Naomba msaada kwa wenye kufahamu zaidi nahitaji kuagiza mzigo AliExpress

VictoniX

Member
Jan 12, 2022
9
5
Naomba masaada kwa wenye kufahamu zaidi nahitaji kuagiza mzigo AliExpress nishaweka order zangu kwenye cart lakini sina uzoefu wowote wa kununua bidhaa online kwa njia hii, nimewahi kununua kupitia kikuu pekee...

Nahisi namna ya kuagiza sio shida sana maana naweza kusoma kwenye tovuti yao na nikaelewa cha kufanya lakini tatizo kubwa linakuja kwenye namna ya kupokea mzigo baada ya kufika nchini maana sina hakika kama AliExpress nao wanaoffice nchini kama ilivyo kwa kikuu.

Pia ningependa kutambua jinsi ya kufunga mizigo yote kwenye parcel moja ili kama ikifika ifike yote kwa pamoja nafikili ni njia nzuri zaidi na pengine inaweza ikapunguza cost za usafirishaji ingawa sina uhakika sana katika hili naomba pia msaada kuelezewa kiundani kwa mwenye uzoefu zaidi.

Bidhaa ninazohitaji kuagiza ni componets ndogondogo za electronics kama regulators, resistors, capacitors, transistors n.k
kwajili ya matumizi yangu binafsi.

Kama kuna maandalizi yakufanya kabla ya kuagiza naomba mnisaidie kufahamu tafadhali AU kama kuna njia nzuri zaid ya kuagiza tofauti na AliExpress pia naomba kusidiwa kufahamu kwa mwenye uelewa zaidi

Vitu ninavyohitaji kufahamishwa zaidi:
  • Namna ya kufunga mizigo yote ije kwenye parcel moja kama inawezekana kufanya hivyo
  • Namna ntakavyopokea mzigo wangu baada ya kufika Tanzania na mahali ninapotakiwa kwenda kupokelea mzigo
  • Kufahamishwa kuhusu tozo zozote za kiserikali ili kupokea mzigo (kama zipo) na tathimini ya gharama kwa harakaharaka
 
Kufungiwa pamoja vitu vyote unaweza ongea na muuzaji na itawezekana kama umenunua kwa vendor mmoja tu.
Mzigo unapokea kupitia sanduku la posta. Lazima uwe na address Yako.
Kuhusu charges inategemea na sehemu. Posta ya hapa Mimi hawanichaji japo parcel zangu ni zile ndogo ndogo.
 
Kufungiwa pamoja vitu vyote unaweza ongea na muuzaji na itawezekana kama umenunua kwa vendor mmoja tu.
Mzigo unapokea kupitia sanduku la posts.Lazima uwe na address Yako.
Kuhusu charges inategemea na sehemu.Posta ya hapa Mimi hawanichaji japo parcel zangu ni zile ndogo ndogo.
Ko natakiwa kufungua sanduku la posta kwanza au wanatuma kwa posta yoyote iliyokaribu na mahali ninapoishi...!!!?
 
Ko natakiwa kufungua sanduku la posta kwanza au wanatuma kwa posta yoyote iliyokaribu na mahali ninapoishi...!!!?
Sio lazima ufungue japo ukifungua ni vizuri. Unaweza tumia la taasisi au la mtu mwingine. Uzuri mzigo Huwa wanaandika jina na namba yako so ukifika postal unatumiwa ujumbe
 
Sio lazima ufungue japo ukifungua ni vizuri.Unaweza tumia la taasisi au la mtu mwingine.Uzuri mzigo Huwa wanaandika jina na namba yako so ukifika postal unatumiwa ujumbe
Ok, nimekupata kiongozi, vipi kuhusu taratibu za kufungua sanduku la posta vitu gani vya msingi labda vinayohitajika au vya kuzingatia..!?
 
Ok, nimekupata kiongozi, vipi kuhusu taratibu za kufungua sanduku la posta vitu gani vya msingi labda vinayohitajika au vya kuzingatia..!?
Hapo kwenye kufungua kwa kweli sijajua maana Mimi natumia box la taasisi.
Nadhani ufike postal utapata utaratibu wote na kiasi Cha kulipia si kikubwa kwa mwaka.
 
Nenda posta utapewa utaratiibu. Ila vitu vichache ni majina yako, namba ya Nida na malipo Tsh 48000/. Pili fuata maelekezo ya mdau hapo juu, amekuambiwa unaweza kutumia sanduku la posta la jirani yako au taasisi iliyo jirani yako.
 
Nenda posta utapewa utaratiibu. Ila vitu vichache ni majina yako, namba ya Nida na malipo Tsh 48000/ .pili fuata maelekezo ya mdau hapo juu , amekuambiwa unaweza kutumia sanduku la posta la jirani yako au taasisi iliyojirani yako
Pamoja Mtemi nashukuru kwa msaada...
 
Nenda posta utapewa utaratiibu. Ila vitu vichache ni majina yako, namba ya Nida na malipo Tsh 48000/ .pili fuata maelekezo ya mdau hapo juu , amekuambiwa unaweza kutumia sanduku la posta la jirani yako au taasisi iliyojirani yako

Huwezi ukatumia agent wa kusafirisha tofauti na njia ya posta?
 
Kimsingi hakuna changamoto yoyote mkuu weka sanduku la posta
Namba zako za simu
Majina yako sahihi yanayomatch na ID zako
Kuhusu gharama za kupokelea utajuzwa pale pale na post office, huwa zipo dynamic kutokana na value mzingo ulioagiza. Mwisho wa siku utapigiwa simu au unaeza kwenda mwenyewe deadline inapokaribia maana huwa wanapitiwa
 
Sanduku la posta sio lazima hata ukiandika Jina la wilaya mzigo utafika kwenye ofisi za posta za wilaya husika.
Nimeagiza saa wamenipa track number ila cna sanduku la posta cjui nitapaje saa yangu na cjui itafikia wapi ili nifanye kama unaelewa zaidi nifaamishekuu
 
Back
Top Bottom