Naomba ushauri: Mume wangu ananiachia majukumu

Naomba ushauri: Mume wangu ananiachia majukumu

Nakubali angeolewa badala ya kuonana. Sasa hiyo ya pili kwanini wajenge wote? Ukishaolewa wewe mwanamke maana yake uzae na kulea watoto tu. Mume ndio ahusike kuhudumia familia ikiwa pamoja na kuhakikisha wanayo makazi ya kuishi.
You cant get both ways.

Mwanamama amekwishatoa sabubu za msingi za kujenga wote ili kuepusha matatizo mengi yanayowakumba watoto endapo ndoa zinavunjika au baba anapoondoka duaniani. Kujenga wote ni security yake na watoto wake.
 
Tobaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!! usikubali hata, ajenge tu mwenyewe, wanaume wenye gubu aiseee utajutia na utaacha hiyo nyumbaa, mamaweeeeee usikubali kabisaaa, hapo hamna mwanaume. kumpenda mtu sio sababu yakua mtumwaa, utajutaa wewe dada, kweli nakuonea hurumaa.
 
Nakubali angeolewa badala ya kuonana. Sasa hiyo ya pili kwanini wajenge wote? Ukishaolewa wewe mwanamke maana yake uzae na kulea watoto tu. Mume ndio ahusike kuhudumia familia ikiwa pamoja na kuhakikisha wanayo makazi ya kuishi.
You cant get both ways.
Nakuunga mkono. Mia kwa mia hizi dhana za kuchanganya uchumi baadala ya kupangiana majukumu zina madhara lukuki. Mama angeangalia masuala ya msosi na baba akaangalia masuala ya ustawi wa familia ikiwa ni pamoja na suala la ujenzi wa nyumba.
 
Unawezaje kubadili hati ya kumiliki kiwanja kwa mfano?

kama unaulizia procedures... ofisi za ardhi kuna forms wanakupa za kujaza, kuna documents/ vithibitisho pia watahitaji. Ni kama unavyobadili umiliki mfano kama umenunua kiwanja/ nyumba kutoka kwa mtu mwingine.
 
habari zenu,

ni hivi nimeolewa, mume wangu ana watoto 2 kabla ya ndoa yetu nasi tuna watoto wawili. Wote ni waajiriwa nje ya jiji la dsm. Baada ya kuoana tukaanza maisha nikajikuta naachiwa majukumu ya kutunza nyumba. Jamaa kila nikimuuliza anasema hana hela na haishi sababu ambazo mimi zikawa zinanitia shaka. Nikavumilia nikawa natoa hela maisha yanakwenda kama kawaida pale home.

Ikafika kipindi nikaamua kuchunguza kweli hana hela? Nikawa nakuta deposit slip jamaa ana deposit hela kwenye account yake, nikichungulia wallet yake ina hela wekundu wa kutosha n.k. Nikimuomba hela za kuhudumia home anasema hana, nikamuuliza mbona kwenye wallet yako zipo akasema sio zake! Nikaanza kuhisi naibiwa mchana, nikabana uchumi pale home nikawa napika dona na mlenda, dagaa kwa sana basi jamaa baada ya muda akaanza kutoa hela kidogo kidogo.

Chukua hii nunua mchele na kuku! Hahaha kumbe dona na mlenda inachosha anyway nisiwachoshe, jamaa baada ya kipindi cha miezi kadhaa jamaa akarekebika na tukawa tunaishi vizuri tu. Linalonileta hapa ni kuwa sasa mume wangu anataka tujenge wote nyumba kwenye kiwanja chenye jina lake. Jamani naingiwa na ubaridi. Inakuwaje hapa? Ukizingatia background hiyo hapo juu, huyu mtu kabadilika kweli?

Najiuliza sasa tena tujenge wote kwenye kiwanja chake? Pia mwenzangu ana watoto 4 mie nina wawili, hii inakuwaje? Mama wa watoto hawa yu hai na ana uwezo tu kwanini mie nijinyime nijenge kujengea wanne na baba yao? Jamani nakuwa na roho ya kichoyo au nakaribia kuibiwa mchana? Nimejaribu kuzungumza na mume wangu kumwambia japo tutafute kuwanja cha pamoja tujenge huko ila akahamaki na kuanza kunishutumu nina roho mbaya.
ni sawa mie kujenga nae hapo?

naomba ushauri
kwanza kabisa nakupa pole sana kwa yote,hayo ni mapito ya kimaisha yakupasa uyashinde na sio yakushinde wewe, cha msingi ni kusugua goti kwa mungu,

nakushauri uwe unatenda kwa busara,maana busara ndio itakayo itengeneza ndoa yako,memewako atavutwa na busara yako na kubadilika,ukiitumia busara vyema,delila alimteka samson kwa busara na si kwa maguvu au ujinga,mwombe mungu hekima,
 
Wasiwasi ndio akili ujue!maisha ya kuliana timing hakuna ndoa hapo wala muunganiko ukijichanganya imetafuna upande wako
Hapo ni kuishi kisungura ukifumbua macho ndo umelala.
 
mwambie aanze kujenga wewe huna hela, may be wakati wa finishing utachip in
 
Mimi mke wangu kaniambia anajenga kwao.nikamwambia akifika usawa wa lenta aniambie nimsaidie kuweka paa akashangaa.
 
Shoga jenga ila simamia ujenzi risiti zote piga jina lako utunze siku akimwaga ugali mwaga mboga kuwa wewe ni mwenye nyumba
 
Mhh.. Huu uzi tuwaachie akina miss chagga.. Wanaune tukitoa ushauri tutamponza mwenzetu
 
Mambo ya ndoa raha sana, hasa mwanamke akiachiwa kucontrol familia (kwa kiburi chake) huwa ameonewa na kuhisi kunyanyaswa. Nadhani ushauri wako hakuzingatia maelezo ya upande wa pili ingawa unaweza kuwa sahihi hata kama huna au sina uhakika.

kuna maswali mengi sana ya kujibiwa kabla ya kuanza kushauri kwenye swala hili, je kabla ya kuamua kuishi pamoja taarifa hizi za watoto wa nje ya mahusiano yao zilikuwepo? inahusu alizipokeaje?

Nini makubaliano ya awali kati yao? Isije kuwa inahusu alichangia kuvunja nyumba ya mwanamke mwenzie na sasa uhalisia wake unajidhihirisha kwamba hakuwa na utayari wa kuishi na hao watoto wa mumewe. Nahisi pia kuna uwezekano wa inahusu kumzidi kipato mumewe! na ni ile type ya wadada wanaojifanya kutojali kupanga maswala ya familia na mumewe hasa yanayo husu kipato na matumizi.

Ni rahisi mwanaume kugaili pale anapohisi mkewe anataka kuwa incharge wa kila kitu, anaweza kudhani alibana matumizi na mlenda ugali umemuadabisha mume kumbe nae mume alikuwa anasubili mkewe akwame ili mchango wake uthaminiwe?. Wanawake wana sura nyingi sana za kibaguzi hasa wanapokuwa kwenye ndoa zenye watoto wa mwanamke mwingine kabla yao.

Hivi amu unajua kwamba wanaume huwa ni nadra sana kuwabagua watoto wa wanaume wenzao? labda kama mke atajaribu kutumia nguvu nyingi au upendeleo wa wazi kwa wanae. Nimeona mengi wacha ninywe bia tu weita ongeza moja baridi huku.

Naomba nijibu hoja:
Nilifahamu kabla ya ndoa kuwa kuna watoto wengine na niliambiwa watakuwa wanaishi na mama yao as mama yao hataki kuwaachilia. Ila moyoni nilijiwekea kwamba vyovyoye vile ni sawa wakija kuishi na baba yao au waishi ma mama yao.
Mkuu sikuvunja ndoa ya mtu, nilikuta wameachana na niliomba uthibitisho wa kimaandishi kabla sijaanza uhusiano. Alinionyesha hati (sijui inaitwaje) ya talaka inayotolewa na mahakama.
Mkuu mume wangu ananizidi kipato na sio mie ndo namzidi. Haikujalisha, nilishare nilicho kuwa nacho. Lakini kila nikitoa nikawa naona mwenzangu ndo anazidi kubana
Namheshimu mume wangu kadri niwezavyo na sina mipango ya kushindania kuwa mwanaume!
Ila nina swali..
Unavyosema ni nadra kwa mwanaume kubagua watoto wa mke, hebu let us reverse the situation:
suppose mke ndo angekuwa na watoto 2 kwenye previous ndoa then mkazaa 2 pamoja kisha akakwambia mume wangu tujenge kwa pamoja kwenye kiwanja cha mke ungekubali hata kama mkeo anakuzidi kipato? Na mwanamke huyo basi iwe hela zake huzioni pale home?! Easier said than done mkuu!
Naomba niseme binadamu wana tabia tofauti including wabinafsi, wachoyo na wapenda kutumia wenzao huku wenyewe wakiendelea kula maisha na kutamba mtaani. To me hakuna justification ya mwanaume mzimaaa mwenye kipato kuficha hela na kutegemea wife ndo akulishe.
 
Dadangu, akili kichwani!

Kimsingi ata mkijenga kwenye kiwanja chake, bado mali hiyo itakuwa yenu wote, wewe na yeye, kama mali za ndoa.

Hivyo mtakapoachana(ikitokea), hiyo nyumba itakuwa ni miongoni mwa vitu mtakavyogawana.

Kuhusu watoto wako kukosa nyumba hii itategemea labda nyie au wewe(Mungu aepushie mbali) mkifa kabla, then mirathi huku nyuma huwezi jua itakavyoamuliwa. Kama msingi wa hofu yako ni wanao basi komalia kiwanja hicho muandike majina ya wanao hao, then itatoka kuwa mali yenu na itabaki kuwa mali ya hao watoto.

Na ata ukijenga kwenye kiwanja cha jina lako, bado mali hiyo itabaki kuwa yake pia, maana kiswahiliswahili sio rahisi muandikiane mikataba kuwa hahusiki chochote hapo.Akiamua kuifuatilia mtasumbuana tu.

Ndio maana kama upo kwenye mahusiano ya kindoa ya mguu ndani-mguu nje ni risk sana kuandika mali kwa jina lako, huyo mchwa atapata ata asipochuma.
 
Pole sana wandugu, mimi mwenyewe wa kwangu ananifanyia hivyo nikaamua ili kuleta uwajibikaji ikabidi tugawane majukumu kwenye familia, mimi nikamwambie kipato changu nielekeze kwenye ujenzi na yeye alishe familia maana nilijiona nachukua jukumu zito la kulea familia at the same time kusave pesa kwa ajili ya ujenzi.
 
Habari zenu,

Ni hivi nimeolewa, mume wangu ana watoto 2 kabla ya ndoa yetu nasi tuna watoto wawili. Wote ni waajiriwa nje ya jiji la DSM. Baada ya kuoana tukaanza maisha nikajikuta naachiwa majukumu ya kutunza nyumba. Jamaa kila nikimuuliza anasema hana hela na haishi sababu ambazo mimi zikawa zinanitia shaka. Nikavumilia nikawa natoa hela maisha yanakwenda kama kawaida pale home.

Ikafika kipindi nikaamua kuchunguza kweli hana hela? Nikawa nakuta deposit slip jamaa ana deposit hela kwenye account yake, nikichungulia wallet yake ina hela wekundu wa kutosha n.k. Nikimuomba hela za kuhudumia home anasema hana, nikamuuliza mbona kwenye wallet yako zipo akasema sio zake! Nikaanza kuhisi naibiwa mchana, nikabana uchumi pale home nikawa napika dona na mlenda, dagaa kwa sana basi jamaa baada ya muda akaanza kutoa hela kidogo kidogo.

Chukua hii nunua mchele na kuku! Hahaha kumbe dona na mlenda inachosha anyway nisiwachoshe, jamaa baada ya kipindi cha miezi kadhaa jamaa akarekebika na tukawa tunaishi vizuri tu. Linalonileta hapa ni kuwa sasa mume wangu anataka tujenge wote nyumba kwenye kiwanja chenye jina lake. Jamani naingiwa na ubaridi. Inakuwaje hapa? Ukizingatia background hiyo hapo juu, huyu mtu kabadilika kweli?

Najiuliza sasa tena tujenge wote kwenye kiwanja chake? Pia mwenzangu ana watoto 4 mie nina wawili, hii inakuwaje? Mama wa watoto hawa yu hai na ana uwezo tu kwanini mie nijinyime nijenge kujengea wanne na baba yao? Jamani nakuwa na roho ya kichoyo au nakaribia kuibiwa mchana? Nimejaribu kuzungumza na mume wangu kumwambia japo tutafute kuwanja cha pamoja tujenge huko ila akahamaki na kuanza kunishutumu nina roho mbaya.
Ni sawa mie kujenga nae hapo?

Naomba ushauri
Pole! Lakini sijui ndoa kwako ina tafsiri gani? Kwa kukusaidia rudini kanisani kwenu muanze mafundisho upya.
Lakini zaidi mimi sijawahi ona mali ya baba ninachojua mimi kuna mali ya wanandoa mliyochuma pamoja ambayo ndio hiyo mnayoenda kujenga (maana kiwanja si lazima mtatoa hela mnunue) na mali ya mama tu. Mali Ya baba huwa tunatoka nayo pasu pasu au zaidi kama una ndoa yenye cheti cha Serikali kinachoashiria ndoa ni ya mke mmoja.
Cha kusikitisha huwa hatusomi vile vyeti vyetu vya ndoa tukishafunga ndoa tunaviweka tunasubiri siku ya mtifuano wanasheria watusaidie kutafsiri. Ebu jipe muda kisome leo.
Alafu usiwe na mashaka na hao watoto wake wala wangine atakaoleta ebu kumbuka Mungu alimwambia nini ibrahim kuhusu mtoto wa Hajar! (kama wewe ni mkristo) na hili ni kwa dini zote. Mtoto wa nje ya ndoa harith ila kilichopo ni ubinadam tu unaofanyika ili kusaidiana.
Na wewe pia kwa vile uliwakubali watoto wewe muhimize awasomeshe wawe na muelekeo huko baadae utapata thawabu lakini pia utaondokana na usumbufu kawaida migogoro mingi chanzo ni umaskini wa akili.
Ninachokiona kwenye maelezo yako hujiamini na mwenzio hajiamini na hii ni kwa sababu ya tabia za wanawake wengi kulazimisha ndoa ndio matokeo yake hayo mko desparate mnataka ndoa mwanzoni mnakua tayari kwa lolote lakini kumbe moyo wa kubeba mizigo hiyo hamna matokeo yake mnaanza kulalamika.
Kama mngeoana kwa upendo na si kutaka ndoa upendo huwa una tabia zake "upendo huvumilia, hauhesabu mabaya, husitiri. ........" mmeshakua mwili mmoja hayo mengine achana nayo acha kuishi kwa wasiwasi. soma biblia yako vizuri.
Mwisho mwanamke simama katika nafasi yako ukiamini ulipo haupo kwa bahati mbaya upo hapo kwa sababu Mungu anataka uwepo. Jenga na mume wako kama bado hujiamini ukinunua vifaa wewe andika jina lako kwenye risit piga copy hifadhi kuonyesha mchango wako ingawa hata kumpikia, kumfulia hata kumpa pole akitoka site ni mchango tosha na utapewa haki yako.
Zaidi kama wewe ni mkristo chukua bible yako soma Mithali 31 yote uone wajibu wa mwanamke katika nyumba alafu ujiulize je umetimiza hayo?
Kila laheri be positive kanisa lipone.
 
Mmmh... kujenga nae sio kwa dalili hizo.
Kashaonesha dalili mbaya, Pole sana.
 
Back
Top Bottom