Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,643
3,874
Habari zenu wanajamvi,

Naomba ushauri kutoka kwenu,

Mimi ni binti wa early twenties na nina mchumba ambae mpaka kwa wazazi anajulikana na Mungu akipenda mwaka huu tutaoana.

Kilichonileta hapa ni hiki kuanzia mwaka Jana nilikua nataka nianze process nirudi shule nilipomshirikisha huyu mchumba kakataa kabisa tena kaenda mbali zaidi na kuniambia siku utakayokwenda shule kata mawasiliano na mimi.

Na mimi nimemwambia mbona inawezekana kwenda chuo na mambo yote yakaendelea kama kawaida lakini bado ameshikilia uzi huohuo wa mimi nisiende chuo.

Naombeni ushauri nisimamie wapi maana najikuta nawaza nashindwa kujua ni choose ni kitu gani.

Nb: Yeye amesoma
 
Muulize ni sababu zipi ambazo zinamfanya wewe akukatalie kusoma.
Hana sababu ya msingi maana anasema hayo hayakua makubaliano yetu Mara aseme nisubiri tuoane nizae angalau mtoto mmoja ndo nirudi shule lakini kwa upande wangu naona ukishazaa majukumu yanaongezeka na ndio maana nko njia panda
 
Wengi wa Wanaume wenye upeo mdogo huisi mwanamke akienda Chuo basi tena atajanjaruka, uamuzi wako unataka kuolewa ama utengeneze future yako kwanza.
K asante kwa shauri nahisi anaona nikienda chuo itakua ivo lakini sio sahihi kugeneralize
 
Hana nia njema nawe huyo!!! Tena wa kumtupilia mbali. Mwanaume gani hataki maendeleo ya mwenza wake? Kama unatamani kuendelea kusoma bora ufanye hivyo saivi, kwenye ndoa itakua ngumu kidogo.
Wanaume wengine wanataka wakikuoa waku-control hadi unapotaka kununua peni. Wanaogopa ukiwa msomi utakua na akili yako na kuweza kujitegemea.
Wadada wengi ata hivyo tunakumbwa na tamaa tukiwa chuoni, anaweza akawa anaogopa mwanamke wake kuibwa.
Jaribu kuongea nae ujue sababu ya yeye kutotaka wewe usome. Utajua anakataa kwa mema au mabaya.
 
Hana sababu ya msingi maana anasema hayo hayakua makubaliano yetu Mara aseme nisubiri tuoane nizae angalau mtoto mmoja ndo nirudi shule lakini kwa upande wangu naona ukishazaa majukumu yanaongezeka na ndio maana nko njia panda
Ukishazaa kurudi shule ni ngumu!
 
Mi nadhani katumia neno mchumba vibaya... Atakua ni boyfriend. Mchumba ni mpaka awe amekutolea posa.
Nyumbani wanamtambua na posa ameshatoa ila mahari bado.......

....... Sitaki kuyasema yote maana sifahamu kama muhusika yupo uku jf ama laaa
 
Soma mwaya tena kama anataka kukata mawasiliano akate haraka wanaume ni wengi angalia future yako elim ni silaha kwa mwanamke angalie usimskilize ukaja kujuta badae
 
Back
Top Bottom