"Naomba Shilingi ishuke ifikie 5,000 kwa dola?" Why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Naomba Shilingi ishuke ifikie 5,000 kwa dola?" Why?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Nxt Millionaire, Nov 5, 2011.

 1. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu mtazamo hasi (NEGATIVE PERCEPTION) wa baadhi ya watu, tena si wachache, ni wengi kweli pale mtu anapowaambia kuhusu Biashara ya ya Masoko ya Mtandao ama Network Marketing, au Multi LevelMarketing, Referral Business, Business of 21st Century, DirectSelling, Recession Proof Business, Nk.


  Katika kufanya utafiti nimekutana na watu maarufu duniani wakiwamo marais, wasomi wakubwa, wafanyabiashara wakubwa duniani ambao wameamua ama kuifanya ama kuipigia debe kwa nguvu zote kwa ni mkombozi pekee anayeweza kumtoa mtu katika maisha ya chini kabisa na hatimaye kumwezesha naye kumiliki si pesa za kutosha bali nyumba na usafiri wa maana, (angalia mfano wa Bw na Bi Kayombo) katika karne hii ya 21 ama Zama za habari (Information Age).


  Nimekuwa nikijiuliza watu hawa wengi wenye mtazamo hasi wanajua nini ambacho mtu kama Donald Trumpna Robert Kiyosaki hawajui? ama wanapesa nyingi sana kuliko Warren Buffet na Donald Trump? Pengine wana nafasi ama mamlaka kuubwa kuliko aliyowai kuwa nayoBill Clinton? Labda ni wasomi sana au wachumi kulikoPaul Zane Pilzer na Dr Charles King? au maarufu sana kuliko Robert Kiyosaki?


  Pengine wananafasi katika jamii yetu kuliko alizowai kuwa nazo mtu kama Juma Kapuya, au Mbunge wa Dodoma Mjini, ama alizonazo Mch Getrude Rwakatare, lakini ikiwa huna pesa kuliko Warren Buffet au Donald Trump, fikiri mara mbili juu ya fursa hii, ama hunayo au huna elimu kama Prof Paul ZanePilzer na Dr Charles King, tafakali, au hunazo au huna nyadhifa kama alizowahi kuwa nazo Bill Clinton, chukua hatua.  Afrika Mashariki kuna watu wasiozidi laki moja walioamua kufanya fursa hii, hawa ndio wanaofurahia kila siku inapotangazwa kuwa shilingi imeshuka thamani, je ni kwanini wanafurahia kushuka kwa shilingi? Jana nilikuwa naongea na dada Mmoja anaitwa Erika, yuko kwenye NWM kwa muda wa mwaka Mmoja na nusu sasa anasema, nami nanukuu, "Naomba shilingi ishuke kila siku, ifikie hata 5,000 kwa dola moja"
  Kwanini anasema hivi? Network Marketers dunia nzima wanalipwa pesa zao kwa Dola za marekani, yeye mwezi uliopita alilipwa dola 6.800 na ushee hivyo kama thamani ya shilingi ilikuwa sawa na 1,700 inamaana atakuwa na zaidi ya Tsh 11.5 Millioni, na mwezi huu anatarajia kupata zaidi ya dola 7,000, je si anasababu ya kuomba shilingi izidi kushuka? kwa nini? dola 6,800 x 5,000 (kama anavyoomba) = Milioni 34! kwanini Wanamtandao wasiendelee kuomba shilingi ishuke?

   
 2. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Jitahidi kuhamasisha utawapata wafuasi wasio na uelewa! Kama biashara na Network marketing ingekuwa rahisi jinsi unavyo portray basi kila mtu angekuwa tajiri dunia hii.
   
 3. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Aksante Mkuu, Sihamasishi, bali naeleza ukweli, kuukubalia au kuukataa ni juu yako, ni maamuzi yako binafsi, hatuwezi kuwa wote matajiri kwa sababu ya tofauti za mtazamo, ila tukibadili mtazamo lolote linawezekana.
   
 4. Lonestriker

  Lonestriker JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Economical nonsense!Akipata hizo hela 'nyingi' wakati kila kitu kimepanda at the same rate atabaki na nini?Ukiongezewa mshahara kwa Tsh.50,000 na matumizi yako yakapanda kwa 50,000,utabaki kuwa na net gain ya zero.
  Nilikuwa nampenda sana R.Kiyosaki,bought his pirated books,downloaded Pdf's of his books and mp3 cds,he makes making money sounds soo easy...then came the bombshell,the guy is a liar,inflated his networth,he was even sued by his fellow co-author.Easy come easy go...
   
 5. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  What about Bill Clinton, Donald Trump or Paul Zane Pilzer? je wote ni waongo?
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo Network Marketing ni ngumu sana theoretcally ni rahisi sana but in reality ni ngumu sana. na kwa nini network marketing kwenye bidhaa za wazungu tu? kwa nini isiwe katika bidhaa za mkonge wetu tunao zarisha? kwa nini isiwe katika kahawa yetu? kwa nini isiwe katika korosho zetu?

  Hii network marketing imebuniwa na wazungu kwa ajili ya wa africa but wazungu huwezi kuwaambia watafute watu 100 wawauzie bidhaa za foreve living.

  na zile story za mafanikio mnazo eleza watu ni danganya toto tu.
   
 7. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Niwie radhi M-pesa, nilipokujibu sikuangalia kama uliisoamvia mobile, ukiwa ktk pc isome tena, fuata links hizo uzipitie, najua utakuja na comments tofauti na hiyo.
   
 8. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Komandoo, I agree with you 1000%, NM ni ngumu sana, kuliko kupata kazi ya kima cha chini serikalini, kusaini mahudhurio na kusubiri mwisho wa mwezi, ama kulima huo mkonge, ni ngumu sana.
  Labda ni kazi au biashara gani iliyorahisi sana hapa duniani? Sijui, kama wajua, tujuze.

  Network Marketing ni Ngumu sana, But its worth it! I can assure you, I've done my due diligence, you can do yours, sijui wasema wazungu wapii, ila marekani hivi sasa wametengeneza mtaala na unafundishwa vyuo vikuu, why? think twice!

  Nina materials na vitabu naweza ku-share na wewe kuhusu hii, (ikiwa sio mvivu wa kusoma kama Watanzania tunavyosifika) kwa miaka miwili niliamua kuitafiti hii, naongea kutokana na utafiti wangu, hiyvo nina uhakika asilimia 100 kile ninachosema, kwani "No research no Right to speak" nitwangie ikiwa wataka hayo materials 0784475576
   
 9. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lonestriker, I can assure you Network Marketing ni ngumu saana, pengine 200% au zaidi ya shughuri za kawaida, ikiwa unataka kufanikiwa ni lazima ujitoe kikweli kweli, si shughuri ya kufanya mtu anayetaka utajiri wa haraka haraka, bali fanya kama hobby au kama wapenda kusaidia wengine, utaifurahia, lakini kinyume cha hapo ni NGUMU SANA, BUT ITS WORTH IT!

  Ukiwa katika pc, zisome vyema links mbalimbali ambazo nimeambatanisha, ukishazipitia nipe maoni yako, I can share with you more materials if you want, just PM me.
   
 10. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Hapo kwenye RED, Network Marketing ni mfumo tu, yeyote anaweza akatumia kusambazia bidhaa zake, iweni hizo kahawa au mkonge, si ya wazungu, kinachofanyika ni kuondoa kila aina ya matangazo ya biashara na fedha hizo zinarejea kwa wale wanaosambaza taarifa kwa wengine juu ya ama huduma au bidhaa, kampuni au mtu yeyeto anaweza kufanya hivyo, rejea POST yangu katika www.winnersstreet.com juu ya mfumo huu.

  Hivi ushawai kufikiria Makampuni ya simu au soda yanalipa fedha kiasi gani kwa matangazo? fikiria gharama ikiondolewa na badala yake ukapewa weye asilimia ndogo tu kwa kumwambia mtu anywe soda ama atumie mtandao fulani, na kisha kampuni husika ikupe wewe sh 100 katika kila mtu atakapotumi 1000 katika kampuni husika, je utawaambia watu wangapi kwa siku, mwezi au mwaka? Tafakari, chukua hatua.
   
 11. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  We millionea Una ushamba ule wa utoto, enzi zetu tulivyokuwa watoto ukipewa buku unaenda kulichenji ili nazo nyingi!! coins kibao mfukoni!! sasa sijui mwenzetu bado upo utotoni ama Ndoto zako za alinacha zinakusumbua!! shilingi kila inavyoshuka tanzania wananchi vilio. kilo ya unga wa ngano unaijua bei yake lakini ama unaomba tu shilingi ishuke?? Siwezi kukuita pimbi ila hapo kidogo umepotea!!
   
 12. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Unapofikiria kuongeza kipato, fikiria na matumizi. If 34m pcm ni loads of munnie now. Vipi ikiwa inflated kama zimbabwe??? Hivi kuna mabilionea wangapi? Halaf hata mkaa hawana pa kuupata, na wakiupata wanatumia milioni kuununua?

  Nb: mod hebu regulate links attachments bana, naona watu wanatangaza tu humu bila kulipia.


  If its too good to be true, then it probably is.
   
 13. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nashukuru Kitope, huo ni mtazamo wako, nilichokiandika ni FACTS, kama wakubali au wakataa huo ni uhamuzi wako, Bali waweza kujiunga na kina Kayombo, Erika, na wengine wengi kufurahia shilingi kushuka ama kukaa na kulaumu serikali kila dola inavyopanda, The choice is yours!
   
 14. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 15. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Hapo kwenye RED Naamini hapa si mahali pa porojo tu, bali na kuelimishana pia, JF is where we dare talk openly, for Great Thinkers, Be Great thinker too,
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nakupa hi kwa uvumulivu mkuu, maana kila uki-post habari za milele living unapata changamoto nyingi zaidi. Jitahidi kaka uko kazini.
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Sijui kuhusu networking bussiness but najua wapo watu wanafaidika na kushuka kwa thamani ya pesa
  na wangetamani ishuke zaidi......
  kama main bussiness yako ni ku export basi pesa ikishuka unapata faida zaidi

  ndo maana Japana huwa wanashusha thamani kwa makusudi pesa yao
  ningekuwa nina kiwanda na nina export bidhaa europe ningefurahi pesa kushuka thamani...
   
 18. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hujui usemacho ila unajaribu kuwa win watu waingie kwenye biashara ambapo inaonekana hata wewe umebaki kuandika tu ila imekushinda, kama unajua basi umesimuliwa au umehudhuria hizo wanazoita presentation za hao walioko kwenye mitandao... nikwambie ukweli wa hiyo biashara. Ni rahisi kuongea na kujaribu kuwashawishi watu ila si rahisi kuifanya, ongea na watu walioifanya na wako wapi usilinganishe na matajiri ambao ninauhakka hawajatajirika kupitia biashara hiyo
   
 19. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Isome vyema hii thread, kuwa GT, usiwe mvivu wa kusoma, nilichokiandika nimekitafiti kwa miaka miwili, kwa makusudi kabisa hivyo naandika ninachokijua kwa theoretically and practically, Ndio maana nikauliza Why most people are so NEGATIVE about MLM? bahati mbaya hakuna aliyejibu maswali katika hii thread, bali kushambulia mleta thread, Tell me, ni kweli una wadhifa kuliko aliwai kuwa nao Bill Clinton, Je ni Mfanyabiashara mkubwa au Billionaire kuliko Warren Buffet, Donald Trump au Robert Kiyosaki, au u msomi sana kuliko Prof Paul Zane Pilze au Dr Charles King???

  Wewe wajua nini kuhusu Network Marketing ambacho hao niliowataja hawajui?????
   
 20. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Boss, yeyote anayelipwa kwa hard cash ananufaika sana, ndio mana ukienda maduka ya wahindi wana quote bidhaa zao kwa US$ sababu wanajua kwao ni faida tele kwa tele, ndivyo ilivyo kwa Network Marketers pia.

  Wajanja wengi hivi sasa wanafungua akaunti za Forex, its better you do that, cause US$ 2,000 at Tshs 1,500/- rate is not same at 1,800/- and it keeps going up. Hakuna siku dola itashuka dhidi ya Shiling.

  Its very obvious, but I wonder why people don't see, or is it because it too good to be true?

  Hii ndio sababu ya Network Marketers kufurahia, wanalipwa in USD.
   
Loading...