Kaka ni swala la muda tu utakuja kuelewa maandiko na misingi sahihi ya Ukristo,
Hao wakatoliki ndio waliokuwa na hiyo Biblia unayotamba nayo sasa, wao wangeamua wangeweza kufanya chochote na kuharibu hayo maandiko, lakini hawakufanya hivyo, ila waliotoka ndani ya Ukatoliki ndio wakaanza kutoa baadhi ya vitabu, ukae ukijua katika vitabu alivyovipunguza Martin Luther hata Kitabu cha Jakobo na Ufunuo alivitoa na kisha kuvirudisha baadae
Hoja yangu ni kuwa, Wakatoliki huwa hawakurupuki na huwa wanaitafsiri Biblia kwa kina kirefu ambacho madhehebu mengine inawachukua miaka kuiona hiyo kweli
Ulokole ulipoanza hasa hapa Tanzania, walikuwa na Biblia tu lakini siku zimeenda na wameanza kurudi kwenye Ukatoliki kwa mlango wa nyuma, Ilikuwa si rahisi kwa Mlokole kumkuta na Mafuta, Maji, Nguo na vitu vingine vikiwa kama silaha ya maombezi, kwa Ukatoliki ni vitu vya kawaida kwa walokole haikuwa kawaida
Wakatoliki wanaamini Yesu ni Mungu, kama Aliombwa kufanya vitu fulani na akavifanya inakuwaje sasa akiombwa asiweze kufanya?