Naomba niwaage

Naomba niwaage

Boss naomba tips kidogo. Kusema kweli sijisikii vizuri.
Dah kumbe tupo wengi, ujue huu ugonjwa wengi sana tunaumwa ila hatujui tu na ndomana siku za karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaanguka tu wanakufa inamaana hawa walikuwa wanatembea na korona bila kujijua

Ushauri, kwa ambae ameshapata dalili za korona na akatumia either dawa za mitishamba ama mchanganyiko wa dawa za dukan tupe hints humu na wengne wengi wanufaike

Sent using My phone
 
Kwa heshima na taadhima, sio mbaya nikiwaaga members wenzangu ambao nimefahamiana nao hapa JF. Pia, kwa dhati kabisa naomba wote wenye niliwakwaza kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wanisamehe.

Siamini kama kuna yeyote anaeye tamani kuhitimisha safari yake hapa duniani akiwa mwenye dhambi, kwasababu Mungu wetu mwenye upendo ametupa nafasi ya kutubu dhambi zetu siku zote.

Baada ya kazi sasa nimeona nijitenge kwa muda wa siku kadhaa ili niitazame afya yangu. Kama Mungu akipenda basi tutaendelea kujiona tena, lakini akinipenda zaidi basi yote kheri.

Hakika ninaogopa, nimekuwa na hofu kuu, moyo wangu unahuzunika.

Ngoja nipambanie hii pumzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushimen my nizzle for shizzle, MUNGU aliye mwingi wa rehema hakika atatuhifadhi kwa pendo lake lililo kuu
 
Kwa heshima na taadhima, sio mbaya nikiwaaga members wenzangu ambao nimefahamiana nao hapa JF. Pia, kwa dhati kabisa naomba wote wenye niliwakwaza kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wanisamehe.

Siamini kama kuna yeyote anaeye tamani kuhitimisha safari yake hapa duniani akiwa mwenye dhambi, kwasababu Mungu wetu mwenye upendo ametupa nafasi ya kutubu dhambi zetu siku zote.

Baada ya kazi sasa nimeona nijitenge kwa muda wa siku kadhaa ili niitazame afya yangu. Kama Mungu akipenda basi tutaendelea kujiona tena, lakini akinipenda zaidi basi yote kheri.

Hakika ninaogopa, nimekuwa na hofu kuu, moyo wangu unahuzunika.

Ngoja nipambanie hii pumzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Comandante, you will survive and come back stronger.
 
Kulikoni tena jamaa yng?
Ukishajenga hofu ya ugonjwa flan
Chakwanza utasoma dalili za ugonjwa huo,

Cha pili utaanza kujitengenezea dalili zako kuhisi zinaendana na ugonjwa wa hofu yako, na kwa imani utaona kweli zinaendana,

Tatu utaona unao ugonjwa husika..
Nne utajenga hofu na kukata tamaa,

Tunarudi pale pale,
hofu ni ugonjwa mkubwa sana, huongeza unyonge, hukatisha tamaa, hupunguza maarifa.

Mwisho wa yote, hujatuweka wazi tatzo n nini,
kikubwa jipe nguvu Kaka Mkubwa.
 
Kinachotuuguza ni hofu

Ukiwa na hofu unakufa hata kama ni mzima wa afya

Pia wakuu tujitahidi kufanya mazoezi, japo kukimbia tu

Corona hahitaji kukaa kaa tu

December nilikua na dalili zote lakini Mimi sio mtu wa kujikalisha kalisha tu nafanya sana mazoezi

Nilipata shida kidogo kupambana lakini dalili zilipotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeongea nae, hajaniambia nini tatizo, tuliahidiana kuongea tena usiku.....msiache kumuombea na tuombeane wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kama una nafasi hiyo jitahidi kumjenga aondoe hofu maana ana dalili za kukata tamaa. Hofu ni zaidi ya ugonjwa, nasi kwa nafasi yetu twaendelea kumsihi Mungu amponye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mm situation ndio Kama hiyo nikivuta pumzi nakohoa,mafua ,siskii harufu ya kitu chochote,uchovu bila kufanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilikua sina mafua.. ila koo na kifua mdio vilinitesa. Nikilala ndio linazidi kutaka nikohoe.
Mm toka wiki iloyopita natumia mchanganyiko huo wa asali,Tangawizi unga na Limao. Pia hua namungunya tangawizi kipande kidogo everyday na kula chungwa moja.
Mkuu tafuta mnyaa ni mzuri sana.. kipindi hiki sijatumia maana nilikua napanik hadi nikasahau kama ni dawa. Ndio nikakumbushwa maana utotoni tulikua tunapewa na wazazi
 
Back
Top Bottom