliki pamoja na warithi wanaandikwa. Kubadili mbona siyo kazi kubwa?

Tatizo naona linakuja kwenye warithi. Sidhani kama kuna ke au me atakubali warithi wawe watoto wasiokuwa wake wa kuwazaa. Hapo ndipo joint ownership inapokuwa ngumu aisee.
 
1. kosa la kwanza ni 'kuoana' badala ya wewe kuolewa na yeye kukuoa,
2. Pili, kama anataka mjenge nyumba ya familia basi ni vyema hiyo hati ya kiwanja iwe na 'joint ownership' yaani mkabadilishe ili rohoni mwenu na nje kwa watu wote na objectively ijulikane ni mali yenu. Kama akikataa, basi mpango huo inabidi uwe hadithi kwani huyo jamaa na hayo majibu yake hamtafika mbali.

Nakubali angeolewa badala ya kuonana. Sasa hiyo ya pili kwanini wajenge wote? Ukishaolewa wewe mwanamke maana yake uzae na kulea watoto tu. Mume ndio ahusike kuhudumia familia ikiwa pamoja na kuhakikisha wanayo makazi ya kuishi.
You cant get both ways.
 
Inaonekana kakufananisha na mchepuko wake eeh? Hahaha
Yani wewe ndo umenishangaza zaidi.... Hivi sasa ni saa ngapi kwa saa za Afrika Mashariki??

Huku Bosnia ndo tunaenda pata lunch ya asubuhi.
 
Mi wangu alibadili umiliki bila hata ugomvi. Ni vizuri muamue hizo fixed assets zikawa na umiliki wa pamoja. Inaleta incentive ya kila upande kuinvest pesa yake. Hata mkinunua mali nyingine mnamiliki pamoja na warithi wanaandikwa. Kubadili mbona siyo kazi kubwa?

Tatizo naona linakuja kwenye warithi. Sidhani kama kuna ke au me atakubali warithi wawe watoto wasiokuwa wake wa kuwazaa. Hapo ndipo joint ownership inapokuwa ngumu aisee.
Unawezaje kubadili hati ya kumiliki kiwanja kwa mfano?
 
Yani wewe ndo umenishangaza zaidi.... Hivi sasa ni saa ngapi kwa saa za Afrika Mashariki??

Huku Bosnia ndo tunaenda pata lunch ya asubuhi.

Nabandika makongoro mwenzio wateja wa supu wasitindikiwe.
Duh usingizi umekata aisee, imebidi nigeuke mzungu wa nne The Boss asishtukie mwanga wa simu
 
Last edited by a moderator:
Nabandika makongoro mwenzio wateja wa supu wasitindikiwe.
Duh usingizi umekata aisee, imebidi nigeuke mzungu wa nne The Boss asishtukie mwanga wa simu
Kheee.... kama huna power bank, kesho nisipokuona hapa ntakunywa sumu. Ole wako uje kunizika.
 
Mapenzi ya siku hizi bwana yamekaa "kimachale machele" ukifumba tu macho umeibiwa...
back to topic, tengeneza mazingira , mshauri mumeo mnunue kiwanja kisha muandike jina la mtoto wenu kisha mjenge pamoja.
hicho chake mwambie atajenga tu mkimaliza hiyo nyumba ya familia.
Yupi? Hiyo ni sumu maana akisuggest jina la biological child wa wote mume atanuna kuwa anawatenga wale wa kufikia; wakiweka wa kwanza mama (usisahau kuwa mtoto ana definition tofauti kati ya me na ke, kwa mama ni yule aliyemtoa katika k yake na mtoto kwa baba ni yule aliyetokana na s.perm yake) hivyo ataona kama anamnufaisha mwanamke mwenzie siku za usoni. Nikupe mfano hai, kaka yangu kaoa ile ndoa naita mseto na mke wake wa milimani. Walinunua kiwanja wakaweka majina ya wote wawili, ila ndugu wa mke wakija wanamweleza shemeji yao kuwa ni nyumba ya dada. Sie tunabaguliwa kuwa tunadandia katika nyumba ya dada yao mpaka hata hamu ya kwenda kwa ndugu yetu hatuna. Ukimweleza mke wa kaka yeye anadai ndugu zake ndivyo walivyo. Familia hizi zina mengi
 
Back
Top Bottom