Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Wanasema mwanamke hasomeshwi.
Sio yeye anae nisomesha ntasomeshwa na wazazi in case nkiacha ndoa nkarudi shule ila nkichagua ndoa basy ndo elimu bye bye
 
Mwacheni achukue maamuzi yake akiharibikiwa ndio tuanze kumshauri
..mm najua huyu akichukua maamuzi yake haipiti miezi 6 anakuja kulia humu
Jamaniiii kumbe wewe sio mtu mzuriii... Unataka wenzio waharibikiwe
Mimi nmekuja kuja uku mapema ili kisiharibike chochote nkishaharibikiwa hata nkija kuomba ushauri Haita nisaidia kitu
 
Unajisomesha au nani atakusomesha?
Wazazi ndo wanaenisomesha lakini kama nikichagua ndoa basi ndo sisomeshwi tena labda kama mume mtarajiwa atakubali kunisomesha huko mbeleni
 
Kasome mrembo. Akikata mawasiliano tuwasiliane..🙂🙂🙂
Hahahaha you made me laugh...............
In case aka kata mawasiliano sitakua tayari kuwa kwenye mahusiano mapema. Ntajipa mda kwanza
 
Kasome mrembo. Akikata mawasiliano tuwasiliane..🙂🙂🙂
Hahahaha you made me laugh...............
In case aka kata mawasiliano sitakua tayari kuwa kwenye mahusiano mapema. Ntajipa mda kwanza
 
Story yako inafanana kabisa na watu fulani hivi hapo nyuma kidogo:
Ilikuwa hivi;
Walikutana wakati wamemaliza advance wakaanza kudate, kisha ukafika wakat wa kuanza michakato ya ku apply vyuo, mwanaume akamuomba msichana asiapply kwanza asubirie mwanaume apply kisha aone atapangiwa chuo gani na mambo yataendaje!
Basi mwanaume akafanikiwa kuchaguliwa chuo kimojawapo hapa Tz na akafanikiwa kuanza masomo.
Wakat akiwa shule mwanzoni mapenzi yao yalikuwa moto moto sana simu kila mara iko sikion watu wanalonga mahuba yao.
Ikakata miezi 3 had 6 mbele, jamaa akaanza kuona ni ushamba kuwa na demu huko kijijini ilihal wapo pale arround wanaojua kuvaa mini sket, headphone masikion nk,

Akaanza ku approach dada mmoja hivi, yule dada akamkubalia akalamba asali sasa ili aoneshe yuko serious ikabidi adrop mawasiliano na yule wa kwanza, si unajua tena ukipata kipya unachunguzwa na kuvhunguzana, sema bahat nzuri yule dada wa chuo alikuwa mzuri sana kama jokate na akawa anamdhalau namna fulani mvulana, ikafika siku mwanamke huyu wa chuo akamuacha mwanaume! Daah jamaa akawaza na zile confusion za kuachwa gafla na stress za hapa na pale akasema haiwezekan kwanza nina mpenz ananipenda zaidi yako ishia nenda zako.
Jamaa akakata nauli akamfuata yule wa kijijin alieishia advance akaja nae chuoni wakapanga wakawa wanaishi mtaani lakin lengo kubwa ninavyohisi ni zile paniking za kuachwa na kutaka kumuonesha aliemuacha kwamba amepata new lady ndani ya muda mfupi.

Ni kweli wakaishi pa1 hadi kumaliza chuo pamoja na changamoto za hapa na pale.
Baada ya hapo mwanaume akatafuta kazi akapata mkoa tofauti na alipoachwa huyu mchumba wake na wakat huo alikuwa na mtoto mmoja tayari kazalishwa.
Huko alikopata kazi walau kamshahara na malupu lupu yakawepo kilichofatia hakutaka kumuita huyu mpenzi wake, mpenzi wake akatumia nguvu na vishawishi ikiwemo kusema mtoto yuko taaban hoi kufa kila mara ikafika mahali kuepusha usumbufu jamaa akaamua kumuita kishingo upande.
Kule kazini jamaa akapta wenye mishahara wenzake tena wanofanya nao warsha za mikoani na safari za hapa na pale za kazini zisizoisha basi akanogewa huko.
Akatangaza ndoa huko kwa wengine kisa eti huyu hana elimu, hana kazi, hayuko smart.
Dada wa watu akachanganyikiwa akaanzisha timbwili daily kulia,daily kumfuata nyuma mwanaume na kuvizia mademu wa jama na kuanzisha mbwai mbwai anatumkiwa hatakiwi ila hasikii yan ni full fujo.

Mdada akatumia njia ya kukosanisha amani kwa mshikaji kama njia ya kufikia lengo lake kwamba yeye alimuharibia basi asitegemee yeye kuachwa lazima amugaribie tu.
Naona zile fujo za haja maana daily kuvunjiana simu, kuloanishiwa nguo, kuchaniwa nguo nk jamaa akasalender akamuoa kwa shingo upande.
Wapo wanaishi had sasa.
Somo langu hapa ni kwamba unaweza wekeza moyo wako kwa mwanaume na ukaacha vitu vya msingi sana hasa elimu vikakupita kisha ukaja kujutia akakubadilikia.

Shika elimu kwanza huyu elimu huwa mkombozi pale unapoweza kuachwa na kila kitu.
Mapenzi yapo ila elimu nzuri ni ile unayoipata with in time na with in stage nikimaanisha huna watoto wala majukumu ya kuambiwa toka darasni upokee simu yangu.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Asante nmepata kitu hapo
 
Huyu lkn ameshindwa kujieleza vizuri so wengine tunashindwa kujua hasa issue ni nn!
Kusema yeye mwanaume kasoma, au just kwenda chuo is too subjective: Chuo cha kusomea cherehani, uvuvi, sayansi kimu au na kozi gani hasa ukichukulia unasema mwaka huu mmepanga kufunga ndoa ?

Sema chuo gani, kozi gani na ya muda gani. Nani analipa na why now ?

Then tutakushauri vzr inawezekana jamaa yupo right ( utueleze yy kasoma kwa level gani ?)
Kuna baadhi ya maelezo siezi kuyaeleza moja kwa moja ili kuficha identity huku wapo watu wengi mnoo kama sio yeye basi ata marafiki au ndugu so sitaki........ Ila ada inalipwa na wazazi wangu sio na yeye ila ikitokea akanioa basi ada itakua juu take huko mbeleni
 
Wewe olewa tu dada achan na mambo ya elimu wasome wenzio, unaambiwa ukiolewa kisha ukazalishwa sijui na majukumu ya ndoa chuo either kitakuwa kigumu au kitaleta ukosef wa aman ya ndoa na concetration ya masomo! Ww naona ndoa kwanza hapa tunakupigia madebe tu, ndoa njema bibie
 
Kuna baadhi ya maelezo siezi kuyaeleza moja kwa moja ili kuficha identity huku wapo watu wengi mnoo kama sio yeye basi ata marafiki au ndugu so sitaki........ Ila ada inalipwa na wazazi wangu sio na yeye ila ikitokea akanioa basi ada itakua juu take huko mbeleni

Ok, basi ushauri in general ni kukaa nae na kuongea na kukubaliana nyie wawili. Mtu wa kawaida leo hii kusema ukienda kusoma basi ina maana kuna kitu flani.

Hyo umesema ni fiance' na mnatarajia kuoana mwaka huu au soon, sasa mlipoanza mpaka kufika level hiyo hii issue ya kusoma ilikuwepo au ? Mahari tayari na wazee wameamua kukusmesha ??

Dah maswali mengi, just go talk
 
Nenda shule we binti akikuacha mwambie kiroho safi akuache tu ila tambua elimu ndo kila kitu. Kumbuka anakwambia usiende shule umtegemee yeye ikitokea akafariki japo hatuombei utaishije?

Nenda masomoni tena mwambie hutabadili tabia yako labda utabadili yeye akioa au kukuacha. Nothing else.
Take my advice but who will be responsible for student fees and other expenses during ur study? Kama ni yeye na wazazi hawana uwezo basi ni shidaaa but seatdown with him mtafikia muafaka
 
Mchumba maana yake nn? Nijuavyo Mimi mchumba ni mtu ambaye kaweka kishika uchumba au kapeleka posa ila sio kufahamika tu.
 
Mchumba sio mume wako, hata ukiamua kutokwenda kusoma anaweza akakuacha na kuoa mje mwingine.

Bora angekuwa mume wako, ningeelewa wewe kujiuliza ila mchumba naaaaaaaaa.

Nenda kasome, wanaume hawatabiriki. Na ukiamua kumsikiliza utakuwa boya kwake hata mkioana, na atarumia kukutukana. Naandika haya sababu nimeyaona wanawake wanaoogopa kujiendeleza kisa wanaume.
 
Bado tuna safari ndefu sana nchini mwetu kwa baadhi ya watu kuhusiana na elimu na wanawake. Mwanamke kwa watu hawa ni bado mtu wa jikoni na kulea watoto tu asiyestahili kupata elimu ya juu ambayo si faida kwake tu bali kwa familia yake, watoto wake na Taifa kwa ujumla.

[emoji15] [emoji15] [emoji15]

Hebu nisaidieni kushangaa kwa hii theory manake nikashindwa.
Eti kuna hili somo pia la umaRaya kwenye syllabus?!!..
 
  • Thanks
Reactions: kui
Bado tuna safari ndefu sana nchini mwetu kwa baadhi ya watu kuhusiana na elimu na wanawake. Mwanamke kwa watu hawa ni bado mtu wa jikoni na kulea watoto tu asiyestahili kupata elimu ya juu ambayo si faida kwake tu bali kwa familia yake, watoto wake na Taifa kwa ujumla.

Yaani safari ni ndefu sana, kama bado tuna watu wanafikiri kuwa mwanamke hawezi kuwa na nafasi ya maana ktk jamii.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inashangaza na kusikitisha sana, lakini cha kutia moyo wanawake wengi wameufahamu umuhimu wa elimu hivyo wengi hawalazi damu wanajitahidi kwa kila hali ili nao wapate elimu ya juu.

Yeah ni kweli, afadhali at least hivyo, kuna kujitambua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maisha yenyewe haya ya dunia hii ya leo halafu usiwe na elimu ya juu unaweza juta.

Yeah ni kweli, afadhali at least hivyo, kuna kujitambua.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom