SparkJuniour2020
JF-Expert Member
- Jan 10, 2018
- 291
- 120
Ndo utamu wa marioo wote, tena wa kwako ana afadhali hata kusimamia hiyo biashara japo huoni hata kumi, by the way mzigo wako huo komaa nao ikishindikana temana nae. Cha mwisho kwa huyu kijianaume acha ufala unamuumiza mtoto wa watu ukue basi cha umariooHabari za mchana wanajamii,
Naombeni mbinu za kuishi na mume bahili/mchoyo.
Mwanaume ni mchoyo jamani, vitu viikisha ndani atajikausha utafikiri sio yeye ndo baba wafamilia. Umeme unakatika atauchuna na mtalala gizani, asubuhi ataondoka bila kuacha hata mia sijui anawaza mtakula nini, kwakuwa nina mtoto mdogo na wadada wa kazi inabidi niwaachachie pesa za matumizi, gari akiriharibu hatengenezi ng'o na litaendeshwa hivyo hivyo mpaka utakavyoamua kulipeleka gereji mwenyewe.
Nimechoka jamani basi ikokea katoa hela utakuta kaweka 100,000 kabatini na hakwambii kama ni pesa ya matumizi.
Akishatoa hiyo atajikausha hata miezi minne inaweza pita bila kutoa kitu na bado ataendelea kukuomba hela,mara naomba hela nikaweke mafuta kwenye gari, mara naomba hela ya sadaka ili mradi ile aliotoa mpaka iishe.
Basi nikafungua biashara sehemu, akaidakia yeye akaanza kuisimamia, sijawahi ona hata mia kutoka kwenye ile biashara, kodi ya pango ikaisha, hela hata mia, ikabidi nilipie tena kodi, bado sioni kitu yaani kama hakuna biashara inaendelea,ukimuuliza anakuwa mkali
Basi nimeamua kutolipa tena kodi ya pango ikiisha, na TRA Silipi. Nimemsema sana lakini naona habadiliki.
Nimfanyeje mwanaume wa hivi khaaaa