Naomba leo nisemezane na wanaume wenzangu………………!

Mkuu nakubaliana na maoni yako, lakini hebu tufanye ni mchumba na mko kwenye michakato ya kufunga ndoa au ndio mmefunga ndoa mwaka mmoja uliopita (Na Ndoa bado haijajibu) halafu anapata hiyo nafasi ya kwenda ughaibuni kuongeza ilmu, na wewe ni mwajiriwa ukiwa na nafasi ya kawaida tu...........Hii ina maana kwamba akirudi cheo kitapanda na responsibility zitaongezeka lakini pia atakuzidi kipato.......... Hebu niambie hapo unachukua uamuzi gani?


Inauma sana aisee!Yani nita. . . . . . . . !
 
Kama ni mke its okay ila kama ni mchumba tu tunaelewana jambo hili,kwnza siwezi kumzuia asiende kusoma, pili; the moment anaiacha ardhi ya tanzania kwenda nje kusoma aelewe kuwa huku nyuma hajaacha mchumba wala msebule...yan kila kitu kimeishia hapo..
Sababu: mapenzi ya mbali mengi ni ya kinafiki na usaliti mwingi. Siwezi kumwamini binadamu mwenzangu achilia mbali kivuli changu hasa linapokuja suala la mapenzi..
Sometimes nachukia hii kitu mapenzi aagh...
 
kama ni mke au mchumba ntamruhusu kikubwa ni uaminifu kwan kama si mwaminifu anaweza akafa mambo yake hapahpa hata nikizuia asiende kusoma nje .
 
Kwa mwanaume ambaye hajawahi kuishi ughaibuni anaweza kumruhusu kirahisi mkewe kwenda kusoma huko peke yake, lakini kwa aliyewahi kuishi ughaibuni inaweza kuwa ngumu kidogo, unless waende wote.


Kwa hiyo utaacha kazi yako??
 
Nahisi naweza kumruhusu, kama watoto ni wakubwa. kama hatuna watoto tutaenda wote, kazi naacha. nikacheck opportunities nyingine. kama watoto wadogo sana (under 5 yrs) haendi mtu!
 
Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.

Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?
Hapo kwwenye Red ninawasiwasi nako maana kabla ya kumruhusu angalia mchakato wa kuchaguliwa mke wako!
 
Kwa mwanaume ambaye hajawahi kuishi ughaibuni anaweza kumruhusu kirahisi mkewe kwenda kusoma huko peke yake, lakini kwa aliyewahi kuishi ughaibuni inaweza kuwa ngumu kidogo, unless waende wote.
Uko sahihi 100%. Ndoa nyingi sana zimekwisha kwa style hii. Kama umemchoka na haumtaki mruhusu aende.
 
Kuna rafiki yangu alikuwa na mimba kuubwa lakini alikuwa ananambia kila akisema atembee kufanya mazoezi wanaume wa kidhungu huku nilipo wanamtongoza; nilikuwa nashangaa sana. Akanambia si yeye tu kuna dada mwingine nae yeye ndio alichukuliwa jumla maana mimba yake ilikuwa haijulikani baba nani. Mzungu kamtokea na kulea mimba na kukubali kulea mtoto. Nikajiuliza sasa hawa ingekuwa Tz ningesema washirikina; yani wanaona wanawake wenye mimba attractive sana

Sijuhi ni hapa tu au wadhungu wote wanapenda wanawake wenye mimba.

Nilitaka kumwambia huyo anaesema atampa mimba wife ili awe safe; wengine wanapenda hizo mimba. Lol.
 
Hilo la watoto ndugu linataka umakini. Watoto under 5 ni rahisi kuwaacha kuliko above 7 au teenagers. Fikiri tena kuhusu umri gani mtoto anahitaji close supervision. Kikubwa baba awe caring na watoto wawe na mwangalizi mzuri.

Nahisi naweza kumruhusu, kama watoto ni wakubwa. kama hatuna watoto tutaenda wote, kazi naacha. nikacheck opportunities nyingine. kama watoto wadogo sana (under 5 yrs) haendi mtu!
 
Ninamruhusu bila pingamizi yoyote.
Wengi wanaotia wasiwasi hapa wanaonesha wanaogopa mke kutokuwa mwaminifu. Ikiwa ni hilo, anaweza kutokuwa mwaminifu hata kama upo pamoja naye.

Lakini pia kwa nini hili swali lisiwalenge wanawake pia?, yaani inakuwaje mume anapokuwa masomoni kuanzia miaka miwili na zaidi, na kurejea nyumbani ndio hivyo, mwezi mmoja kwa mwaka?

Ninahisi kikubwa ni ustahamilivu na kuaminiana kwa pande zote mbili, muwe mko pamoja au mbali mbali.
 
Back
Top Bottom