Naomba ufafanuzi kuhusu ulazima wa mwalimu kulipia mchango wa Mwenge

Duduvwili

JF-Expert Member
Jan 31, 2015
3,884
3,807
Wakuu, sina haja ya kuwasalimia kutokana na mvurugo bila kusahau matusi ya Mkuu Mpwayungu naomba kuuliza wajuvi hivi mwalimu akishindwa kuchangia mchango wa MWENGE ambao ni shilingi elfu tano katika halmashauri hii anakuwa amemkosea nani kwa sababu naona ni wazi tunatafutana lawama. Kuna wananchi wengi tu lakini hawabanwi, why Walimu?

Mikwara miiingi mara majina sijui yanatumwa kwa mkuu wa wilaya kwa wasio changia mwenge kwa Nini mnatulazimisha kama ni lazima si muwe mnakata hukohuko kabla mshahara haujatoka?

Binafsi sioni mantinki naona ni uonevu wa Hali ya juu mwalimu amekua ndio jalala la majanga huo mwenge wenyewe ukifika mwalimu hatambuliwi watu wanatafuna vyuku kwa michango ya walimu masikini Serikali tafadhali msituonee hivi kuweni na chembe ya huruma magoli mnanunua milioni20 mchango wa MWENGE unawashindaje?
 
5k kitu gani mkuu? Jifanye mjinga toa tu hiyo 5k halafu pita hivi. Japo siyo halali.
Kweli sio ishu lakini kwa Nini watuonee hivi? Uhalali upo wapi kama ni haki yao wangekua wanakata juu kwa juu kama makato mengine tungezoea mtu unakuta huna hiyo 5k halafu mbaya zaidi wanabana wilaya za machakani kwenye maisha magumu zaidi binafsi sintochangia.
 
Kweli sio ishu lakini kwa Nini watuonee hivi?uhalali upo wapi kama ni haki yao wangekua wanakata juu kwa juu kama makato mengine tungezoea mtu unakuta huna hiyo 5k halafu mbaya zaidi wanabana wilaya za machakani kwenye maisha magumu zaidi binafsi sintochangia

unadhani wanaochangia wajinga sio? Tatizo la nchi yetu linaanzia kwenye mifumo yake mibovu iliyowapa watu wachache amri juu ya wengine halafu hawagusiki.

Tukishindwa kubadilisha mifumo hiyo ni heri kujifanya mjinga siku ziende hasa kwenye mambo kama haya ambayo hayaumizi sana. Otherwise utaumia.
 
Kweli sio ishu lakini kwa Nini watuonee hivi?uhalali upo wapi kama ni haki yao wangekua wanakata juu kwa juu kama makato mengine tungezoea mtu unakuta huna hiyo 5k halafu mbaya zaidi wanabana wilaya za machakani kwenye maisha magumu zaidi binafsi sintochangia
Nadhani ungegoma kuchangia halafu uone watakufanya nini.
 
Usitoe hiyo hela, na hakuna kitu utafanywa ? Shida mnajengana hofu unaweza kukuta ni mchango wa Hiari ila sasa wakereketwa wanavyokua na hofu mpaka mnaanza kulazimishana. Naonaga pia wanalazimishwa kulala kwenye mkesha wa Mwenge au kuwepo eneo mwenge ulipo hadi wanaandikwa majina.

Karne hii watu wameshaelevuka sana, Mwenge umeshapoteza maana sasa sehemu ya kupata attention ni kwa watumishi wa Umma ndo wataongeza idadi ya watu ila bila hivyo wangekua wanahudhuria watu kidogo sana hasa watoto na watu wasio na kazi za kufanya au mtu awe ameamua tu maana kuna watu huwa wanapenda shamra shamra.

Vitu vyote vinaweza kufanyika bila hata huo mwenge kuwepo! Au ndo mazindiko.
 
Usitoe hiyo hela , na hakuna kitu utafanywa ? Shida mnajengana hofu unaweza kukuta ni mchango wa Hiari ila sasa wakereketwa wanavyokua na hofu mpaka mnaanza kulazimishana !! Naonaga pia wanalazimishwa kulala kwenye mkesha wa Mwenge au kuwepo eneo mwenge ulipo hadi wanaandikwa majina !
Karne hii watu wameshaelevuka sana ,Mwenge umeshapoteza maana sasa sehemu ya kupata attention ni kwa watumishi wa Umma ndo wataongeza idadi ya watu ila bila hivyo wangekua wanahudhuria watu kidogo sana hasa watoto na watu wasio na kazi za kufanya au mtu awe ameamua tu maana kuna watu huwa wanapenda shamra shamra.

Vitu vyote vinaweza kufanyika bila hata huo mwenge kuwepo ! Au ndo mazindiko.
Hhhahaha walim bhana dah
 
Wakuu, sina haja ya kuwasalimia kutokana na mvurugo bila kusahau matusi ya Mkuu Mpwayungu naomba kuuliza wajuvi hivi mwalimu akishindwa kuchangia mchango wa MWENGE ambao ni shilingi elfu tano katika halmashauri hii anakuwa amemkosea nani kwa sababu naona ni wazi tunatafutana lawama. Kuna wananchi wengi tu lakini hawabanwi, why Walimu?

Mikwara miiingi mara majina sijui yanatumwa kwa mkuu wa wilaya kwa wasio changia mwenge kwa Nini mnatulazimisha kama ni lazima si muwe mnakata hukohuko kabla mshahara haujatoka?

Binafsi sioni mantinki naona ni uonevu wa Hali ya juu mwalimu amekua ndio jalala la majanga huo mwenge wenyewe ukifika mwalimu hatambuliwi watu wanatafuna vyuku kwa michango ya walimu masikini Serikali tafadhali msituonee hivi kuweni na chembe ya huruma magoli mnanunua milioni20 mchango wa MWENGE unawashindaje?
Hoja za mkuu Mpwayungu Village zina mashiko kuhusu uelewa na uwezo wa waalimu
 
Hapa ndipo Mpyayungu anajichukulia pointi. Tatizo la walimu wanapenda kujipendekeza na kupata upendeleo kwenye kusimamia mitihani na visemina semina ndio maana wanakuwa waoga hata kwenye mambo mepesi.

Lakini kwa mwalimu ambaye anapata mshahara na anapambana nje ya kazi huwezi kumkuta anaogopa kutochangia mwenge kwa sababu hategemei kupangwa kusimamia mitihani kazi ngumu malipo kiduchu.

Usipochanga haufanywi chochote zaudi hizo hela zinaenda mifukoni mwa watu kwa sababu bajeti ya mwenge ilishatengwa kabla mbio hazijaanza. Labda hao makada ma-afisa elimu ndio wataacha kuwapa nafasi ya kusimamia mitihani mara moja kwa mwaka.

Hakuna kosa la kiutumishi ambalo utaadhibiwa kwa sababu ya kushindwa kuchangia mwenge. Kasome standing order upate maarifa mwl, acheni kujazana woga, hii nchi inawategemea nyie mlete mabadiliko!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom