Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Naomba kujuzwa kwanini marehemu anaombewa?

Kawaida kuna mahala inakua inakwenda ila maskani yake ni pale kwenye kaburi mpaka utafufuliwa ama kaburi lihame pale lipelekwe sehemu nyengine
 
Kwa kiokua na elimu ya roho walikua wakiweza kuisemesha na kupata majibu
 
Ibada inapaswa kuwa ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya huyo mtu hapa duniani na kuifariji familia huku ikitukumbusha tuluobakia jukumu letu la kumtumikia Mungu

Kumuomba Mungu amsamehe marehemu huo ni wendawazimu. Ukristo unasema wazi kutubu ukiwa hai, ukishakufa hakuna namna yoyote ya kupunguza adhabu ya Mungu kwako

Makanisa hasa RC (ambalo mimi naabudu) sijui wanatoa wapi huu utaratibu wa kuwaombea marehemu ndani ya vitabu vya Mungu
Ulishawahi kuisoma biblia ya kikatoliki?Huko ndiko justification ya kuombea marehemu inatoka
 
Kwenye Ukristo wa Kiprotestant hakuna maana yoyote ya kumuombea mtu akiwa amefariki maana Biblia inakataza kabisa ibada za wafu.

Ila ibada ile ya siku ya msiba ni kwa ajili ya kuwafariji tu na kuwakumbusha wanadamu umuhimu wa kumkumbuka Mungu kabla ya umauti ndio maana huwa yanasisitiswa mahubiri zaidi kuliko sala.

Ibada ile siku ya msiba ni muhimu kwa sababu kubwa kwamba ni kipindi kigumu sana kwa wafiwa kuondokewa na mtu wa karibu(kama umeshawahi kufiwa utalijua hili) na jamii ya kiroho inabidi iwe karibu sana na wafiwa.

Jambo jingine nafikiri ni busara tu ya viongozi wa kidini kuzuia mabalaa yanayoambatana na misiba, kwa maana misiba hutumiwa sana na washirikina kufanya mambo yao mazito kwa waliobaki, lakini pia kupenyeza imani zao za kishirkikina.

Ibada ya Kimungu isipofanyika hupelekea watu waliofiwa kugeukia upande mwingine wa kishetani kufanya matambiko na matambiko ya misibani huwa yana nguvu sana kufunga hata vizazi vinne alivyoviacha marehemu.

Binafsi naunga mkono ibada hizi siku za misiba, japo si katika kuwaombea waliokufa wasamehewe dhambi au kupunguziwa adhabu, ila kwa ajili ya kuwalinda hawa waliobaki kiroho, maana zisipofanyika shetani ata-take advantage na matambiko lazima yatafanyika tu.
Wakatoliki wanapenda kishenzi kuombea wafu. Wote waende mbinguni, irrespective of their sins before death.
 
Wakatoliki wanapenda kishenzi kuombea wafu. Wote waende mbinguni, irrespective of their sins before death.
Unawezaje kuyajua nahusiano ya mtu na Mungu wake kabla hajafa??? Kwann nini unahukumu...?Kasome Mhubiri 7:12
Roho haifi, kinachokufa ni mwili...kinachoombewa ni roho ya marehemu

Ahsanta
 
Back
Top Bottom