Naomba ushauri na mapendekezo kuhusu Suzuki Escudo old

Vangiporini

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
310
217
Wakuu habari ya muda huu,

Nimekuja mbele yenu nipate ushauri na mapendekezo zaidi kuhusiana na gari aina ya Suzuki Escudo old model.

Mimi napiga sana mihangaiko ya vijijini mashambani ambako ni 100% rough road. Kulingana na mazingira hayo nilitamani gari yenye spec zifuatazo;

iwe juu na iwe imara
iwe na ulaji mzuri wa mafuta angalau 10km/l
iwe na 4WD au hata AWD

Sasa kulingana na vigezo hivyo nikawaza Suzuki Escudo old model maana naskia zina ulaji mzuri wa mafuta naskia zinafika hadi 12km/l, pia nasikia 4WD yake ni balaa. Japo nasikia zina changamoto ya bodi kuingiza vumbi ndani. Nina mpango wa kuchukua mkononi na bajeti yangu ni 6m max.

Awali niliwaza kuhusu Rav4 old, changamoto ikawa ni ulaji wa mafuta maana naona nyingi zinaenda 7km/l sasa kwa mizunguko yangu nikaona haitanifaa japo sifa nyingine inazo.

Naombeni ushauri wenu kama nipo sahihi kwa chaguo hilo na kama kweli escudo old ina sifa hizo na pia kama kuna mbadala tofauti na hiyo escudo old kwa bajeti hiyo ya 6m mkononi. Asanteni.
 
G16 engine
Screenshot_20231107-182426_1.jpg
 
Sasa kama G16 ikikushinda wewe ni wa kuendesha Suzuki Swift tu maana hamna namna ingine. Kila gari ina zama zake, kwa zama za hio gari ilikuwa ni fuel efficient sana.

Nadhani ilikuwa ina average ya 9-10 km/l wakati magari mengi yakiishia 7km/l ila kwa namna teknolojia imekuwa na maboresho mengi kwenye magari sahizi gari nyingi zenye uwezo sawa na hio escudo zinapata zaidi kati ya 10-15km/l.

Kwa sasa suzuki vitara ya generation ya 4 toka 2015 yenye 1.6L engine inatumia 17-18Km/l very efficient.

Ila kwa mtu anayeanzia maisha ni gari nzuri ya kuanzia life.
 
vitara ipi iyo mkuu? ebu picha
 
Back
Top Bottom