Jinsi ya kuagiza Bidhaa kiwandani

Blacklight

Member
Jun 5, 2023
7
8
Naombeni msaada Kwa wenye uzoefu katika jambo hili.Nilikuwa nahitaji kuagiza ngano na mafuta ya kula Moja Kwa Moja kutoka kiwandani.Hivyo naomba kujua utaratibu wake upoje,wanaanzia pcs ngapi minimum,namna ya kuweka order na utofauti wa Bei maybe ukilinganisha na ya wholesalers Huwa inarange tshs ngapi,pia kama Kuna mambo ya kisheria kwenye Kodi nayo inakuwaje
 
Fika kiwanda husika utapewa utaratibu hapo kiwandani au wacheki kwa hotlines namba zao za simu.....

Ila kwa upande wa kiwanda wana bei zao kulingana na scale au ukubwa na wingi wa bidhaa unazotaka, watauza jumla au rejareja kulingana na kiasi utakacho....mfuko mmoja utauziwa sawa na rejareja tu.
 
Kila kiwanda kina utaratibu wake. Kuna vingine mzigo wote ulisha nunuliwa kabisa hivyo ukienda watakuelekeza uende kwa delear.

Jaribu kwenda kwenye kiwanda husika uongee na mtu wa masoko.

Kama unachukua mzigo kidogo bei itakuwa sawa na maduka ya jumla tu
 
Back
Top Bottom