Naomba niwaage

Naomba niwaage

Kwa heshima na taadhima, sio mbaya nikiwaaga members wenzangu ambao nimefahamiana nao hapa JF. Pia, kwa dhati kabisa naomba wote wenye niliwakwaza kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wanisamehe.

Siamini kama kuna yeyote anaeye tamani kuhitimisha safari yake hapa duniani akiwa mwenye dhambi, kwasababu Mungu wetu mwenye upendo ametupa nafasi ya kutubu dhambi zetu siku zote.

Baada ya kazi sasa nimeona nijitenge kwa muda wa siku kadhaa ili niitazame afya yangu. Kama Mungu akipenda basi tutaendelea kujiona tena, lakini akinipenda zaidi basi yote kheri.

Hakika ninaogopa, nimekuwa na hofu kuu, moyo wangu unahuzunika.

Ngoja nipambanie hii pumzi.



UPDATE.....

Wakuu..... hata sasa niseme naendelea vizuri sana, na Mungu amenisimamia katika hili.
Asante kwa MAOMBI yenu yalio niinuwa.
Asante kwa michango na PM zenu zilizo nifariji na kunitia moyo.
Asante kwa comments zenu zilizo nijenga na kunitoa hofu pakubwa.
Asante kwa kuniweka mawazoni mwenu na kunijulia hali, najivunia zaidi nikisema mnanijali sana.
Asante kwa msaada wote ule mliotoa kwa ushauri na pia member ulie nitumia dawa.
Asante kwa kujumuika nami kimawazo na kiroho.
Asante kwa urafiki wenu.
Asante kwa upendo wenu.
ASANTE, ASANTE, ASANTE tena nasema ASANTE.


Na hivi ndivyo nilivyo pambana na dhoruba:-

1. Nilijifukiza nyungu kwa kutumia muarobaini mixer na mshana mixer na mkaratusi × 3 kwa siku
2. Nili kunywa juice ya tangawizi mixer na limao mixer na kitunguu swaumu × 3 kwa siku.
Kuna dawa nilitumiwa na nilikunywa vijiko 2 vya chai kila baada ya masaa 3.
Sasa nimekuwa mzima, sina mafua, sina maumivu, sina kikohozi, sina maumuvu ya kichwa, sina mamumivu ya mwili, asante Mungu nimerudi barabarani kama kawaida
Pole mkuu,na hongera kwa kupona,sasa karibu jamii forum tuchati kaka.
 
Wala usiogope mkuu mimi toka ijumatatu ya wiki iliyopita nilikua hoi mno. Mbavu,kifua,joint,kichwa,homa na kikohoo

Niliogopa sana yaani kifua na koo vilivyokua vinauma nilijua naondoka asee. Ila leo niko poa kabisa.(Sikuambia yoyote juu ya hiki)

Cha msingi acha Hofu kabisa kama una Kwaya Video angalia sana zinaondoa temptation..

Chukua Baking Soda kijiko cha kula kimoja changanya kwenye glasi kunywa kabla ya kula chochote.Nimepona kifua na Mbavu kwa hili.

Chukua Tangawizi,Asali na liamao uwe unakunywa.
Chukua mnyaa/mnyara ubabue kwenye moto kifogo kisha tafuna meza maji yake kikohoo kitapona.

Au tafuna majani ya mbaazi kifua na Kikohoo vitapona
Mimi nimepona koo kwa mchanganyiko huo
View attachment 1436458
Mkuu habari.
Naumwa hapa kooni mwezi sasa. Nimetumia antibiotics zote.
Nimetumia azuma twice wapi.
Pen v twice wapii.
Nikatunia ampiclox juzi imeisha ndo kwanza maumivu yanazidi.
Nikanunia na mouth wash sion msaada. Nimesukutua na maji ya chumvi wapi.
Jana nimeenda hospital wameniandikia power safe. Leo nimechoma ya 2. Bado 3. Hii baking powder uliitumia mara ngapi per day?
Naumia mno kwenye koo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niilitumia siku 3 tu..
Unasikia kama kitu kimekaa kooni.?
Unakohoa.?
Unasikia kama unakohoa kikohozi hakitoki..?
Una Ulcers.?
Sina ulcers kabisa.
Sikohooi.
Yaani panauma balaa.
Nadhan kama kitu hivi kimekaa sijui.
Halaf mwanzon makohozi hayakua yakitoka. Sasa hivi yanatoka. Its as if pana kidonda hata sielewi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuna tangawizi mkuu kama hua hutafuni.
Pia jaribu kumeza punje za tangiwizi kila siku asubuhi na jioni kama utashindwa kutafuna.
Ikishindikana kwa tangawizi na Kitunguu swaumu sijui tena
Nilikua nasaga tangawizi na limao nakunywa. Sasa hivi nasaga tangawizi peke yake nainywa plain. Naipasha moto tu then nainywa plain bila kitu. Nakunywa asubiluhi na jion. Hii nimeianza jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom