Wanaume tuache kuharibu watoto wetu kwa tamaa ya Pesa

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,372
Salamu.

Kichwa cha habari kinahusika.

Jana nilipata kisa kimoja kinasikitisha sana nikaona niwashirikishe.

Kuna Dada mmoja alikuja kununua dawa kwa ajili ya mtoto wake anayesumbuliwa na kifua,anasema kifua huwa kinambana mara kwa mara na anapata homa usiku na hio Jana alipokuja hali haikuwa nzuri maana hata shuleni alimpeleka yeye na jioni alichelewa sana kurudi kwa sababu anatembea taratibu na kupumzika,ikabidi hadi ampigie mwalimu kumuuliza kama Leo wanafunzi wamechelewa kurudi, mwalimu alimjibu kwamba hawakuchelewa,tena mtoto wake walimhurusu mapema tu(nadhani wanajua hali yake) alipofuatilia akamkuta mtoto amelala njiani ndio akaondoka nae kwenda nyumbani.

Sasa aliponieleza hili nikaona hali kama tete hivi ikabidi nimuulize kama alishawahi kutibiwa hospitali,akamesema hospitalini ameenda sana hajapata nafuu na Mara ya mwisho alikuwa hospitali moja kubwa huko Dar ambako alikaa muda mrefu kidogo na huko alichukuliwa na baba yake mkubwa(shemeji wa huyu dada)ambaye pia ni dakatari hapo lakini akarudi na hali hiohio bila unafuu.

Sasa nikataka nijue huko aliambiwa shida ni nini hasa na aliandikiwa dawa gani akanijibu kwamba hawakuona ugonjwa wowote ila akasema ngoja ampigie daktari wa huko(huyu Shemeji yake) ili anipe maelezo vizuri,kweli akampigia kupitia simu yangu maana hakuwa na salio muda huo,aliposalimiana nae akanipa niongee nae,nilipomuuliza huyo Daktari akasema huyo mtoto anasumbuliwa na Chronic bronchitis Pnemonia na kwamba alitibiwa ila muda waliokaa ni mdogo mama yake akasema wanaondoka wamekaa muda mrefu,maana wanaishi mkoani,nilipotaka anishauri nimpe dawa gani au walikuwa wakimpa dawa gani akasema mtafutie tu dawa inayomfaa kwa tatizi hilo basi tukaachana.

Sasa baada ya kukata simu nikamuuliza mbona kuna utofauti wa maelezo kati yake na Daktari,maana yeye alisema amekaa muda mrefu lakini hawakuona ugonjwa na hakupona,Dr anasema walikaa muda mfupi wakataka kuondoka ndio maana hakupona lakini huyu Dada akasema huyo Shemeji yake hasemi ukweli maana yeye ndiye aliyeomba aletwe kwake ili amshugulikie na mtoto akapelekwa na baba yake na akaachwa huko zaidi ya miezi miwili hakupata unafuu wowote mpaka ikabidi arudi tu maana shule alishachelewa,hapo nikapata swali lingine inawezekanaje ugonjwa wa kawaida tu mtoto ashindikane kupata tiba sahihi kwenye hospitali kubwa kama ile tena baba mkubwa ni Daktari hapo,ndipo yule dada machozi yakaanza kumlenga na kunieleza haya;

Kwamba huyo mtoto pamoja na kuwa na hali hiyo baba yake hata hana habari nae,baba yake ni fundi ujenzi mzuri na huwa anasafiri kwenda kufanya kazi anaweza kukaa huko na miezi mitatu au minne ,lakini hata akiambiwa mtoto amezidiwa anaumwa huwa hashtuki hata kusema atafute muda kuja kumuona, hataki,huwa anasema tu atakuja na hata akiomba atumiwe hela ya matibabu hatumi,akaendelea..

Unaweza ukasema hana muda sawa,lakini hata akiwepo mtoto anaweza kuwa anaumwa usiku na anatapika hapo yeye wala hashtuki wala kuamka mama yake ndio anahangaika,hata kumpeleka hospitali hataki,sasa anajiuliza huyu ni mtu gani asiye na utu?.Pia huwa akiambiwa atume hela mtoto akatibiwe hatumi, unaweza kusema hana hela lakini anasema si kweli kwa sababu Jumamos iliyopita alituma 50,000 za matumizi lakini,akamjaribu tu kumwambia sasahivi kuna baridi atume hela anunulie watoto wadogo masweta(wana watoto watatu,huyu mgonjwa ndio mkubwa yupo darasa la 5)Jana hiohio akatuma 40,000 sasa anajiuliza kwanini huyu mwingine huwa hamjali?

Pia anasema tangu mtoto huyo awe kwenye hali hio huyu baba mtu mambo yake yananyooka tu na hela sikuhizi kwake sio tatizo ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Anasema anahisi huyu baba ameamua kumfanya mtoto wake ndondocha ili apate pesa kama kabila la( )analitaja wanavyofanya ili kupata utajiri hivyo akaamua aende kwa 'mtaalam' ambapo aliona kwenye kioo jinsi baba wa mtoto alivyofanya kumtoa mwanae ili apate mafanikio na hivyo akawa amethibitisha wasiwasi wake.

Cha kushangaza baada ya kutoka huko kwa Sangoma mume wake alimpigia simu akamwambia ameona alipoenda na aache kumfuatilia maisha yake ,akasema walifokeana sana siku hio.

Huyu dada anaumia sana juu ya hili maana mtoto anateseka sana,akienda shule analala tu na kuna muda mtoto anamwambia mama mbona mimi nateseka sana ,siko kama wenzangu ni bora nife tu niondoke duniani,na anasema kuna muda anamsimulia jinsi anavyofuatwa na watu usiku wanamlazimisha kunywa damu za watu.

Sasa mimi najiuliza hivi mtu unasikia raha gani kutumia pesa ambayo inatokana na kumuua au kumharibu mtoto wako?hivi unapata amani kabisa moyoni?Mimi nadhani tunatafuta Mali ili familia ziishi kwa raha na amani?

Wanaume tuache tamaa mbaya mpaka za kufikia kuwatoa kafara watoto wetu,wazazi au wanafamilia kwa tamaa ya pesa,sijui kama wanawake nao wanafanya haya.Inasikitisha sana.

Mwisho nilimpa ushauri tu kama atauzingatia huyo mtoto atapona vizuri lakini kama atachelewa huyo mtoto atakuwa zezeta jumla au kumpoteza kabisa maana hali aliyofikia sasa anasema hata kula hali na kuna muda haongei kabisa anakuwa kimya tu.

Kisa cha Pili;

Kuna Dada mmoja aliolewa na akazaa watoto watatu na Mme wake baadae wakaachana watoto wakiwa bado wadogo,mwanamke akabaki na watoto bila msaada wa mume lakini alijitahidi akawasomesha mpaka yule mkubwa akamaliza sekondari akampekeka chuo fulani cha mambo ya Afya.

Akiwa mwaka wa mwisho chuoni, mtoto akaaga kwamba anaenda kurudia baadhi ya masomo aliyofeli baada ya hapo simu yake ikawa haipokelewi, baada ya kuendelea kupiga mfululizo kama siku tatu hivi simu ikapokelewa na Mama mmoja aliyejibu kwamba 'Kijana hajambo ila wamepumzika baada ya maombi ya usiku kucha,wamechoka sana,Mama akashangaa sana,alipouliza yeye nani na hapo ni wapi hakusema ila akasema tu huyo mtoto yupo pale amepelekwa kwa ajili ya mafunzo ya unabii simu ikakatwa, Mama akachanganyikiwa, alipompigia baba yake hakupatikana hata hivyo anasema baba yake hawajawasiliana siku nyingi na hata mtoto haishi kwake kwahio hakumtilia maanani sana.

Siku ya pili akapiga tena simu ikaita na kupokelewa na mtu yuleyule na majibu walikuwa ni Yale yale, baadae ikawa haipatikani kabisa, siku ya tatu anapokea mtoto ila alipoulizwa uko wapi na kwanini hupokei simu, akajibu nipo nasomea Unabii alipotakiwa kuondoka hapo haraka akasema hawezi kuondoka mpaka amalize mafunzo na kwamba atarudi mwezi fulani,simu ikakatwa haikupatikana tena.

Hapo mama akachanganyikiwa na ikabidi ahusishe polisi,baada ya kuanza kuifuatilia namba baadae alipatikana lakini inaonekana alishaondoka kwa yule mama kuepusha kukamatwa nadhani.

Baada ya mtoto kupatikana aliachana na mambo mengine lakini uchunguzi ulibaini kwamba pale alipelekwa na baba yake malengo aliyoambiwa ni kujifunza unabii lakini haikuwa hivyo kwani yule mama walikuwa ni Mganga ambaye huyo Mme wake amekuwa akimtumia kufanya mambo yake yakae sawa.

Hata hivyo akili ya kijana ilishatetereka tayari na kuna muda anaongea mwenyewe na kufanya ishara za vidole zisizieleweka hivyo ufahamu wake haukuwa vizuri na hivyo yaliyofanyika huko hakuweza kuniju hasa ni nini walikuwa wanafanya.

Baada ya kufuatilia sana ikaonekana huyo Bwana alimpekeka pale ili kumtoa kafara kwa ajili ya kujipatia mali, hivyo angechelewa hali ingekuwa mbaya zaidi.

Mpaka sasa Mama anahangaika na mtoto ili akae sawa, mtoto ambaye amemhangaikia kwa taabu ili asome na sasa amefikia hatua ya mwisho baba anaamua kumtoa kafara ili apate mali.

Haya ni matukio mawili ya kusikitisha sana jinsi gani tamaa za Mali zimewashika wanaume na kuamua kuwatoa kafara au kuwaharibu watoto wao ili wao wafaidi mali, ni unyama wa hali ya juu.

Hivi pesa Chafu kama hizi zitakupeleka wapi kama sio kukaribisha laana kwako?hivi unapata usingizi kabisa au unakula chakula na unakifurahia huku unajua kabisa ni zao la kafara au maumivu ya mtoto wako?au ukimuona mwanao akiwa zezeta wewe moyoni mwao unajisikaje?

Wanawake chunguzeni sana,kuna wanaume wameingiwa na tamaa mbaya sana,wapo tayari kumwaga damu ya mtoto wake ili apate Mali.

Mungu atusaidie sana.
 
Duh!,kweli hii ni changamoto kubwa kwa jamii yetu ya sasa,nadhani hali ngumu ya maisha inachangia lkn pia kutokuwa na hofu ya Mungu miongoni mwa Wanajamii.
 
Hao wanaume watakuwa wamechanganikiwa…watu wa ajabu ni wanawake wanaochomoa vichanga na kuviua kwa kufanya…
 
Huu ni ufala tu, utajiri wa masharti huku kuna wenzio ni matajiri bila masharti yeyote.

Utajiri wa masharti hauwezi hata kurithisha mtu yeyote zaidi ya wewe mwenyewe na ukifa wenyewe nao unakufa na kurudi kwa mizimu huko ambako na wewe unakwenda kuwa msukule.

Kifupi matajiri wote wa hela za uchawi wakifa wanakwenda kuwa misukule huko na utajiri wote unarudi ulikotoka kwa waliokupa.

Ni Mungu pekee ndio anatoa utajiri ambao hauhitaji kumlipa chochote zaidi ya wewe kumuabudu, kutoa sadaka, kutenda yaliyo mema, na ukifa anakupeleka peponi kula bata na utajiri aliokubariki unabaki kuwanufaisha uliowaacha na unaweza kuwepo vizazi na vizazi.
 
Salamu.

Kichwa cha habari kinahusika.

Jana nilipata kisa kimoja kinasikitisha sana nikaona niwashirikishe.

Kuna Dada mmoja alikuja kununua dawa kwa ajili ya mtoto wake anayesumbuliwa na kifua,anasema kifua huwa kinambana mara kwa mara na anapata homa usiku na hio Jana alipokuja hali haikuwa nzuri maana hata shuleni alimpeleka yeye na jioni alichelewa sana kurudi kwa sababu anatembea taratibu na kupumzika,ikabidi hadi ampigie mwalimu kumuuliza kama Leo wanafunzi wamechelewa kurudi, mwalimu alimjibu kwamba hawakuchelewa,tena mtoto wake walimhurusu mapema tu(nadhani wanajua hali yake) alipofuatilia akamkuta mtoto amelala njiani ndio akaondoka nae kwenda nyumbani.

Sasa aliponieleza hili nikaona hali kama tete hivi ikabidi nimuulize kama alishawahi kutibiwa hospitali,akamesema hospitalini ameenda sana hajapata nafuu na Mara ya mwisho alikuwa hospitali moja kubwa huko Dar ambako alikaa muda mrefu kidogo na huko alichukuliwa na baba yake mkubwa(shemeji wa huyu dada)ambaye pia ni dakatari hapo lakini akarudi na hali hiohio bila unafuu.

Sasa nikataka nijue huko aliambiwa shida ni nini hasa na aliandikiwa dawa gani akanijibu kwamba hawakuona ugonjwa wowote ila akasema ngoja ampigie daktari wa huko(huyu Shemeji yake) ili anipe maelezo vizuri,kweli akampigia kupitia simu yangu maana hakuwa na salio muda huo,aliposalimiana nae akanipa niongee nae,nilipomuuliza huyo Daktari akasema huyo mtoto anasumbuliwa na Chronic bronchitis Pnemonia na kwamba alitibiwa ila muda waliokaa ni mdogo mama yake akasema wanaondoka wamekaa muda mrefu,maana wanaishi mkoani,nilipotaka anishauri nimpe dawa gani au walikuwa wakimpa dawa gani akasema mtafutie tu dawa inayomfaa kwa tatizi hilo basi tukaachana.

Sasa baada ya kukata simu nikamuuliza mbona kuna utofauti wa maelezo kati yake na Daktari,maana yeye alisema amekaa muda mrefu lakini hawakuona ugonjwa na hakupona,Dr anasema walikaa muda mfupi wakataka kuondoka ndio maana hakupona lakini huyu Dada akasema huyo Shemeji yake hasemi ukweli maana yeye ndiye aliyeomba aletwe kwake ili amshugulikie na mtoto akapelekwa na baba yake na akaachwa huko zaidi ya miezi miwili hakupata unafuu wowote mpaka ikabidi arudi tu maana shule alishachelewa,hapo nikapata swali lingine inawezekanaje ugonjwa wa kawaida tu mtoto ashindikane kupata tiba sahihi kwenye hospitali kubwa kama ile tena baba mkubwa ni Daktari hapo,ndipo yule dada machozi yakaanza kumlenga na kunieleza haya;

Kwamba huyo mtoto pamoja na kuwa na hali hiyo baba yake hata hana habari nae,baba yake ni fundi ujenzi mzuri na huwa anasafiri kwenda kufanya kazi anaweza kukaa huko na miezi mitatu au minne ,lakini hata akiambiwa mtoto amezidiwa anaumwa huwa hashtuki hata kusema atafute muda kuja kumuona, hataki,huwa anasema tu atakuja na hata akiomba atumiwe hela ya matibabu hatumi,akaendelea..

Unaweza ukasema hana muda sawa,lakini hata akiwepo mtoto anaweza kuwa anaumwa usiku na anatapika hapo yeye wala hashtuki wala kuamka mama yake ndio anahangaika,hata kumpeleka hospitali hataki,sasa anajiuliza huyu ni mtu gani asiye na utu?.Pia huwa akiambiwa atume hela mtoto akatibiwe hatumi, unaweza kusema hana hela lakini anasema si kweli kwa sababu Jumamos iliyopita alituma 50,000 za matumizi lakini,akamjaribu tu kumwambia sasahivi kuna baridi atume hela anunulie watoto wadogo masweta(wana watoto watatu,huyu mgonjwa ndio mkubwa yupo darasa la 5)Jana hiohio akatuma 40,000 sasa anajiuliza kwanini huyu mwingine huwa hamjali?

Pia anasema tangu mtoto huyo awe kwenye hali hio huyu baba mtu mambo yake yananyooka tu na hela sikuhizi kwake sio tatizo ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Anasema anahisi huyu baba ameamua kumfanya mtoto wake ndondocha ili apate pesa kama kabila la( )analitaja wanavyofanya ili kupata utajiri hivyo akaamua aende kwa 'mtaalam' ambapo aliona kwenye kioo jinsi baba wa mtoto alivyofanya kumtoa mwanae ili apate mafanikio na hivyo akawa amethibitisha wasiwasi wake.

Cha kushangaza baada ya kutoka huko kwa Sangoma mume wake alimpigia simu akamwambia ameona alipoenda na aache kumfuatilia maisha yake ,akasema walifokeana sana siku hio.

Huyu dada anaumia sana juu ya hili maana mtoto anateseka sana,akienda shule analala tu na kuna muda mtoto anamwambia mama mbona mimi nateseka sana ,siko kama wenzangu ni bora nife tu niondoke duniani,na anasema kuna muda anamsimulia jinsi anavyofuatwa na watu usiku wanamlazimisha kunywa damu za watu.

Sasa mimi najiuliza hivi mtu unasikia raha gani kutumia pesa ambayo inatokana na kumuua au kumharibu mtoto wako?hivi unapata amani kabisa moyoni?Mimi nadhani tunatafuta Mali ili familia ziishi kwa raha na amani?

Wanaume tuache tamaa mbaya mpaka za kufikia kuwatoa kafara watoto wetu,wazazi au wanafamilia kwa tamaa ya pesa,sijui kama wanawake nao wanafanya haya.Inasikitisha sana.

Mwisho nilimpa ushauri tu kama atauzingatia huyo mtoto atapona vizuri lakini kama atachelewa huyo mtoto atakuwa zezeta jumla au kumpoteza kabisa maana hali aliyofikia sasa anasema hata kula hali na kuna muda haongei kabisa anakuwa kimya tu.

Kisa cha Pili;

Kuna Dada mmoja aliolewa na akazaa watoto watatu na Mme wake baadae wakaachana watoto wakiwa bado wadogo,mwanamke akabaki na watoto bila msaada wa mume lakini alijitahidi akawasomesha mpaka yule mkubwa akamaliza sekondari akampekeka chuo fulani cha mambo ya Afya.

Akiwa mwaka wa mwisho chuoni, mtoto akaaga kwamba anaenda kurudia baadhi ya masomo aliyofeli baada ya hapo simu yake ikawa haipokelewi, baada ya kuendelea kupiga mfululizo kama siku tatu hivi simu ikapokelewa na Mama mmoja aliyejibu kwamba 'Kijana hajambo ila wamepumzika baada ya maombi ya usiku kucha,wamechoka sana,Mama akashangaa sana,alipouliza yeye nani na hapo ni wapi hakusema ila akasema tu huyo mtoto yupo pale amepelekwa kwa ajili ya mafunzo ya unabii simu ikakatwa, Mama akachanganyikiwa, alipompigia baba yake hakupatikana hata hivyo anasema baba yake hawajawasiliana siku nyingi na hata mtoto haishi kwake kwahio hakumtilia maanani sana.

Siku ya pili akapiga tena simu ikaita na kupokelewa na mtu yuleyule na majibu walikuwa ni Yale yale, baadae ikawa haipatikani kabisa, siku ya tatu anapokea mtoto ila alipoulizwa uko wapi na kwanini hupokei simu, akajibu nipo nasomea Unabii alipotakiwa kuondoka hapo haraka akasema hawezi kuondoka mpaka amalize mafunzo na kwamba atarudi mwezi fulani,simu ikakatwa haikupatikana tena.

Hapo mama akachanganyikiwa na ikabidi ahusishe polisi,baada ya kuanza kuifuatilia namba baadae alipatikana lakini inaonekana alishaondoka kwa yule mama kuepusha kukamatwa nadhani.

Baada ya mtoto kupatikana aliachana na mambo mengine lakini uchunguzi ulibaini kwamba pale alipelekwa na baba yake malengo aliyoambiwa ni kujifunza unabii lakini haikuwa hivyo kwani yule mama walikuwa ni Mganga ambaye huyo Mme wake amekuwa akimtumia kufanya mambo yake yakae sawa.

Hata hivyo akili ya kijana ilishatetereka tayari na kuna muda anaongea mwenyewe na kufanya ishara za vidole zisizieleweka hivyo ufahamu wake haukuwa vizuri na hivyo yaliyofanyika huko hakuweza kuniju hasa ni nini walikuwa wanafanya.

Baada ya kufuatilia sana ikaonekana huyo Bwana alimpekeka pale ili kumtoa kafara kwa ajili ya kujipatia mali, hivyo angechelewa hali ingekuwa mbaya zaidi.

Mpaka sasa Mama anahangaika na mtoto ili akae sawa, mtoto ambaye amemhangaikia kwa taabu ili asome na sasa amefikia hatua ya mwisho baba anaamua kumtoa kafara ili apate mali.

Haya ni matukio mawili ya kusikitisha sana jinsi gani tamaa za Mali zimewashika wanaume na kuamua kuwatoa kafara au kuwaharibu watoto wao ili wao wafaidi mali, ni unyama wa hali ya juu.

Hivi pesa Chafu kama hizi zitakupeleka wapi kama sio kukaribisha laana kwako?hivi unapata usingizi kabisa au unakula chakula na unakifurahia huku unajua kabisa ni zao la kafara au maumivu ya mtoto wako?au ukimuona mwanao akiwa zezeta wewe moyoni mwao unajisikaje?

Wanawake chunguzeni sana,kuna wanaume wameingiwa na tamaa mbaya sana,wapo tayari kumwaga damu ya mtoto wake ili apate Mali.

Mungu atusaidie sana.
Utajiri una Siri nyingi mkuu,na Kama una roho nyepesi haya Mambo unatakiwa uwe unapita mbali .huyo jamaa binafsi sitaki kumsemea neno.ila Kuna wakati wanawake pia ni chanzo Cha wanaume kuamua kusaka utajiri kwa plan B.
 
hakuna excuse hapo, kumfanya mwanao ndondocha kisa utajiri hakuna aisee.

Hizo ni dalili za kushindwa tu maisha.
 
Mimi sijawahi kupata mtoto ambaye ni wangu na nikaacha kumpenda, ukimpenda mtoto wako hutaweza kufanya huo upuuzi
 
Back
Top Bottom