Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Kwa umri wako na elimu yako, better ukaenda shule kwanza. Kama ni ngumu kwake kukuruhusu uende shule sasa hivi; ni ngumu zaidi yeye kukuruhusu uende shule once you are married +watoto. Maisha hayarevolve around ndoa only, kuna Maisha nje ya ndoa. Sijui kama ndoa inaua ndoto za wanawake wengi, but ukishaolewa ni kazi zaidi kutimiza ndoto zako binafsi. Omba hata wazee wako waongee naye, maybe itasaidia kukuelewa. Kila la kheri
Ok sawa
 
Sawa mkuu asante ntalitafta

Mimi pia nmemwambia tuoane huku nikiwa shule kakataa... Kaniambia nifute hayo mawazo kama nataka kua ña yeye.....
Kwa muonekano wangu huyo mumeo mtarajiwa utaisoma namba hakika anataka uwe goli kipa ili badae uisome namba vizur, nafikir wanaumme wako kibao nenda chuo kama anakupenda mtaoana ila kama msimamo wake ukienda chuo usimtafute bas chagua mapenz au ndoa
 
Nenda kasome mrembo, mume mtarajiwa asiyetaka maendeleo yako ya aina yoyote ile ikiwemo elimu hakufai. Kumbuka elimu ni ufunguo wa maisha. Kila la heri na baraka kwenye masomo yako.
Elimu ni broad term! Sio lazima iwe formal.....labda tunaelewa vibaya hii phrase "Elimu ni ufunguo wa maisha".
 
Kwangu mimi elimu ni ufunguo wa maisha kwa muhusika kama ataajiriwa, atajiajiri, ataoa au kuolewa na hata kwa Taifa lake pia. FYI siilewi vibaya hiyo kauli.

Hahahaha ushauri wa watu wengi humu ni "nenda shule, mwanaume wako anaonekana hapendi mafanikio yako".
Nani kawaambieni kwenda shule kuna-guarantee ultimate success(mafanikio)??
 
Kwangu mimi elimu ni ufunguo wa maisha kwa muhusika kama ataajiriwa, atajiajiri, ataoa au kuolewa na hata kwa Taifa lake pia. FYI siilewi vibaya hiyo kauli.
Hata Elimu itolewayo nje na mfumo maalumu ni Elimu na ipo advocated kwenye hiyo phrase "Elimu ni ufunguo wa maisha"
 
Mimi naongelea elimu ya mfumo maalum ambayo ina ubora zaidi ukilinganisha na hiyo ya mfumo usio maalum

Hata Elimu itolewayo nje na mfumo maalumu ni Elimu na ipo advocated kwenye hiyo phrase "Elimu ni ufunguo wa maisha"
 
Nenda shule utengeneze future yako usikubali kuburuzwa. Mwanamme anaekutakia mema hawezi kukataa mafanikio yako. Inakua vizuri nyote mukiwa wasomi kwenye ndoa za ulimwengu huu. Umri wako unakuruhusu sana kutafuta elimu kwanza hayo mengine yatafuatia. Chukua uamuzi ambao unahisi unaweza kukuletea maendeleo mazuri baadae kama ni kukaa nyumbani kulea watoto au kujiendeleza kielimu ili uweze kujitegemea. Inawezekana hataki mulingane kielimu au ufanye kazi.
 
Habari zenu wanajamvi,

Naomba ushauri kutoka kwenu,

Mimi ni binti wa early twenties na nina mchumba ambae mpaka kwa wazazi anajulikana na Mungu akipenda mwaka huu tutaoana.

Kilichonileta hapa ni hiki kuanzia mwaka Jana nilikua nataka nianze process nirudi shule nilipomshirikisha huyu mchumba kakataa kabisa tena kaenda mbali zaidi na kuniambia siku utakayokwenda shule kata mawasiliano na mimi.

Na mimi nimemwambia mbona inawezekana kwenda chuo na mambo yote yakaendelea kama kawaida lakini bado ameshikilia uzi huohuo wa mimi nisiende chuo.

Naombeni ushauri nisimamie wapi maana najikuta nawaza nashindwa kujua ni choose ni kitu gani.

Nb: Yeye amesoma
Nenda kasome ww achana na mawazo yake kama hatak huyo sio chagua sahihi
 
Tatizo lenu mkipata elimu ila quality ya kua wife material ghafla tu inapotea mnakua wajinga wajinga sijui kwann ndo mana wanaume wengi wanaoa wanawake wasiosoma au wenye elimu ndogo....jiulize mtu ana master anaoa cheti...kwaninininininini

..tukipata elimu tunakuwa wajinga wajinga. [emoji15] [emoji2]
 
Hahahah nyie wachumba bana mkishafikaga chuo tu mwaka wa pili mnaanzaga vimaneno mkijiona wasomi saaaaanaaaa.....oooo nimepata msomi mwenzangu nk.....weeeeeeee huyo ndo jembe

Halafu ujue kuna ka authority flani hiv wanaume wamepewaga na mungu yaaani hata uwe na ma phd,masters, nk haaa mwanaume akiamua kukukalisha waaaiiiiiiiiii elimu yote uvunguni so tia akili.............
 
Wengi wa Wanaume wenye upeo mdogo huisi mwanamke akienda Chuo basi tena atajanjaruka, uamuzi wako unataka kuolewa ama utengeneze future yako kwanza.
Tatzo lenu wadada mkiaminiwa mkarudi shulen asilimia kubwa husababisha mahusiano yayumbe either akat yuko chuo au akirud
Ndo maana nw days men atu appreciate hzo mambo sio kama hazina umuhim la hasha bali tabia zenu tu
 
Yeye amesoma.... Amefika mbali kidogo siwezi kutaja hapa elimu yake ili kuficha identity yake

Wa ajabu sana huyu mtu wako, yaani yeye msomi halafu hataki kukupa nafasi ya kusoma kabla hujawa busy na familia!

Lakini nenda shule kwanza ujikamilishe vizuri.
Mtu anaweza kukunyanyasa au kuchukua ulichonacho, but they will never be able to take away your knowledge or your education.
 
Story yako inafanana kabisa na watu fulani hivi hapo nyuma kidogo:
Ilikuwa hivi;
Walikutana wakati wamemaliza advance wakaanza kudate, kisha ukafika wakat wa kuanza michakato ya ku apply vyuo, mwanaume akamuomba msichana asiapply kwanza asubirie mwanaume apply kisha aone atapangiwa chuo gani na mambo yataendaje!
Basi mwanaume akafanikiwa kuchaguliwa chuo kimojawapo hapa Tz na akafanikiwa kuanza masomo.
Wakat akiwa shule mwanzoni mapenzi yao yalikuwa moto moto sana simu kila mara iko sikion watu wanalonga mahuba yao.
Ikakata miezi 3 had 6 mbele, jamaa akaanza kuona ni ushamba kuwa na demu huko kijijini ilihal wapo pale arround wanaojua kuvaa mini sket, headphone masikion nk,

Akaanza ku approach dada mmoja hivi, yule dada akamkubalia akalamba asali sasa ili aoneshe yuko serious ikabidi adrop mawasiliano na yule wa kwanza, si unajua tena ukipata kipya unachunguzwa na kuvhunguzana, sema bahat nzuri yule dada wa chuo alikuwa mzuri sana kama jokate na akawa anamdhalau namna fulani mvulana, ikafika siku mwanamke huyu wa chuo akamuacha mwanaume! Daah jamaa akawaza na zile confusion za kuachwa gafla na stress za hapa na pale akasema haiwezekan kwanza nina mpenz ananipenda zaidi yako ishia nenda zako.
Jamaa akakata nauli akamfuata yule wa kijijin alieishia advance akaja nae chuoni wakapanga wakawa wanaishi mtaani lakin lengo kubwa ninavyohisi ni zile paniking za kuachwa na kutaka kumuonesha aliemuacha kwamba amepata new lady ndani ya muda mfupi.

Ni kweli wakaishi pa1 hadi kumaliza chuo pamoja na changamoto za hapa na pale.
Baada ya hapo mwanaume akatafuta kazi akapata mkoa tofauti na alipoachwa huyu mchumba wake na wakat huo alikuwa na mtoto mmoja tayari kazalishwa.
Huko alikopata kazi walau kamshahara na malupu lupu yakawepo kilichofatia hakutaka kumuita huyu mpenzi wake, mpenzi wake akatumia nguvu na vishawishi ikiwemo kusema mtoto yuko taaban hoi kufa kila mara ikafika mahali kuepusha usumbufu jamaa akaamua kumuita kishingo upande.
Kule kazini jamaa akapta wenye mishahara wenzake tena wanofanya nao warsha za mikoani na safari za hapa na pale za kazini zisizoisha basi akanogewa huko.
Akatangaza ndoa huko kwa wengine kisa eti huyu hana elimu, hana kazi, hayuko smart.
Dada wa watu akachanganyikiwa akaanzisha timbwili daily kulia,daily kumfuata nyuma mwanaume na kuvizia mademu wa jama na kuanzisha mbwai mbwai anatumkiwa hatakiwi ila hasikii yan ni full fujo.

Mdada akatumia njia ya kukosanisha amani kwa mshikaji kama njia ya kufikia lengo lake kwamba yeye alimuharibia basi asitegemee yeye kuachwa lazima amugaribie tu.
Naona zile fujo za haja maana daily kuvunjiana simu, kuloanishiwa nguo, kuchaniwa nguo nk jamaa akasalender akamuoa kwa shingo upande.
Wapo wanaishi had sasa.
Somo langu hapa ni kwamba unaweza wekeza moyo wako kwa mwanaume na ukaacha vitu vya msingi sana hasa elimu vikakupita kisha ukaja kujutia akakubadilikia.

Shika elimu kwanza huyu elimu huwa mkombozi pale unapoweza kuachwa na kila kitu.
Mapenzi yapo ila elimu nzuri ni ile unayoipata with in time na with in stage nikimaanisha huna watoto wala majukumu ya kuambiwa toka darasni upokee simu yangu.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Akishaolewa akileta swala la kwenda shule ataulizwa uende shule ili iweje!? Kwani unalala njaa humu ndani!? Unatembea uchi!? Una shida ipi hadi utake kwenda kusoma!? Lakini mwanaume huyu huyu mwambie binti yake aishie la saba au O'level kisha aolewe utaona jinsi anavyokuja juu kama mbogo!

It is okay kwa mtoto wa kike wa mwenzie asipate elimu ya juu lakini si wa kwake! Baadhi ya wanaume na undumilakuwili wao kwenye issue hii wanashangaza sana kusema kweli.

Kwa umri wako na elimu yako, better ukaenda shule kwanza. Kama ni ngumu kwake kukuruhusu uende shule sasa hivi; ni ngumu zaidi yeye kukuruhusu uende shule once you are married +watoto. Maisha hayarevolve around ndoa only, kuna Maisha nje ya ndoa. Sijui kama ndoa inaua ndoto za wanawake wengi, but ukishaolewa ni kazi zaidi kutimiza ndoto zako binafsi. Omba hata wazee wako waongee naye, maybe itasaidia kukuelewa. Kila la kheri
 
Ada halipi yeye nilishawahi kufanya kazi nka save pesa na bado nyumbani watani support pale ntakapo kwama nkiwa shule.....
Ila nyumbani wananiambia hayo ni maisha yangu nifuate nacho ona ni sahihi kama nataka kuolewa watani support niolewe na pia kama nataka kusoma watani support nirudi shule

Mbona jibu unalo already, hayo ni maisha yako, usiwahi fanya mistake ya kuacha kujiendeleza because of a man, lazima utajutia tu!
 
Huyu lkn ameshindwa kujieleza vizuri so wengine tunashindwa kujua hasa issue ni nn!
Kusema yeye mwanaume kasoma, au just kwenda chuo is too subjective: Chuo cha kusomea cherehani, uvuvi, sayansi kimu au na kozi gani hasa ukichukulia unasema mwaka huu mmepanga kufunga ndoa ?

Sema chuo gani, kozi gani na ya muda gani. Nani analipa na why now ?

Then tutakushauri vzr inawezekana jamaa yupo right ( utueleze yy kasoma kwa level gani ?)
 
Story yako inafanana kabisa na watu fulani hivi hapo nyuma kidogo:
Ilikuwa hivi;
Walikutana wakati wamemaliza advance wakaanza kudate, kisha ukafika wakat wa kuanza michakato ya ku apply vyuo, mwanaume akamuomba msichana asiapply kwanza asubirie mwanaume apply kisha aone atapangiwa chuo gani na mambo yataendaje!
Basi mwanaume akafanikiwa kuchaguliwa chuo kimojawapo hapa Tz na akafanikiwa kuanza masomo.
Wakat akiwa shule mwanzoni mapenzi yao yalikuwa moto moto sana simu kila mara iko sikion watu wanalonga mahuba yao.
Ikakata miezi 3 had 6 mbele, jamaa akaanza kuona ni ushamba kuwa na demu huko kijijini ilihal wapo pale arround wanaojua kuvaa mini sket, headphone masikion nk,

Akaanza ku approach dada mmoja hivi, yule dada akamkubalia akalamba asali sasa ili aoneshe yuko serious ikabidi adrop mawasiliano na yule wa kwanza, si unajua tena ukipata kipya unachunguzwa na kuvhunguzana, sema bahat nzuri yule dada wa chuo alikuwa mzuri sana kama jokate na akawa anamdhalau namna fulani mvulana, ikafika siku mwanamke huyu wa chuo akamuacha mwanaume! Daah jamaa akawaza na zile confusion za kuachwa gafla na stress za hapa na pale akasema haiwezekan kwanza nina mpenz ananipenda zaidi yako ishia nenda zako.
Jamaa akakata nauli akamfuata yule wa kijijin alieishia advance akaja nae chuoni wakapanga wakawa wanaishi mtaani lakin lengo kubwa ninavyohisi ni zile paniking za kuachwa na kutaka kumuonesha aliemuacha kwamba amepata new lady ndani ya muda mfupi.

Ni kweli wakaishi pa1 hadi kumaliza chuo pamoja na changamoto za hapa na pale.
Baada ya hapo mwanaume akatafuta kazi akapata mkoa tofauti na alipoachwa huyu mchumba wake na wakat huo alikuwa na mtoto mmoja tayari kazalishwa.
Huko alikopata kazi walau kamshahara na malupu lupu yakawepo kilichofatia hakutaka kumuita huyu mpenzi wake, mpenzi wake akatumia nguvu na vishawishi ikiwemo kusema mtoto yuko taaban hoi kufa kila mara ikafika mahali kuepusha usumbufu jamaa akaamua kumuita kishingo upande.
Kule kazini jamaa akapta wenye mishahara wenzake tena wanofanya nao warsha za mikoani na safari za hapa na pale za kazini zisizoisha basi akanogewa huko.
Akatangaza ndoa huko kwa wengine kisa eti huyu hana elimu, hana kazi, hayuko smart.
Dada wa watu akachanganyikiwa akaanzisha timbwili daily kulia,daily kumfuata nyuma mwanaume na kuvizia mademu wa jama na kuanzisha mbwai mbwai anatumkiwa hatakiwi ila hasikii yan ni full fujo.

Mdada akatumia njia ya kukosanisha amani kwa mshikaji kama njia ya kufikia lengo lake kwamba yeye alimuharibia basi asitegemee yeye kuachwa lazima amugaribie tu.
Naona zile fujo za haja maana daily kuvunjiana simu, kuloanishiwa nguo, kuchaniwa nguo nk jamaa akasalender akamuoa kwa shingo upande.
Wapo wanaishi had sasa.
Somo langu hapa ni kwamba unaweza wekeza moyo wako kwa mwanaume na ukaacha vitu vya msingi sana hasa elimu vikakupita kisha ukaja kujutia akakubadilikia.

Shika elimu kwanza huyu elimu huwa mkombozi pale unapoweza kuachwa na kila kitu.
Mapenzi yapo ila elimu nzuri ni ile unayoipata with in time na with in stage nikimaanisha huna watoto wala majukumu ya kuambiwa toka darasni upokee simu yangu.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
I like it, wale mnaojali mapenz badala ya shule tujifunze hapa, mwanaume anayekupenda atakushaur elimu ili mje saidizana badae na c kukalia wivu huyo akishaolewa tuu tayar goli kipa maisha yote hawez kukuacha ukasomee, wanaume ,wanawake wapo tuu, na mapenz yapo tu
 
Back
Top Bottom