Naomba leo nisemezane na wanaume wenzangu………………!

Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.

Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?

Hapa kaka yangu Mtambuzi lazima itegemee!. Kuna mambo ya kuangaliwa hapa mfano watoto kama wapo itakuwaje? ataenda nao au watabaki na mimi na pia wana umri gani!. Kiujumla kwenye Ndoa hakuna anayependa kuwa mbali na mtu wake kwa umbali huo na kwa muda huo of course ndio maana ya kuoana, lakini yako mazingira ambamo lazima tuangalie 'opportunity costs' yaani ili upate hiki lazima ukose kile na hili upate kile lazima ukose hiki na hauwezi kuvipata vyote kwa pamoja.
Kwa sababu kila ndoa ni 'unique' na ni vigumu kusemea ndoa za watu wengine. Binafsi yangu kama nilivyosema hapo juu 'nitamruhusu' lakini prior to the mazingira yatakavyoruhusu!
 
Maswali mengine yanafikirisha sana na ni muhimu watu kuwa na majibu kabla halijakukuta! well - miaka miwili? mmh
 
Kiukweli itauma,maana unaweza kwenda kumpokea eapoti next likizo ukamwona ana mtoto wa kisomali!
 
Hapa kaka yangu Mtambuzi lazima itegemee!. Kuna mambo ya kuangaliwa hapa mfano watoto kama wapo itakuwaje? ataenda nao au watabaki na mimi na pia wana umri gani!. Kiujumla kwenye Ndoa hakuna anayependa kuwa mbali na mtu wake kwa umbali huo na kwa muda huo of course ndio maana ya kuoana, lakini yako mazingira ambamo lazima tuangalie 'opportunity costs' yaani ili upate hiki lazima ukose kile na hili upate kile lazima ukose hiki na hauwezi kuvipata vyote kwa pamoja.
Kwa sababu kila ndoa ni 'unique' na ni vigumu kusemea ndoa za watu wengine. Binafsi yangu kama nilivyosema hapo juu 'nitamruhusu' lakini prior to the mazingira yatakavyoruhusu!

Mkuu nakubaliana na maoni yako, lakini hebu tufanye ni mchumba na mko kwenye michakato ya kufunga ndoa au ndio mmefunga ndoa mwaka mmoja uliopita (Na Ndoa bado haijajibu) halafu anapata hiyo nafasi ya kwenda ughaibuni kuongeza ilmu, na wewe ni mwajiriwa ukiwa na nafasi ya kawaida tu...........Hii ina maana kwamba akirudi cheo kitapanda na responsibility zitaongezeka lakini pia atakuzidi kipato.......... Hebu niambie hapo unachukua uamuzi gani?

Mbona ishu nyepesi sana? Siyo tu namruhusu bali pia nampongeza na kumsindikiza eapoti kuhakikisha pipa alilopanda limetokomea mawinguni..... Freedom is coming tomorrow! Source: sarafina
 
Piga mimba kabisa aende nayo huko.Kitu muhimu sana hii mkuu
wanagonga na mimba yake, kwani inang'ata?? mi wakati nna mimba yangu, kuna mshkaji ofisini na kulia alikuwa analia kwamba ye ugonjwa wake ni pregnant women, yaani yupo radhi kufanya chochote!! we dunia hii watu wamedata usisikie kabisa!
 
Mama Ngedule aliwahi kufanya kazi kwenye kambi ya BENACO huko Ngara kisha akahamia Kigali Rwanda, nilikaa naye mbali miaka mitatu wakati ndoa yetu bado ilikuwa changa na mtoto tulikuwa hatujapata ...........Three Years na sikufa itakuwa ni huko Ughaibuni? Ajiendee tu mie nitalea wanangu
 
ishu sio kusoma miaka miwili
ishu ni kuonana wewe na yeye ni vipi?
myu anaweza kusoma hata miaka mitano
lakini ukawa unakwenda kumuona kila mara
toauti na kuonana mara moja kwa mwaka

halafu fimbo iliyo mbali....................
 
Akasome tu lakin kila miezi mitatu lazima umfate ukapige vitu vya kihalali, mana ukiwacha sana inakuwa nayo noma...ile kitu inaweza kukusahau.

Inabidi uwe unaruka ruka kila wakat, mfanoi kazini wakikunyima ruhusa unajifanya mgonjwa unatibiwa kienyeji haitaki sijui a sick leave certificate au nini.
 
Mkuu nakubaliana na maoni yako, lakini hebu tufanye ni mchumba na mko kwenye michakato ya kufunga ndoa au ndio mmefunga ndoa mwaka mmoja uliopita (Na Ndoa bado haijajibu) halafu anapata hiyo nafasi ya kwenda ughaibuni kuongeza ilmu, na wewe ni mwajiriwa ukiwa na nafasi ya kawaida tu...........Hii ina maana kwamba akirudi cheo kitapanda na responsibility zitaongezeka lakini pia atakuzidi kipato.......... Hebu niambie hapo unachukua uamuzi gani?

Kwa hali hii, itakuwa ngumu sana kumruhusu aende. Tutatafuta mafanikio ya maisha kwa namna nyingine.:lock1:
 
Mimi ni marufuku katika ndoa yangu kukaa mbali na waifu zaidi ya miezi miwili, achilia mbali kusoma hata kama anapatiwa ajira ya kutandika kitanda cha Obama marekani kama ni nje ya hiyo katiba hapo juu ni marufuku.

Nazani nimeeleweka.
Maandiko yamehimiza tuishi na kinamama kwa machale na ze boss amegusia hapo juu,
far stick never kill snake.

Nimemaliza
 
Back
Top Bottom