Jiji la Tanga Lawabebesha Walimu Mzigo Wa Mwenge

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WAKATI utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano ukijinisabu kwamba, umejipanga kupunguza makali ya maisha kwa wananchi, kwa Jiji la Tanga mambo hayapo hivyo, anaandika Regina Mkonde.

Halmashauri ya Jiji hilo imepeleka ujumbe kwa walimu wote jijini humo kuchangia pesa kwa ajili ya kugharamia mbio za Mwenge. Mwisho wa kupokea michango hiyo ni tarehe 25 Aprili mwaka huu.

Ujumbe wa barua hiyo umeandikwa na Gwakisa Lusajo kwa niaba ya Dk. Wedson Sichalwe, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.

Barua hiyo imeelekeza kwamba, kila mwalimu anayefanya kazi kwenye jiji hilo anapaswa kuchangia Sh. 1,000 ambapo walimu wakuu kila mmoja ametakiwa kutoa Sh. 10,000.

Pia imeelekeza kuwa, pesa hizo zipelekwe kwa Rehema Said, Mratibu wa Mwenge wa Wilaya ya Tanga.

MwanaHALISI Online umemtafuta Sichalwe ili kujua uhalali wa walimu kuchangishwa fedha kwa ajili ya mbio za Mwenge jijini humo.

Sichalwe amekiri kutambua barua hiyo ya kuhitaji michango kutoka kwa walimu na kudai kwamba, ni jambo la hiyari.

“Lazima watu wajue kuwa, barua iliyotolewa haikuwa na lengo la kushinikiza watu watoe michango hiyo. Ni hiyari ya mtu, na ndiyo maana tulitoa kwa wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafisi na kampuni,” amedai Sichalwe.

Anasema, muhusika atakayepokea michango atatakiwa kutoa stakabadhi ili kuwahakikishia wachangiaji kwamba, fedha zao hazitatumiwa kinyume na makubaliano.

“Vile vile, haimaanishi kwamba ni michango ya fedha tu ndiyo inapokelewa, bali hata mwenye vifaa ambavyo vitasaidia kufanikisha shughuli yetu tunavipokea, kwa mfano mafuta ya gari na vyakula,” anasema.

Hata hivyo, Sichalwe ameshindwa kutoa ufafanuzi kuwa, kama ni mchango wa hiyari kwanini alipanga viwango vya kutoa kwamba, walimu wakuu watoe Sh. 10,000 na walimu wa kawaida watoe Sh. 1,000.

Amedai, michango hiyo ni kwa ajili ya ununuzi wa mahitaji ya wageni siku ya tukio ikiwemo chakula na mafuta ya gari kwa ajili ya usafiri.

Ametaja tarehe ya siku ambayo Mwenge utapokelewa jiji humo kuwa ni tarehe 4 Mei 2016 katika Uwanja vya Tunda Ua vilivyopo kwenye Kata ya Kilale na kwamba, tarehe 5 Mwenge utapelekwa visiwani Unguja.
 
Buku tu?! Changeni ... Lakini ingekuwa vyema kama tungekuwa tunachangia vitu vya msingi zaidi ya huu MWENGE. Sioni faida yake..!
 
Buku tu?! Changeni ... Lakini ingekuwa vyema kama tungekuwa tunachangia vitu vya msingi zaidi ya huu MWENGE. Sioni faida yake..!
utafiti huru nilioufanya ulioambatana na uchunguzi umebaini kwamba Hakuna mradi wowote uliozinduliwa na mbio za mwenge uliodumu japo kwa miezi 6 , hii ni kwa sababu ya LAANA KUTOKA KWA MUNGU inayotokana na watanzania kuabudu KOPO LENYE UTAMBI UNAOWAKA , na kulizungusha nchi nzima .
 
Nchi itangazwe kuwa na dini maana mwenge ina harufu hiyo. Utamulika vipi mipaka wakati una askari?
 
Mimi napenda kuuliza swali moja hapa kila siku huwa linanichanganya akili yangu kabisa!
-Ivi mfano mradi fulani ukiwekewa jiwe la msingi labda na waziri, je mwenge nao unaruhusiwa kwenda kufungua tena huo mradi?
-Mfano mradi wa barabara za juu Tazara ulivyofunguliwa na Rais je Mwenge nao unaweza kwenda pale kufungua?

Nauliza haya kwa sababu kuna mradi fulani ivi wa ujenzi wa bwawa huko kanda ya ziwa kuanzia mwaka 2007 hadi leo huwa unawekewa mawe ya msingi hadi kero!
Huo mradi ulianza mwaka Kati ya 2003/2004 lilijengwa na shirika fulani ivi pamoja na nguvu za wananchi na huo mradi ukakamilika kati ya 2006/2007.
-Mwaka 2007 Rais wa wakati huo JK alienda akafungua huo mradi na mabbomba ya maji.
-Mwaka uliofuata Mwenge nao Ukaenda kufanya kazi ileile iliyofanywa na Rais mwaka mmoja tuu nyuma.
-Mwaka 2013 Ulifunguliwa tena na mwenge wa uhuru kama mwendelezo wa mradi wa usambazaji maji japokuwa huo mradi haueleweki mpaka leo huku wananchi wa eneo husika washachangishwa buku 10 Kila kaya!
-Mwaka uliofuata tena eneo hilo hilo likatembelewa na mwenge ili kukaguliwa ilihali hata mkandarasi amepaki mitambo.
-Mwaka huu tena mwezi feb Waziri mkuu ndugu Majaliwa kipindi kaenda kwenye ziara mikoa ya shinyanga,simiyu,mwanza,kagera na kigoma aliweka tena jiwe la msingi katika huo mradi ambaoo umeshawekewa mawe ya msingi zaidi ya matatu huku ukiwa haufanyi kazi wala hauendelei.

Swali langu ni kwamba je hayo mawe ya msingi yanawekwa kwa maana gani maana mi huwa sielewagi hapo!
Je hizi siyo contradiction na matumizi mabaya ya pesa za umma katika kufanikisha hiyo misafara bila faida yoyote kwa wananchi?

MSAADA TAFADHALI HAPO
 
Kwa sababu ccm imewachukulia wananchi kama ndondocha fulani hivi , Mungu ameamua kuingilia kati , hayo maji hayatokuja kutoka milele , nipo humuhumu jf , baada ya miaka mitano utakuja kuleta ushuhuda .
 
~~~>>> Waalimu wameifanya kazi ya Ualimu kuwa kazi ya LAANA..

Ifike wakati serikali iachane na kuchukua wale Failure kuwa Waalimu..... Inaweza kuwafanya waalimu kutumia vichwa vyao sawa sawa.
 
Inawezekana kuna ka ukweli fulani maana kwa sasa mabomba yaliyokuwa yamefungwa na lile shirika hakuna hata dalili kulikuwa na bomba pale
Mweeeh
 
~~~>>> Waalimu wameifanya kazi ya Ualimu kuwa kazi ya LAANA..

Ifike wakati serikali iachane na kuchukua wale Failure kuwa Waalimu..... Inaweza kuwafanya waalimu kutumia vichwa vyao sawa sawa.
Sio kweli mimi ni mwalimu na sijawahi kufeli pia ni Graduate wa UDSM.
Vipi Polisi,Nesi,Magereza,Jeshi nk walifaulu kuliko walimu
 
Huo mwenge ni wa walimu peke yao au walimu ndo kada pekee ya kudhurumiwa na kuibiwa mchana kweupe?
 
Back
Top Bottom