Naomba leo nisemezane na wanaume wenzangu………………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.

Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?
 
Nampa baraka zote na kumsindikiza airport..
Heeeh! Kumbe ni wanaume only?!
 
Siku hizi hawateui watu kwenda kusoma, lazima mhusika mwenyewe aoneshe nia ya kutaka kwenda kusoma. Na kwakuwa umewaamini kuwa ni watu wema na umewaachie wawe wanashinda na mkeo siku 6 kwa wiki na ofisi za mabosi ni safe contained. Kwenda nje si itakusaidia mzee kuongeza unga akishamaliza masomo? let her go vinginevyo uwe tayari kuachwa na kuchukiwa na koo zote mbili pamoja na ofisi yake kuwa wewe hupendi maendeleo yake
 
Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.

Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?

mbona mruhusu tu kwa roho safi ili niiishi kwa amani..
 
unamruhusu tatizo liko wapi? Wanaume muache ubinafsi.... Ingekuwa ni wewe mwanaume umepata nafasi hiyo mkeo angekupa baraka zote kwa nini wewe ujishauri?
 
Kwa mwanaume ambaye hajawahi kuishi ughaibuni anaweza kumruhusu kirahisi mkewe kwenda kusoma huko peke yake, lakini kwa aliyewahi kuishi ughaibuni inaweza kuwa ngumu kidogo, unless waende wote.
 
Kwa nini tuwe na mashaka mwanamke anapohitajika kwenda ugenini tu, na wakati tunawaacha wanawake hao hao nyumbani tz tunakwenda kubeba mabox ughaibuni kwa miaka mingi tu? Au hapa nyumbani tz hakuna vishawishi? Tuache wivu usio na maana ambao matokeo yake ni kurudisha maendeleo ya familia zetu nyuma.
 
Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.

Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?
Inategemea mpo kwenye stage gani kwenye ndoa.
Kwa ndoa changa inakuwa ngumu kidogo na inaumiza....but kwa sisi vikongwe wala hata hujiulizi mara mbili...hata asiporudi sawa tu!!
 
Back
Top Bottom