Uzi unasema,"Sina chaguo Kati ya kuishi au kufa"
Naogopa, moyo wangu una hofu kuu, nipo ugenini na hata baada ya kumaliza kilicho nileta huku pia sinto kuwa na namna ya kujumuika na familia yangu tena (mke na watoto wangu) hadi pale nitakapo jiridhisha na kuthibitika kwamba sija ambukizwa na hata kama nitakuwa positive basi bilashaka nitalazimika kuishi kama wale ama nawale.
Ni mmoja kati ya tunao fanya nao hili.
Alionekana mwenye hofu na alichukuwa tahadhari zote kama ilivyo takikana.
Alipaa na mwewe hata kwenda kwenye moja kati ta vikao vizito kwaajili ya kazizetu hizi.
Baafa ya siku moja, alirejea na ghafla akaanza kujisikia vubaya.
Mwenzetu mmoja alimpeleka hospital na baada ya vipimo alipatikana na joto la mwili likiwa zaidi ya nyuzi joto 45.
Hali hiyo ilipelekea kupumzishwa na kuchukuliwa sampuli kwaajili ya kwenda Dar kwa vipimo na jana majibu yalirejea akiwa positive, na tayari yupo kule ambapo wengine pia wametengwa.
Inasikitisha sana hasa ninapo mtazama yule aliye chukuwa tahafhari kubwa zaidi ya mimi, lakini tayari ameuguwa.
Ni mtu tulikuwa nae mara kadhaa asubuhi hata jioni, ingawa hatukuruhusu kushukana mikono lakini pale ofisini pake palikuwa na maji na sabuni, na pia alitumia sanitizer kila alipo gusa chochote.
Kwa siku mbili mfululizo alinibeba na gari lake akinirudisha hotel nilipo fikia kwaajili ya mapumziko.
Yes tulizaliwa ili tuishi na kisha tukufe. Pamoja na kwamba ninatambua kwamba nitakufa, lakini ukweli sijioni kama nipo tayari kukufa ama kwa lugha nyepesi hata sina haraka ya kutangulia huko.
Anyway, kikubwa ninawasihi tena mchukuwa tahadhari wakuu maana hii kitu inaogopesha mwili na roho. Pia unapo patwa na hali kama hii hata furaha hutoweka na sura hukosa nuru.
Kwakuwa sijajuwa hatma yangu, basi nimeamua kuzidi kuchukuwa tahadhari na nimeamua kutumia vitu ninavyo shauriwa na wataalam ili kuingeza vitamin mwilini inayo pambana na hili tatizo.
Mengine, nimeamua kumuachia Mungu maana yeye ndiye alie niumba na anaijuwa kesho yangu
Sent using
Jamii Forums mobile app