Naomba kujuzwa Mikoa yenye hali nzuri ya hewa

Songea hakuna Baridi wala hakuna Joto mvua za kutosha ukilima na kufuata taratibu za kilimo kupata ni 100%
 
Mara ni kuzuri especially huku kwa wakurya Tarime. Karibu tuishi. Hali ya hewa nzuri, watu wakarimu (kama hujawachokoza au hujala cha watu), mazao karibu yote yanastawi, wana misimu miwili ya kulima kwahiyo hakuna njaa ya chakula wala matunda. Hela iko nje ya mlango wako ni wewe tu kupambana kuitafuta.
Haswaa,hususani Mogabiri kwenda Nyantira,Nyanungu,Magoto,Kimusi,Nyansincha,Muriba.Nyarero, Nyandoto hadi Sirari hapo ata furahia
 
Anayetaja Kilimanjaro kwa hali ya hewa nzuri ni dhahiri haijui au amekairirishwa tu, ni sehemu chache zenye hali ya hewa nzuri lakini sehemu kubwa joto linaandama sana huu mkoa kwa miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani mfno, ukienda baadhi ya sehemu za moshi vijijini kama Himo, ukienda huko Sia, Hai na Mwanga kuna sehwmu unaweza kusema niko kwenye Jangwa la Kalahar, lakini ukienda sehemu kama Marangu, Rombo (ukanda wa juu) na baadhi ya maeneo hali ya hewa safi sana. Kagera ni wilaya ya Biharamulo ndo yeye hali ya hewa ambayo ni joto zaidi na jua kali sana, lakini wilaya zingine kama Ngara, Muleba, Missenyi, Bukoba, Karagwe hali ya hewa ni nzuri, mkoa wa Mbeya na Iringa hali ya hewa ni nzuri kwa maeneo mengi. Tanga kuna maeneo mazuri pia. Arusha maeneo machache sana yenye hali ya hewa nzuri hasa mjini lakini kwingine ukame ni mkubwa sana. Huko Njombe maeneo mengi mazuri kwa ubaridi. Nilichogundua humu JF watu wengi wanakariri kwa kutumia taarifa za miaka mingi iliyopita hawajui kuwa hali ya hewa inabadirika kila uchao. Mfno sasa hivi ukienda Moshi Mjini unaweza kudhani uko kwenye Jangwa la Namib, dk hii ukienda Songwe baadhi ya maeneo utakimbia, ukienda Biharamulo Kagera hakika utadhini uko jangwani pia kwa baadhi ya maeneo. Ukifika Tukuyu Mbeya hali ya hewa safi sana. Ningetamani niwashauri vijana wa JF ukipata sehemu ya kutembelea mkoa fulani usiishie mjini ikiwezekana zama hadi vijijini ndani ndani na wilaya za pembezoni ndipo ujue hali halisi ya eneo husika. Naomba kukosolewa kama kuna sehemu nimekosea.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom