Naomba ushauri kuhusu kununua gari aina ya SUZUKI LANDY

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
801
546
Wakuu habari za jioni!

Leo nilikuwa naperuzi kwenye mtandao nikakutana na hii gari aina ya SUZUKI LANDY. Kwa ufupi nimeipenda na nikasema nijichange hadi kufikia mwakani niinunue. Lakini cha kushangaza, hizi gari tanzania hazipo nyingi. Gari ina 1990cc na inatumia mafuta ya diesel lita moja inaenda Km 12 -16. Ina seat 8 na ina milango mitano. Naomba kujua matatizo ya hii gari ni nini hadi watu hawapendi kuzinunua? Nimeweka na picha yake hapo chini.
 
Attachments

  • Screenshot_20221020-195014~2.png
    Screenshot_20221020-195014~2.png
    98.4 KB · Views: 57
Haya magari mengine jaman tuziheshim sana hela zetu, ni hela ngumu sana ku risk huku.

Haya magari mengine jaman tuziheshim sana hela zetu, ni hela ngumu sana ku risk huku.

Nimeogopa kabisa gari unique. Jamaa yangu alipata ajali ndogo (aligonga gari lingine kwa nyuma), imemgharimu sana. Spare za kutafuta sana na zikipatikana ni ghali mno.

Rejeta ilipasuka ule uwanda wa juu. Katafuta spare ya kubandika kakosa wakati za toyota zimejaa 30k hadi 50k. Imebidi aagize rejeta complete.

Taa kakosa kote, kaja kuipata sehemu taa mbovu imechoka, imefifia sana, kainunua 1 kwa laki 4 ili apate lile jumba tu then kahamishia zile bulb za taa iliyovunjika. Bado mazaga mengine.
 
Haya magari mengine jaman tuziheshim sana hela zetu, ni hela ngumu sana ku risk huku.

Shukran sana mkuu kwa ushauri wako. Nimesoma huo uzi umenipa funzo
 
Alphard huwa naziona zipo chini sana halafu ni kama hazitaki shuruba na gharama za matunzo nadhani zitakuwa juu mno
Alphard zipo kawaida sana ila angalia km ina ule mustach kimbia itachakaa mapema kwa barabara mbovu
 
Nimeogopa kabisa gari unique. Jamaa yangu alipata ajali ndogo, imemgharimu sana. Spear za kutafuta sana na zikipatikana ni ghali mno.

Gari unique siku zote ni ujinga tu bro, usishawishike na kutaka kuwa tofauti ule ni mzigo wa miiba na utakufa nao gari ikianza kukusumbua, yaani utalia peke ako.

Na hakunaga kitu inauma kama unatafuta spea madukani unaulizwa ni ya gari gani..? Ukitaja jina la gari yako wanakushangaa ndo gari gani?
 
"Fahari Baba wa Ujinga"
 
Back
Top Bottom