Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Naomba msaada; Mchumba hataki mimi niende kusoma

Nenda shule mdogo wangu, ndoa zenyewe ziko wapo siku hizi
 
Wengi wa Wanaume wenye upeo mdogo huisi mwanamke akienda Chuo basi tena atajanjaruka, uamuzi wako unataka kuolewa ama utengeneze future yako kwanza.
Halafu wengi wenye upeo mkubwa waliwaruhusu wachumba kwenda kusoma wakaishia maumivu makali. Kama mume sio future ujue hauko tayari kuwa na mchumba. Mapenzi na shule ni pilau na mrenda!!
 
Habari zenu wanajamvi,

Naomba ushauri kutoka kwenu,

Mimi ni binti wa early twenties na nina mchumba ambae mpaka kwa wazazi anajulikana na Mungu akipenda mwaka huu tutaoana.

Kilichonileta hapa ni hiki kuanzia mwaka Jana nilikua nataka nianze process nirudi shule nilipomshirikisha huyu mchumba kakataa kabisa tena kaenda mbali zaidi na kuniambia siku utakayokwenda shule kata mawasiliano na mimi.

Na mimi nimemwambia mbona inawezekana kwenda chuo na mambo yote yakaendelea kama kawaida lakini bado ameshikilia uzi huohuo wa mimi nisiende chuo.

Naombeni ushauri nisimamie wapi maana najikuta nawaza nashindwa kujua ni choose ni kitu gani.

Nb: Yeye amesoma
Sio sisi tutakaoishi na huyo mwanaume. Hayo na maamuzi yenu wawili.
 
Hana nia njema nawe huyo!!! Tena wa kumtupilia mbali. Mwanaume gani hataki maendeleo ya mwenza wake? Kama unatamani kuendelea kusoma bora ufanye hivyo saivi, kwenye ndoa itakua ngumu kidogo.
Wanaume wengine wanataka wakikuoa waku-control hadi unapotaka kununua peni. Wanaogopa ukiwa msomi utakua na akili yako na kuweza kujitegemea.
Wadada wengi ata hivyo tunakumbwa na tamaa tukiwa chuoni, anaweza akawa anaogopa mwanamke wake kuibwa.
Jaribu kuongea nae ujue sababu ya yeye kutotaka wewe usome. Utajua anakataa kwa mema au mabaya.
Tatizo lenu mkipata elimu ila quality ya kua wife material ghafla tu inapotea mnakua wajinga wajinga sijui kwann ndo mana wanaume wengi wanaoa wanawake wasiosoma au wenye elimu ndogo....jiulize mtu ana master anaoa cheti...kwaninininininini
 
Sio kua tunakua wajinga mkuu! Tunapata ujasiri, na hicho ndicho mwanaume hapendi.
 
"....mpaka kwa wazazi anajulikana...". Kujilikana kwa wazazi sio tiketi kwamba ni mtu sahihi kwako.
"...siku utakavyokwenda shule kata mawasiliano na mimi". Akupe sababu ya msingi ya kukuzuia kwenda masomoni.

Labda yeye anataka kuoa mtu mwenye kiwango cha elimu ulichonacho kwa sasa. Sasa ni wewe mwenyewe kukaa chini na kutafakari kati ya elimu na ndoa unachagua kipi.

Kama kakataa saiz usome wakati hamjaoana uwezekano ni mkubwa sana hata mkioana atakukataza kwenda kusoma.

Mwenye maamuzi ni wewe.

Ni mawazo yangu.
 
Habari zenu wanajamvi,

Naomba ushauri kutoka kwenu,

Mimi ni binti wa early twenties na nina mchumba ambae mpaka kwa wazazi anajulikana na Mungu akipenda mwaka huu tutaoana.

Kilichonileta hapa ni hiki kuanzia mwaka Jana nilikua nataka nianze process nirudi shule nilipomshirikisha huyu mchumba kakataa kabisa tena kaenda mbali zaidi na kuniambia siku utakayokwenda shule kata mawasiliano na mimi.

Na mimi nimemwambia mbona inawezekana kwenda chuo na mambo yote yakaendelea kama kawaida lakini bado ameshikilia uzi huohuo wa mimi nisiende chuo.

Naombeni ushauri nisimamie wapi maana najikuta nawaza nashindwa kujua ni choose ni kitu gani.

Nb: Yeye amesoma
Wewe unataka nini? Kuolewa au kusoma? Au vyote kwa mpigo? Kipi kwako ni muhimu? Ushauri anza na unachodhani ni muhimu kuliko kingine. By the way ni binti mdogo, think big
 
Endelea na mchumba wako huyo, mana ubashite unaukaribisha mwenyeweeee
 
Kasome mwaya huo mkwaju upo tu utaukuta kama akioa mwingine na wewe utapata mwingine
 
Back
Top Bottom